Monday, December 17, 2012

Serikali Wilayani Singida yazindua awamu ya pili ya kampeni ya Vita dhidi ya Jangwa.

 Mkuu wa wilaya ya Singida Mwalimu Queen Mlozi akizindua upandaji miti katika kijiji cha Kitope manispaa ya Singida.

 Mkuu wa wilaya ya Singida mwalimu Queen Mlozi akishiriki kampeni ya kupanda miti ili kuokoa wilaya hiyo isikumbwe na balaa la Jangwa.


 Mtoto Juma Sungi wa darasa la tatu katika shule ya msingi ya Mwankoko manispaa ya Singida akishiriki kampeni ya kupanda miti kwa lengo la kunusuru manispaa hiyo isigeuke jangwa.
Mkuu wa wilaya ya Singida mwalimu Queen Mlozi akionyesha miche ya miti maji ambayo amedai kuwa inatumika kuvuna mbao na pia kutengenezea sabuni.

 Serikali wilayani Singida imepiga marufuku mara moja uvunaji ovyo wa misitu, kwa madai kwamba uvunaji wa aina hiyo, unatishia
wilaya hiyo kugeuka jangwa.
Mkuu wa wilaya hiyo mwalimu Queen Mlozi, ametoa agizo hilo la kupiga marufuku, wakati akizindua awamu ya pili ya kampeni ya vita dhidi ya jangwa katika wilaya hiyo.
Amesema kumekuwa na uvunaji wa ovyo wa msitu usiokuwa na uwiano na upandaji wa misitu, unachochewa kwa kiasi kikubwa na biashara ya mkaa.
Mlozi amesema hivi sasa kuna malori mengi kutoka wilaya ya Arusha na Manyara, ambayo yanasafirisha mamia kwa mamia ya magunia ya mkaa kutoka Wilaya ya Singida, biashara ambayo inataka kuacha wilaya yetu kuwa jangwa, haikubaliki na hatutaki iendelee ni lazima tuikomeshe.
Mkuu huyo wa wilaya amesema kuanzia sasa, vizuizi viwekwe kwenye sehemu husika  ili kuyakamata malori hayo ya mkaa na wahusika wachukuliwe hatua kali za kisheria.
 Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi ya Ant desert environment scheme Kitanto Said, alisema katika awamu hii ya pili ya kampeni dhidi ya jangwa, wanatarajia kupanda miti zaidi ya elfu moja.

No comments:

Post a Comment