Friday, September 16, 2011

LATEST UPDATES: CHANZO CHA KUUNGUA KWA SOKO KUU LA SIDO MWANJELWA MBEYA CHAFAHAMIKA


ASUBUHI YA LEO TAREHE 16.09.2011 NCHI IMEINGIA KATIKA JANGA LENGINE AMBAPO SOKO KUU JIPYA LA SIDO MWANJELWA MKOANI MBEYA LILITEKETEA KWA MOTO MAJIRA YA SAA 9:50AM ASUBUHI, MOTO HUO AMBAO ULISIMAMA UKIWAKA KWA MUDA WA MASAA MAWILI BILA KUZIMIKA NA KUSABABISHA UHARIBIFU NA KUPOTEZA MALI ZA WATU WENGI. IKIWA NI MIAKA MICHACHE TUU KUPITA BAADA YA WAFANYA BIASHARA HAO KUPATA PIGO KUBWA BAADA YA SOKO KUU LA MWANJELWA KUUNGUA MOTO NA KUWALAZIMU WAANZE UPYA BIASHARA ZAO.


HABARI ZAIDI ZINASEMA BAADA YA MOTO HUO KUANZA ILICHUKUA MASAA MAWILI MPAKA MAGARI YA ZIMA MOTO KUFIKA NA KUANZA KAZI YA KUSAIDIA KUZIMA MOTO HUO AMBAPO WALIKUWA WAMECHELEWA HIVYO KUZIDI KUSABABISHA UPOTEVU WA MALI ZA WENYE MADUKA.


JESHI LA POLISI WAKISHIRIKIANA NA JWTZ PAMOJA NA MIGAMBO WALIKUA KATIKA ENEO HILO KUHAKIKISHA USALAMA KUTOKANA NA KUWA NA VIBAKA WENGI AMBAO WALIPATA NAFASI YA KUIBA MALI ZA WANANCHI.


KATIKA TUKIO HILO LA MOTO KUCHOMA SOKO LA SIDO MWANJELWA MBEYA BAADHI YA MAMBO YALITOKEA IKIWA NI PAMOJA NA MTU MMOJA KUGONGWA NA GARI ALIPO KUWA ANAJARIBU KWENDA KUOKOA MALI ZA WAFANYA BIASHARA HAO, PIA KULIKUWA KUNA MFANYA BIASHARA ALIKUA ANAZUIDA DUKA LAKE ILI WEZI WASIIBE KATIKA DUKA LAKE NA KUUNGUA KWA MOTO, INAHOFIWA HUYO NDIE MTU PEKEE AMEPOTEZA MAISHA KATIKA TUKIO HILO. PIA INARIPOTIWA KUWA KUNA MAMA MJAMZITO AMBAE ALIPATWA NA UCHUNGU NA KUTAKA KUJIFUNGUA KATIKA ENEO LA TUKIO LAKINI WASAMALIA WEMA WALIMWOKOA NA KUJIFUNGUA SALAMA.


WANANCHI WASIO NA MEMA AMBAO WAKATI JESHI LA POLISI LILIKUWA LIKIJARIBU KUWASAIDIA WATU, WANANCHI HAO WALIANZA KUPIGA MAWE MAGARI HAYO YA POLISI NA PIA KUWATUPIA MAWE MAPOLISI HATA HIVYO MAPOLISI HAO WALIFANIKIWA KUWASHINDA BAADA YA KUWATUPIA MABOMU YA MACHOZI.


AKIZUNGUMZA NA MMOJA WA WAFANYA BIASHARA JINA LAKE ANAITWA GODEN MWAKALINGA ALIELEZA KUWA CHANZO CHA MOTO HUO KILITOKANA NA HITILAFU YA UMEME KATIKA KIBANDA CHA BIASHARA CHA BWANA GHALIFA NA KUSABABISHA MOTO HUO KUWAKA NA KUSABABISHA HASARA KUBWA KATIKA SOKO HILO KUU LA SIDO MWANJELWA MBEYA

HABARI MPASUKO : SOKO LA MWANJELWA KIWANJA CHA SIDO LAWAKA MOTO

Soko la mwanjelwa eneo la sido mbeya lawaka moto chanzo mapaka sasa hakijajulikana

