Wednesday, September 19, 2012

GARI LA POLISI LAUA SITA LIKISAFIRISHA MAITI

 Wananchi wa mji wa Singida wakiwa wamekusanyika nje ya viwanja vya chumba cha kuhifadhia maiti ktk hospitali ya mkoa wa Singida

          Wauguzi wakijiandaa kuingiza moja ya maiti ya ajali hiyo mochwari

 WATU wanane wamefariki dunia katika ajali mbili tofauti zilizotokea mjini Singida kwa kuhusisha magari mawili, ikiwemo Landrover ya polisi na kusababisha jumla ya majeruhi 25. Ajali hizo zimetokea jana (14/9/2012) moja saa 5:30 asubuhi na nyingine saa 6:30 mchana.
Landrover ya polisi iliyohusika na ajali hiyo ni namba PT 1149 kutoka mkoni Morogoro ikiwa na abiria 11 waliokuwa wanasindikiza mwili wa askari polisi Regu Kamamo, kwenda Musoma kwa ajili ya maziko.

Kamanda wa polisi mkoa mkoa wa Singida, Linus Sinzumwa alisema kuwa gari hilo lilipata ajali katika kambi ya Wachina iliyopo eneo la Manguajunki nje kidogo ya mji wa Singida.Aliwataja walifariki katika ajali iliyohusisha gari la polisi ni, staff sajenti Rose Mary Nyaruzoki (53), Nyamwenda Juma, Rehema Juma.


Sinzuma alisema uchunguzi zaidi bado unaendelea ili kubaini chanzo cha ajali hiyo huku akifafanua kuwa majeruhi wanane wa ajali hiyo wamelazwa hospitali ya mkoa Singida na hali zao zinaendelea vizuri.
Katika tukio la pili, alisema lori Fusso T.126 AEU likiwa na wafanyabishara wa mnadani likitokea Singida mjini kwenda mnada wa Mtavira kata ya Minyunge wilaya ya Singida, lilipinduka na kusababisha vifo vya watu watano na majeruhi 17

Alisema ajali hiyo ilitokea jana saa 6.30 mchana katika kijiji cha Mtavira, Singida vijijini.Aliwataja waliofariki dunia papo hapo ni Sarafina Ally, Pili Saida, Charles Thomas na wengine wawili waliofahamika kwa jina moja moja la Bakari na Bilali.


Alisema chanzo cha ajili ya fuso,bado hakijafahamika na uchunguzi zaidi bado unaendelea. Hata hivyo Sinzumwa alisema taarifa kamili kuhusiana na ajali hizo, atazitoa kesho (leo 15/9/2012) .Mganga mfawidhi hospitali ya mkoa Singida, Dk. Joseph Malunde alisema majeruhi hao 17, wamelazwa hospitali ya mkoa wa Singida na hali zao zinaendelea vizuri.

"Maiti zote tisa pamoja na ile ya askari aliyekuwa anasafirishwa na gari la polisi na zile za Fusso, zimehifadhiwa chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya mkoa,"alisema Dk. Malunde.

Kwa mjubu wa mmoja wa majeruhi wa fuso,Maulidi Mohammed,fuso hilo lilipinduka baada ya breki zake kufeli likiwa kwenye mteremko mkali hali iliyosababisha dereva ambaye hata hivyo hajafahamika ashindwe kulimudu.

Thursday, September 13, 2012

HUYU NDIYE MTOTO ALIYEMUOA MAMA YAKE MZAZI






NATURE NI BABA YANGU ILA AMENIKATAA

Kijana huyu anadai kuwa yeye ni mtoto wa msanii Juma Nature na kujitambulisha kama Samson Juma Kassim Kiroboto, Samson anatokea Morogoro na kwa maelezo yake yeye amezaliwa mwana 1995.
 
"mama yangu ameshafariki na nilishawahi kwenda mpaka kwa baba yangu Juma Temeke nikiwa na bibi yangu, lakini aliponiona tu akanifukuza akasema hataki kuniona tena " hayo ndio yalikua maelezo ya Samson.

 
                        Unaona kuna kufanana na nature katika picha hiyo?

Wednesday, September 12, 2012

DEMU ACHEZA NUSU UCHI UZINDUZI WA VIDEO MPYA YA BAADAYE BY OMMY DIMPOZ CLUB BILLICANAZ












HUYU NDIYE ALIYEMUUA MWANDISHI DAUDI MANGOSI

Askari Namba G.2573 Pacificus Cleophase Simon(23),afisa wa polis mkazi wa FFU Iringa, anashitakiwa kwa mauaji kufatia sheria namba 196 kifungu kidogo (i) sura ya 16,marejeo ya mwaka 2002. Manamo tarehe 2/9/2012 katika kijiji cha Nyololo Wilaya ya Mufindi alimuua kwa kukusudia Ndg, Daudi Mwangosi . Akisomewa shitaka na mwendesha mashitaka mkuu wa serikali MICHAEL LUENA mkoa wa Iringa mbele ya hakimu mkazi mwandamizi wilaya ya Dyness Lyimo,mshitakiwa hakutakiwa kujibu chochote. Upelelezi wa kesi hiyo bado unaendelea na kesi imeahirishwa na itatajwa tena tarehe 26/9/2012.

