Sunday, December 16, 2012

Dkt. Kone awataka wakuu wa wilaya Singida kuhakikisha watoto wanapata chanjo mbili mpya za Rotavirus na PCV 13.

 Mkuu wa mkoa wa Singida Dk.Parseko Kone akizungumza kwenye mkutano maalum wa uhabarishaji juu ya umuhimu wa chanjo mpya za Rotavirus inayokinga maradhi ya kuharisha na PCV 13,inayokinga ugonjwa wa Nimonia.Chanjo hizo ambazo ni mpya,zinatarajiwa kuanza kutolewa kuanzia Januari mwakani.
Mkuu wa wilaya ya Iramba.Yahaya Nawanda akichingia mada juu ya chanjo mpya za totavirus na PCV 13 kwenye mkutano maalum kwa lengo la kuhabarisha juu ya chanjo hizo.

 Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Parseko Kone amewaagiza wakuu wa wilaya kuhakikisha wanawahamasisha wananchi juu ya umuhimu wa watoto wao kupata chanjo mbili mpya, za Rotavirus na PCV 13 ili kujikinga na magonjwa  ya
kuharisha na nimonia.
Dk. Kone ametoa agiza hilo wakati akizungumza kwenye mkutano maalum ulioitishwa kwa ajili ya uhabarishaji wa chanjo hizo mpya, ambapo amesema lengo la serikali kupitia wizara yake ya afya na ustawi wa jamii ni kuhakikisha wananchi wake wanakuwa na afya bora.
Mkuu huyo  wa mkoa amesema ili lengo hilo liweze kufanikiwa, imeanzisha chanjo mpya ya Rotavirus ambayo ni kwa ajili ya kukinga magonjwa ya kuharisha na PCV 13 ya kuzuia nimonia kwa watoto wote walio chini ya umri wa chini ya mwaka moja.
Amesema chanjo hizo zinatarajiwa kuanza kutolewa kuanzia Januari mwakani, na zitatolwewa kwenye kliniki zote.
Akifafanua zaidi, amesema kuharisha kunakosababishwa na virus vya rota, kunazuilika kwa chanjo inayoitwa Rotavirus.
Kuhusu chanjo ya PCV 13, amesema chanjo hiyo inayo uwezo wa kuzuia magonjwa hatari yakiwemo homa ya kichomi (nimonia) na uti wa mgongo.

No comments:

Post a Comment