Baadhi ya mabanda sokono hapo tayari yameteketea kabisa na moto


Kufa kufaana kibaka tayari ameshaiba huyooo anatimka

Dada nae hayuko nyuma katika wizi keshachukua kapeti


Mama huyu akilia kwa uchungu akiangalia duka lake likiteketea kwa moto


Hii ni hatari

RAIS KIKWETE ATEUA WAKUU WA MIKOA WAPYA.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


RAIS KIKWETE ATEUA WAKUU WA MIKOA WAPYA


RAIS Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko ya Wakuu wa Mikoa nchini.


Katika mabadiliko hayo, amewateua Wakuu wa Mikoa wapya 15, kuwabadilisha vituo vya kazi Wakuu wa Mikoa watano na wengine saba wamestaafu kwa mujibu wa taratibu. Mkuu wa Mkoa wa Singida amebaki kwenye kituo chake cha kazi wakati Wakuu wa Mikoa wengine wanne watapangiwa kazi nyingine.


Aidha, Wakuu wa Mikoa mipya minne ya Simiyu, Geita, Katavi na Njombe itakayoundwa baada ya taratibu kukamilika watatangazwa baadaye.


Kwa mujibu wa mabadiliko hayo, Wakuu wa Wilaya 11 wamepandishwa Vyeo na kuwa Wakuu wa Mikoa kama ifuatavyo: Bw. John Gabriel Tupa ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara; Bw. Saidi Thabit Mwambungu (Ruvuma); Bi. Chiku S. Gallawa (Tanga); Bw. Leonidas T. Gama (Kilimanjaro); Dk. Rehema Nchimbi (Dodoma); Bw. Elaston Mbwillo (Manyara); Kanali Fabian Massawe (Kagera); na Bibi. Fatma Abubakar Mwassa (Tabora). Wakuu wa Wilaya wengine walioteuliwa ni Bw. Ali Nassoro Rufunga, (Lindi); Eng. Ernest Welle Ndikillo, (Mwanza); na Bw. Magesa Stanslaus Mulongo Mkuu wa Mkoa (Arusha).


Walioteuliwa nje ya nafasi hizo ni Eng. Stella Manyanya (Rukwa); Bibi Mwantumu Mahiza, (Pwani); Bw. Joel Nkaya Bendera (Morogoro) na Bw. Ludovick Mwananzila (Shinyanga).


Waliobadilishwa vituo vya kazi ni Bw. Abbas Kandoro anayekwenda Mbeya akitokea Mwanza; Bw. Said Mecki Sadiki anayekwenda Dar es Salaam akitokea Lindi; Bibi Christine Ishengoma anayekwenda Iringa akitokea Ruvuma; Lt. Kanali Issa Machibya anayekwenda Kigoma akitokea Morogoro; na Kanali Joseph Simbakalia anayekwenda Mtwara akitokea Kigoma. Dk. Parseko Ole Kone ataendelea kuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida.


Waliostaafu ni Bw. Mohammed Babu, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera; Bw. Isidore Shirima aliyekuwa Arusha; Kanali (mst.) Anatory Tarimo aliyekuwa Mtwara; Bw. John Mwakipesile, aliyekuwa Mbeya. Wengine ni Kanali Enos Mfuru aliyekuwa Mara; Brig. Jen. Dk. Johanes Balele aliyekuwa Shinyanga; na Meja Jen. Mst. Said S. Kalembo aliyekuwa Tanga.


Wakuu wa Mikoa wanne waliostaafu ambao watapangiwa vituo vingine vya kazi ni Bibi Amina Mrisho aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani; Dk. James Msekela aliyekuwa Dodoma; Bw. Abeid Mwinyimusa aliyekuwa Tabora na Bw. Daniel Ole Njoolay aliyekuwa Rukwa.


