Tuesday, December 4, 2012

Diwani kata ya Ikungi Singida (CHADEMA) amesema ripoti ya uwajibikaji haitochakachuliwa kamwe.

 Mkuu wa wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida Manju Msambya (aliyesimama) akitangaza kuahirishwa kwa mkutano wa mrejesho wa ripoti ya uwajibikaji katika halmashauri ya wilaya ya Singida.Wa tatu kutoka kushoto ni mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Singida na wa pili kushoto ni makamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Singida Alli Nkhangaa.
 Pichani juu na chini ni Baadhi wa wadau wa maendeleo wa halmashauri ya wilaya ya Singida wakimsikiliza kwa makini mkuu wa wilaya ya Ikungi,Manju Msambya (hayupo pichani) wakati akiahirisha mkutano wa mrejesho wa ripoti ya uwajibikaji.

 Mmoja wa maafisa kutoka shirika lisilo la kiserikali la Sikika akikusanya ripoti zilizosababisha kuahirishwa kwa mkutano wa mrejesho wa ripoti ya uwajibikaji katika halmashauri ya wilaya ya Singida.
Kiongozi wa timu ya shirika lisilo la kiserikali la Sikika Mahindi Simon akieleza kusikitishwa kwake kuahirishwa kwa mkutano wa mrejesho wa ripoti ya uwajibikaji.


Diwani wa viti maalum (CHADEMA) tarafa ya Ikungi wilayani Ikungi mkoani Singida Tedi Daghau, amesema pamoja na halmashauri ya wilaya ya Singida kusogeza mbele mkutano wa mrejesho wa ripoti ya uwajibikaki, haitakuwa na ubavu wa  ‘kuichakachua’ ripoti hiyo kwa lengo la.....
kulindana na kuficha uozo.
Akifafanua, amesema ripoti hiyo ambayo imeandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Sikika, imeanika wazi uozo pamoja na matumizi mbaya ya raslimali ya umma, imefahamika vizuri kwa wajumbe waliofika kuhudhuria mkutano huo, na hawatadanganywa.
Kwa  upande wake kiongozi wa timu ya Sikika Mahindi Simon, amesema kwa ujumla wameshangazwa na kusikitishwa na uamuzi wa kusogeza mbele mkutano huo.
Amesema kwenye ripoti yao, hawakulenga kushutumu kiongozi/mfanyakazi ye yote wa halmashauri, bali ripoti hiyo inahitaji tu kufafanuliwa kwenye maeneo yenye utata.

No comments:

Post a Comment