Wednesday, September 12, 2012

MGOMBEA ALIYEDAI ATATETEA KITI CHA UENYEKITI WA JUMUIYA YA WAZAZI WILAYANI MANYONI, AJITOA DAKIKA ZA MWISHO.

Mwenyekiti wa zamani wa jumuiya ya wazazi wilaya ya Manyoni Hemed Salum Hamad, akitoa nasaha zake kabla ya kujiuzulu na kamati yake ya zamani ili kupisha uchaguzi mpya kufanyika.Wa kwanza kulia ni mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Manyoni,Mosses Matonya,anayefuata ni mweka hazina wa CCM wiilaya ya Manyoni, Hersi, Katibu wa UVCCM na Mkuu wa wilaya ya Manyoni,Fatuma Toufik (mwenye miwani).

Mmoja wa wanachama wa jumuiya ya wazazi wilaya ya Manyoni akipiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa jumuiya hiyo.

Msimamizi wa uchaguzi wa jumuiya ya wazazi Manyoni, ambaye ni katibu msaidizi CCM wilaya ya Singida vijijini Johari Seleman,akitoa maelekezo ya mkutano mkuu wa uchaguzi kabla zoezi la uchaguzi halijaanza.

Aliyekuwa mgombea wa nafasi ya mwenyekiti  wa jumuiya ya wazazi wilaya ya Manyoni Hemed Salum Hamad ambaye alijitoa ghafla,akisaini hati ya kitendo chake cha kutoa jina kwa hiari yake mwenyewe.

Mwenyekiti mpya wa jumuiya ya wazazi aliyepita bila kupigwa,Yahaya Omari Masare akisaini hati ya kuchaguliwa kwake kwenye nafasi hiyo ya uenyekiti.

Mwenyekiti mpya wa jumuiya ya wazazi CCM wilaya ya Manyoni,Yahaya Omari Masare akiwapungia kwa furaha wapiga kura wake kwa kitendo cha kumpitisha bila kupingwa.

Mwenyekiti mpya wa jumuiya ya wazazi CCM Yahaya Masare akipongezwa na mwanachama wa jumuiya ya wazazi wilaya ya Manyoni.

Mwenyekiti mpya wa jumuiya ya wazazi CCM wilaya ya Manyoni, Yahaya Omari Masare (kulia) na mwenyekiti wa zamani wa jumuiya hiyo,mzee Hemed Salum Hamad. 

HABARI KAMILI:
Aliyekuwa mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi wilaya ya Manyoni mkoani Singida, Hemed Salum Hamad (65) ameushangaza mkutano mkuu wa uchaguzi kutoka na kitendo chake cha kujitoa ghafla kutetea nafasi yake.
Kitendo hicho  hiyo kitendo kimepelekea mpinzani wake Yahaya Omari Masare (52) kupita bila kupingwa.
Awali mzee Hemed akiwa na viongozi wenzake wa kipindi kilichopita wakati wakijiuzulu ili kupisha uchaguzi kufanyika, katika nasaha zake, alisema atatetea nafasi yake hiyo.
Baada ya wagombea hao kusimama mbele ya wapiga kura, kwa mshangao mkubwa mzee Hemed alisema anatoa jina lake katika kinyang’anyiro hicho cha nafasi ya mwenyekiti wa jumuiya wa wazazi.
Kutokana na mzee kuondoa jina, msimamizi Johari alimtangaza Yahaya Omari Masare, kuwa mwenyekiti mpya wa wazazi wilaya ya Manyoni, kwa kipinid cha miaka mitano ijayo.
Masare ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya Azirona ya Itigi, Juni mwaka huu, pia alipita bila kupingwa kwenye nafasi ya mwenyekiti wa wazazi kata ya Itigi.

No comments:

Post a Comment