Wakuu wote wa Mikoa waliopo sasa wameagizwa kuandaa Hati za Makabidhiano (Handing Over Notes) katika muda wa siku 14 kuanzia siku ya kuapishwa kwa Wakuu wapya wa Mikoa. Aidha Wakuu wa Wilaya ambao wamepandishwa vyeo kuwa Wakuu wa Mikoa nao wanapaswa kufanya hivyo hivyo kwa ajili ya Wakuu wa Wilaya watakaopangiwa vituo vitakavyokuwa vimeachwa wazi kutokana na uteuzi wao.


Wakuu wa Mikoa ile minne mipya na Wakuu wa Wilaya watakaoteuliwa hapo baadaye nao watatakiwa kuandaa Hati za Makabidhiano ndani ya siku 14 tangu kuapishwa.


Makabidhiano hayo lazima yahusishe pia kutembelea kwa pamoja baadhi ya maeneo na miradi ambayo ni muhimu kama sehemu ya makabidhiano yao.
Wakuu wote wa Mikoa walioteuliwa na Wakuu wa Mikoa minne mipya wakaoteuliwa pamoja na Wakuu wote wa Wilaya watakaoteuliwa baada ya zoezi kukamilika watatakiwa kuhudhuria mafunzo ya wiki tatu kwenye Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Dodoma kwa lengo la kuwajengea uwezo zaidi wa kiuongozi na kiutendaji.


Wakuu hao wapya wa mikoa wataapishwa siku ya Ijumaa, Septemba 16, 2011 saa 4.00 asubuhi kwenye viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.


Wakuu hao wapya wa mikoa; vituo wanavyokwenda na vituo walivyotoka ni kama ifuatavyo:


Na. JINA LA MKUU WA MKOA KITUO AENDAKO KITUO ATOKAKO
1. Bw. Saidi Mecki Sadiki DAR ES SALAAM RC - Lindi
2. Bw. John Gabriel Tupa MARA DC - Dodoma
3. Bw. Saidi Thabit Mwambungu RUVUMA DC - Morogoro
4. Kanali Joseph Simbakalia MTWARA RC Kigoma
5. Bi. Chiku S. Gallawa TANGA DC - Temeke
6. Bw. Abbas Kandoro MBEYA RC Mwanza
7. Bw. Leonidas T. Gama KILIMANJARO DC – Ilala
8. Dkt. Parseko Ole Kone SINGIDA RC Singida
9. Eng. Stella Manyanya RUKWA Mbunge V/Maalum
10. Bibi Christine Ishengoma IRINGA RC Ruvuma
11. Dk. Rehema Nchimbi DODOMA DC - Newala
12. Bw. Elaston John Mbwillo MANYARA DC – Mtwara
13. Col. Fabian I. Massawe KAGERA DC - Karagwe
14. Bibi. Mwantumu Mahiza PWANI Mbunge/NW Mstaafu
15. Bibi. Fatma A. Mwassa TABORA DC - Mvomero
16. Bw. Ali Nassoro Rufunga LINDI DC - Manyoni
17. Eng. Ernest Welle Ndikillo MWANZA DC - Kilombero
18. Lt. Col. Issa Machibya KIGOMA RC Morogoro
19. Bw. Magesa S. Mulongo ARUSHA DC - Bagamoyo
20. Bw. Joel Nkaya Bendera MOROGORO Mbunge/NW Mstaafu
21. Bw. Ludovick Mwananzila SHINYANGA Mbunge/NW Mstaafu







IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 3021,
DAR ES SALAAM
JUMATANO, SEPTEMBA 14, 2011.

TATIZO LA KUKOSEKANA KWA UMEME KATIKA KIWANJA CHA NDEGE CHA KIMATAIFA CHA JULIUS NYERERE USIKU WA TAREHE 10 SEPTEMBER, 2011


Usiku wa Jumamosi tarehe 10 Septemba, 2011 kulitokea hitilafu ya kiufundi ya umeme katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere hali iliyosababisha kuvurugika kwa ratiba za ndege kadhaa ambazo wakati huo zilipaswa kuruka au kutua katika kiwanja hicho


Kutokana na hitilafu hiyo baadhi ya ndege zililazimika kuahirisha safari zao kwa kushindwa kuruka na nyingine ziililazimika kutua katika viwanja vingine vya jirani kama vile Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Kilimanjaro, Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Zanzibar na Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Jomo Kenyatta nchini Kenya.


