Thursday, November 20, 2014

Serikali kutoajiri wahitimu wa vyuo visivyosajiliwa.

Waziri wa nchi ofisi ya Rais, Menejiment ya Utumishi wa Umma,Celina Kombani, akizungumza kwenye mahafali ya 20 ya chuo cha uhazili Tanzania mjini Singida. Kombani aliwaasa wahitimu hao 4,960, kwamba wasiridhike na elimu waliyopata, bali waongeze bidii zaidi katika kujiendeleza.
Kaimu Mkuu wa mkoa wa Singida na mkuu wa wilaya ya Singida, Queen Mlozi, akizungumza kwenye mahafali ya 20 ya chuo cha uhazili Tanzania yaliyofanyika mjini Singida. Jumla ya wahitimu 4,960 walitunukiwa vyeti vya fani mbalimbali.

Serikali yaonya ubadhilifu wa wahitimu.

Wahitimu 1,808 wa fani mbalimbali wa vyuo vya uhasibu tawi la Mwanza na Singida, wakiwa kwenye maandamano ikiwa ni sehemu ya mahafali yao ya 12 yaliyofanyika mjini Singida.

Naibu Waziri wa Fedha, Mh. Mwigullu Lameck Nchemba, akizungumza kwenye mahafali ya 12 ya tawi la Mwanza na Singida, yaliyofanyika katika viwanja vya chuo cha uhasibu mjini Singida. Mwigulu aliwaasa wahitimu hao waweke mbele uadilifu,uaminifu na kuchapa kazi kwa bidii na maarifa ili kujijengea mazingira ya kuaminika mbele ya jamii.

Katibu tawala Singida ataka mikakati kuwekwa kuongeza wakulima wanaotumia mbegu bora.

Katibu Tawala mkoa wa Singida, Liana Hassan, akizungumza kwenye ufunguzi wa semina juu ya kuongeza upatikanaji wa mbegu bora na mbolea kwa wakulima wadogo wadogo kwa kuimarisha masoko ya pembejeo katika mikoa ya Singida na Dodoma.
Baadhi ya wakulima wadogo wadogo mkoa wa Singida na Dodoma,wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa kwenye semina ya siku mbili iliyohusu kuongeza upatikanaji wa mbegu bora na mbolea.

Agizo la kukabidhi vyumba vya maabara kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida bado kutekelezwa.

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari kata ya Ikungi wilayani Ikungi mkoa wa Singida,wakishiriki ujenzi wa vyumba vitatu vya maabara jana kama walivyokutwa na mpiga picha wetu. Mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Vicent Kone, aliagiza akabidhiwe vyumba vitatu vya maabara kwa kila shule ya sekondari 153 za kata za mkoa huo kabla ya oktoba 15 mwaka huu.Mambo yamekuwa tofauti kwa shule ya sekondari ya kata ya Ikungi ambayo hadi sasa bado ujenzi upo ngazi ya msingi.

135 wafa katika ajali Singida.

Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Singida, ACP, Thobias Sedoyeka ,akitoa taarifa ya utendaji kazi mkoani Singida kwa kipindi cha kuanzia Januari hadi Septemba mwaka huu.

Baadhi ya waandishi wa habari na askari polisi waliohudhuria hafla ya kamanda wa polisi mkoa wa Singida kwa ajili ya kutoa taarifa ya utendaji kazi kwa kipindi cha miezi tisa.

Halmashauri ya Ikungi yakusanya zaidi ya shilingi billion 2 ndani ya miezi 3 kutoka vyanzo mbalimbali vya mapato.

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida, Celestine Yunde, akizungumza kwenye kikao cha kawaida cha baraza la madiwani.Kulia ni makwamu mwenyekiti, Ali Mwanga na wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ikungi,Hassan Tanti na anayefuatia ni Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri wilaya Ikungi, Mahammud Nkya.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi, Mahammud Nkya, akitoa taarifa yake mbele ya kikao cha kawaida cha baraza la madiwani kilichofanyika Ikungi. Kulia ni mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Ikungi, Celestine Yunde na kushoto ni mwenyekiti CCM wilaya ya Ikungi, HassanTanti.

Picha za tukio la kuuwawa kwa Fisi mjini Singida ziko hapa!

Baadhi ya askari polisi wakishiriki kumtoa Fisi ambaye alikuwa amejificha ndani ya duka la mitumba mjini Singida.
Baadhi ya wananchi wa mji wa Singida wakishuhudia kutolewa nje Fisi aliyekuwa amejificha ndani ya duka la mitumba mjini Singida.