Mamlaka ya Viwanja vya Ndege inapenda kutoa ufafanuzi wa kuhusu chanzo cha tatizo hilo na hatua zilizochukuliwa kama ifuatavyo:


Chanzo cha tatizo hilo la kiufundi ni kushindwa kufanyakazi kwa mfumo wa mitambo unaotenganisha umeme unaofuliwa na jenereta za dharula kuruhusu matumizi ya umeme wa TANESCO. Hali hii ilipelekea kiwanja kuendelea kutumia jenereta za dharula hadi tatizo hilo liliporekebishwa asubuhi ya jumapili tarehe 11/09/2011 kwa ushirikiano wa wataalam wa TAA na TANESCO.


Wakati kukiwa na tatizo hilo katika mfumo wa mitambo ya kutenganisha matumizi ya umeme kulijitokeza hitilafu nyingine ya kuzimika kwa taa katika njia ya kurukia na kutua ndege na hivyo kushindikana kwa ndege kutua au kuruka kwa kipindi chote hicho.




Kufuatia hali hiyo wahandisi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege waliweza kufanya matengenezo ya mfumo huo wa umeme na Mnamo saa 7.30 usiku wa manane wataalam hao waliweza kufanikiwa kurudisha umeme kiwanjani hapo na kufanya baadhi ya ndege kuruka na kutua. Matengenezo kamili ya mfumo huo yalikamilika siku ya Jumapili, tarehe 11 Septemba, 2011. Kwa sasa shughuli za uendeshaji kiwanjani hapo zimeendelea kama kawaida.


Kikundi kazi cha wataalam kimeshaundwa kufanyia kazi suala hilo kwa undani zaidi kwa lengo la kupata kiini cha tatizo hilo, kufanya tahmini ya athari ziliopatikana na pia kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa tatizo hilo kwa lengo la kuhakikisha kwamba halijitokezi tena.


Mamlaka ya viwanja vya ndege Tanzania inasikitika sana kwa usumbufu na hasara zilitokana na tatizo hilo na tunawaomba radhi wateja wetu wote , hususani mashirika ya ndege, abiria, wadau wote na wananchi kwa ujumla.


Mwisho tunapenda kuwahakikishia kuwa hitilafu hiyo ya umeme ambayo kwa bahati mbaya ilitokea kiwanjani hapo usiku huo wa kuamkia tarehe 11 Septemba, 2011 halina uhusiano wowote na tishio la kigaidi kama ambavyo baadhi ya watu walihusisha tatizo hilo na lile lililotokea nchini Marekani tarehe 11 Septemba, 2001. Tunawahakikishieni kuwa kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere kina ulinzi wa kutosha kuthibiti matukio kama hayo ya kigaidi.


Mhandisi. Suleiman S. Suleiman


KAIMU MKURUGENZI MKUU

MAITI ZINGINE TANO ZAPATIKANA MOMBASA,KENYA

NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR


Jumla ya maiti 202 tayari zimepatikana katika ajali ya Meli ya Mv.Spice Islander iliyotokea hivi karibuni huko Nungwi hadi hapo jana.


Maiti tano zaidi zilipatikana hapo jana sehemu ya Shimoni Mombasa Kenya ambapo maiti zote hizo zilizikwa huko huko Kenya kutokana na hali ya maiti zilivyo ambapo kabla ya jana maiti 197 zilikuwa zimepatikana.


Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mohammed Aboud Mohammed zilieleza kuwa aliwasiliana na Balozi mdogo wa Tanzania Nchini Kenya na kumthibitishia kwamba isingewezekana kuwasafirisha maiti hao kuwaleta Zanzibar kwa ajili ya kutambuliwa na jamaa zao kutokana na hali ilivyokuwa.


Amesema maiti hao mmoja inakadiriwa ni miaka minane, mwengine miaka 20 hadi 25 na wengine miaka 40 wote ni wanaume na mtoto mchanga mwanamke anakadiriwa na umri wa mwaka mmoja na nusu ambao wamepatikana katika kijiji cha Diani.


Kazi ya uokoaji bado inaendelea kwa ushirikiano mkubwa wa vikosi vya ulinzi na usalama, raia wa Tanzania pamoja na kikosi maalum cha Uokozi kutoka Afrika ya Kusini.


Wakati huo huo michango ya Rambi rambi inaendelea ambapo hapo jana Isnaashir imetoa jumla ya Shl. Milion 30, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wametoa shl. Milion 15 Wabunge wa Afrika Mashariki wamechangia Milion 2 na Benki ya NMB imekabidhi hundi ya Milion 20.


Fedha zote hizo zimekabidhiwa kwa Mwenyekiti wa Kamati ya maafa ya kitaifa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd ambaye pia ni Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar.


Shughuli za uchangiaji bado zinaendelea na wananchi pamoja na Taasisi mabalimbali za binafsi na Serikali zinaendelea kutoa michango yao.

Saturday, September 10, 2011

Just In : ABIRIA 250 WAOKOLEWA WAKIWA HAI KATIKA AJALI YA MELI YA SPICE ISLAND


Watu 250 wameokolewa wakiwa hai katika meli iliyozama ya Mv Spice Islanders iliyokuwa ikitokea Bandari ya Malindi Unguja kuelekea Bandari ya Wete Kisiwani Pemba.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais,Mohamed Aboud Mohamed amesema watu hao wameokolewa na Vikosi vya uokoaji na wananchi mbalimbali wanaotoa msaada wa uokozi katika tukio la kuzama kwa meli hiyo huko Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.


Waziri Aboud amesema watu hao wamesafirishwa kwa kutumia Boti zinazokwenda kasi za Zanzibar ambazo ilikwenda kutoa msaada katika eneo la tukio.


Amesema watu hao baada ya kufika Bandari ya Malindi Unguja watapelekwa Viwanja vya Maisara kwa ajili ya kuungana na familia na jamaa zao.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein yupo katika eneo la tukio huko Nungwi ili kujionea hali halisi ya tukio hilo.
Habari kwa hisani ya Michuzi Blog

Breeking newz: kuzama kwa meli ya spice islanders.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KUZAMA KWA MELI YA SPICE ISLANDERS


Usiku wa kuamkia leo Tarehe 10/09/2011 majira ya saa 9 za usiku kumetokea ajali ya kuzama kwa meli ya MV.SPICE ISLANDERS katika bahari ya eneo la Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.


Taarifa ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais,Mohamed Aboud Mohamed, imesema Meli hiyo ilikuwa ikitokea Unguja kuelekea Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba ambapo Meli hiyo ilikuwa imepakia mizigo na abiria.


Waziri Aboud amesema Serikali inaendelea na juhudi za kukitafuta chombo hicho pamoja na watu waliokuwemo.
Amesema kwamba Serikali tayari imeshatuma vyombo vya uokozi, ulinzi na usalama katika eneo la tukio na mtakuwa mkipewa taarifa mara kwa mara.


Waziri Aboud amewataka Wananchi kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu na tuendelee kusikiliza taarifa za Serikali kupitia vyombo vya habari ili kupata taarifa zaidi.


IMETOLEWA NA:-
IDARA YA HABARI(MAELEZO) ZANZIBAR
10/09/2011

Friday, September 9, 2011

President Jakaya Kikwete In Nairobi


MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AAGANA NA MABALOZI WA VATICAN NA JAPAN, IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Hiroshi Nakagawa, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu Dar es Salaam leo kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake nchini.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Hiroshi Nakagawa, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu Dar es Salaam leo, kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake nchini.
BALOZI WA VATCAN

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Balozi wa Vatican nchini Tanzania, Askofu Mkuu Joseph Chennoth, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu Dar es Salaam leo, kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake nchini. Balozi Chennoth amekaa nchini miaka sita.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Vatican nchini Tanzania, Askofu Mkuu Joseph Chennoth, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam leo.

Mama Salma Kikwete Atembelea Taasisi Ya UVIKIUTA Mbagala-Chamazi

Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete (kulia) akionyeshwa miche ya miti mbalimbali na Mwenyekiti wa Taasisi ya maendeleo ya vijana (UVIKIUTA)Ben Mongi (shati la kitenge)alipotembelea Sept.8.2011 na kuangalia shughuli mbalimbali za taasisi huko Mbagala-Chamazi Mkoani Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete akiwapa nasaha vijana wa UVIKIUTA huko Mbagala Charambe Wilaya Temeke Mkoa wa DSM Sept.8.2011 alipowatembelea. (kushoto) Mwenyekiti wa UVIKIUTA Ben Mongi.

Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete (kulia) akionyeshwa miche ya miti mbalimbali na Mwenyekiti wa Taasisi ya maendeleo ya vijana (UVIKIUTA) Ben Mongi (shati la kitenge) alipotembelea Sept.8.2011 na kuangalia shughuli mbalimbali za taasisi huko Mbagala-Chamazi Mkoani Dar es Salaam.

Baadhi ya vijana wa taasisi ya maendeleo ya vijana nchini wakisikiliza nasaha kutoka kwa Mama Salma Kikwete

Mama Salma Kikwete akiwa kwenye Picha ya pamoja.

Taswira Za Uzinduzi Wa Kampeni Za Chadema igunga

Anaitwa Joseph Kashinye, Mgombea ubunge kwa tiketi ya CHADEMA jimbo la Igunga. "Ninashughulikia kupata mtandao wa uhakika. Leo siku haitoisha, nitakuwa nimepata suluhu la tatizo la Mtandao. Nitawaporomoshea kila kinachojiri huku. Asubuhi hii nimebahatisha kuingiza picha hiyo kwa taabu, imenichukua saa mbili kuingiza picha moja! Pichani Kashindye alikuwa akihutubia maelfu ya wakazi wa Igunga katika uzinduzi wa kampeni jana.
Mabango yenye ujumbe tofauti katika mkutano wa CHADEMA jana.
Katibu mkuu wa CHADEMA Dr Willbroad Slaa akihutubia mjini Igunga jana katika uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo jimboni hapa.Dr Slaaa alisema CCM hawana sababu ya kuchaguliwa kwa nafasi yoyote ile kwani kwa kipindi cha miaka 50 imeshindwa kumkomboa Mtanzania katika lindi la umaskini.Aliongeza kuseam kuwa CCM wanachokizinatia ni kutumia kila mbinu ili kushinda chaguzi na kushika dola ikiwa hawana malengo na mikakati madhubuti ya kumkomboa Mtanzania. Aliwaasa wana Igunga kumchagua Mgombea wa Chadema, Joseph Kashindye, ili awe mwakilishi wao kwani ni mtu makini anaetoka katika chama makini.

Mwenyekiti wa CHADEMA,Freeman Mbowe akihutubia maelfu ya wana Igunga jana katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za chaguzi mdogo jimboni la igunga.Mbowe alisema kuwa wana Igunga mungu amewapa bahati kubwa ya ufaya uchaguzi muda ,fupi baada ya uchaguzi mkuu. Hivyo waitumie bahati hiyo wa kufanya mabadiliko. CCM haistaili kurudishwa tena madarakani jimboi hapa, kwani kuna masuala mengi ya msingi yanayohusiana na maendeleo ya wananchi CC imeshindwa kuyatekeleza kwa kipindi cha miaka 50.

Ilifika zamu ya Mgombea wa Ubunge jimboni hapa kwa Tiketi ya Chadema, Mwalimu, Mkaguzi wa Elimu, Joseph Lashindye.Kashindye alisema kuwa wana Igunga wtarajie mabadiliko ya haraka katika maendeleo.Yeye ameamua kwa makusudi kuacha ualimu na kuingia katika ulingO wa siasa. Amefanya kama Mwalimu Nyerere alivyofanya kwani Mwalimu Nyerere, aliaacha ualimu na kujiunga na TANU, matokea ya uamuzi huo wa mwalimu hakuna Mtanzania asiyeyaju.Na yeye alisema kuwa endapo wana-Igunga watamapa ridhaa ya kuwa mwakilishi atasimamia kwa nguvu zake zote misingi ya utu, uchapakazi na atahakikisha anaziba mianya yote ya rushwa katika halmashauri ya wilaya, ili fedha zinazotafunwa na wajanja, zifanye kazi iliyokusudiwa ya kuwaletea maendeleo wana- Igunga.

Mbunge wa jimbo la Ubungo John Mnyika akiwahutubia wananchi wa jimbo la Igunga jana jioni katikauzinduzi wa kampeni za ubunge jimboni humo.

Mbunge wa jimbo la Mbeya Mjini Mh. Joseph Mbilinyi akiwahutumia wakazi wa Igunga.

Kutoka kulia ni katibu Mkuu wa CHADEMA Dr. Wilbroad Slaa, Joseph Kashindye mgombea ubunge wa Jimbo la Igunga katikati na Mwenyekiti wa Chama hicho na mbunge wa jimbo la Hai wakielekea kwenye mkutano.


Mabango yalikuwa ni mengi lakini pia jeshi la polisi lilihakikisha kunakuwa na usalama wa kutosha.
Hivi ndivyo ilivyokua Iginga.

Kuhusu Matumizi ya Nembo ya Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara na Maonesho Makubwa ya Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara

Katibu mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana Utamaduni na Michezo Bw. Sethi Kamuhanda (katikati) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) jana jijini Dar es salaam kuhusu matumizi ya nembo ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara na maonesho makubwa ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania Bara yatakayofanywa na Wizara hiyo eneo la Butiama, Musoma kuanzia tarehe 7-14 Oktoba na kutoa wito kwa wananchi kujitokeza kushiriki maonesho hayo na kuitumia nembo hiyo kwenye shughuli mbalimbali zikiwemo za biashara .Kushoto ni Bw. Mulwa Msongo Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu na Bw. Raphael Hokororo (kulia) Mkurugenzi msaidizi wa Idara ya Habari.

Wednesday, September 7, 2011

Mchezaji wa kulipwa Nizar Khalfan amkabidhi jezi Rais kikwete Ikulu jijini dar.


Mtanzania anayecheza Soka ya kulipwa katika timu ya White Caps ya jijini Vancouver Canada Nizar Khalfan akimkabidhi Rais Dkt.Jakaya Kikwete jezi ya timu yake wakati alipokwenda kumsalimu na kumshukuru ikulu jijini Dar es Salaam jana jioni.

STARS YATOKA SARE YA 1-1 NA ALGERIA

Mchezaji wa kimaaifa wa Stars anayecheza mpira wa kulipwa Nchini,Vietnam,Dany Mrwanda akijaribu kumpita mchezaji wa timu ya Taifa ya Algeria Laifaoni Abderkadir kwenye mechi iliyochezwa leo uwanja wa Taifa,Dar na mpira kuisha kwa sare ya 1-1,Stars ndio iliyokua ya kwanza kupata bao lililofungwa na Mbwana Samata

Wachezaji wa Stars wakishangilia bao lilifungwa na Mbwana Samata(kati)kushoto ni Amir Maftaha akiwa na Dany Mrwanda.

Mrembo Rose Albert anyakua taji la Vodacom Miss Talent 2011

Mrembo Rose Albert akionyesha kipaji chake katika siku ya kumtafuta Vodacom Miss Talent 2011 ambapo alifanikiwa kunyakua taji hilo, usiku wa kuamkia leo katika hotel ya Giraffe jijini Dar es Salaam

Majaji wa shindano la Vodacom miss Talent 2011 wakiwa kazini,kutoka kushoto Jacqueline Walper,Rachel Sindbard,Bosco Majaliwa.

Baadhi ya warembo wanaoshiriki katika shindano la Vodacom Miss Tanzania wakipozi kwa picha katika kinyang’anyiro cha Vodacom miss talent 2011 ambapo Rose Albert alifanikiwa kunyakua taji hilo, usiku wa kuamkia leo katika hotel ya Giraffe jijini Dar es Salaam.

Warembo tano bora waliofanikiwa kuingia katika kinyang’anyiro cha Vodacom miss talent 2011 ambapo Rose Albert watatu toka kushoto alifanikiwa kunyakua taji hilo usiku wa kuamkia leo katika hotel ya Giraffe jijini Dar es Salaam

Vodacom Miss Talent 2011 Rose Albert akiwapungia mkono watazamaji mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa shindano hilo.