DEMU ANAYEMDATISHA NEY WA MITEGO HUYU HAPA


WAANDISHI WA HABARI SINGIDA NAO WAANDAMANA KUPINGA MAUAJI YA MWANDISHI MWENZAO DAUDA MWANGOSI

Askari wa usalama barabarani akiongoza maandamano ya wanahabari wa Singida walioandamana kupinga mauaji ya mwenzao

 Baadhi ya waandishi wa habari mkoa Singida-SINGPRESS wakiwa ofisi za klabu wakimsikiliza Mwenyekiti waoo, Seif Takaza

MAANDAMANO YAKIENDELEA KATIKA BARABARA MBALIMBALI ZA SINGIDA


MGOMBEA ALIYEDAI ATATETEA KITI CHA UENYEKITI WA JUMUIYA YA WAZAZI WILAYANI MANYONI, AJITOA DAKIKA ZA MWISHO.

Mwenyekiti wa zamani wa jumuiya ya wazazi wilaya ya Manyoni Hemed Salum Hamad, akitoa nasaha zake kabla ya kujiuzulu na kamati yake ya zamani ili kupisha uchaguzi mpya kufanyika.Wa kwanza kulia ni mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Manyoni,Mosses Matonya,anayefuata ni mweka hazina wa CCM wiilaya ya Manyoni, Hersi, Katibu wa UVCCM na Mkuu wa wilaya ya Manyoni,Fatuma Toufik (mwenye miwani).

Mmoja wa wanachama wa jumuiya ya wazazi wilaya ya Manyoni akipiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa jumuiya hiyo.

Msimamizi wa uchaguzi wa jumuiya ya wazazi Manyoni, ambaye ni katibu msaidizi CCM wilaya ya Singida vijijini Johari Seleman,akitoa maelekezo ya mkutano mkuu wa uchaguzi kabla zoezi la uchaguzi halijaanza.

Aliyekuwa mgombea wa nafasi ya mwenyekiti  wa jumuiya ya wazazi wilaya ya Manyoni Hemed Salum Hamad ambaye alijitoa ghafla,akisaini hati ya kitendo chake cha kutoa jina kwa hiari yake mwenyewe.

Mwenyekiti mpya wa jumuiya ya wazazi aliyepita bila kupigwa,Yahaya Omari Masare akisaini hati ya kuchaguliwa kwake kwenye nafasi hiyo ya uenyekiti.

Mwenyekiti mpya wa jumuiya ya wazazi CCM wilaya ya Manyoni,Yahaya Omari Masare akiwapungia kwa furaha wapiga kura wake kwa kitendo cha kumpitisha bila kupingwa.

Mwenyekiti mpya wa jumuiya ya wazazi CCM Yahaya Masare akipongezwa na mwanachama wa jumuiya ya wazazi wilaya ya Manyoni.

Mwenyekiti mpya wa jumuiya ya wazazi CCM wilaya ya Manyoni, Yahaya Omari Masare (kulia) na mwenyekiti wa zamani wa jumuiya hiyo,mzee Hemed Salum Hamad. 

HABARI KAMILI:
Aliyekuwa mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi wilaya ya Manyoni mkoani Singida, Hemed Salum Hamad (65) ameushangaza mkutano mkuu wa uchaguzi kutoka na kitendo chake cha kujitoa ghafla kutetea nafasi yake.
Kitendo hicho  hiyo kitendo kimepelekea mpinzani wake Yahaya Omari Masare (52) kupita bila kupingwa.
Awali mzee Hemed akiwa na viongozi wenzake wa kipindi kilichopita wakati wakijiuzulu ili kupisha uchaguzi kufanyika, katika nasaha zake, alisema atatetea nafasi yake hiyo.
Baada ya wagombea hao kusimama mbele ya wapiga kura, kwa mshangao mkubwa mzee Hemed alisema anatoa jina lake katika kinyang’anyiro hicho cha nafasi ya mwenyekiti wa jumuiya wa wazazi.
Kutokana na mzee kuondoa jina, msimamizi Johari alimtangaza Yahaya Omari Masare, kuwa mwenyekiti mpya wa wazazi wilaya ya Manyoni, kwa kipinid cha miaka mitano ijayo.
Masare ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya Azirona ya Itigi, Juni mwaka huu, pia alipita bila kupingwa kwenye nafasi ya mwenyekiti wa wazazi kata ya Itigi.

Monday, September 10, 2012

SERENGETI FIESTA 2012 JINSI ILIVYO TINGISHA SINGIDA

 Msanii wa muziki wa kizazi kipya Cirryl a.k.a Kamikazi akikamua jukwaani usiku huu ndani ya tamasha la Serengeti Fiesta 2012.

             Ni Kushangweka tu ndani ya viwanja vya Singida Motel usiku huu

 Rich Mavoco akiwaimbisha mashabiki wake waliofika kwenye tamasha la Serengeti Fiesta usiku huu,ambapo wakazi wa mji huo wamejitokeza kwa wingi kuwashuhudia wasanii mbalimbali wanaotumbuiza kwenye tamasha hili

 Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Shillole akijimwaya mwaya jukwaa mbele ya umati wa wakazi wa mji wa Singida (hawapo pichani),usiku huu. 

  Pichani juu na chini Sehemu ya Umati wa watu waliojitokeza kwa wingi usiku huu kwenye viwanja vya Singida Motel ambako tamasha la Serengeti Fiesta 2012 likiendelea

  Pichani kati ni msanii wa bongofleva kutoka THT,Recho akiwa sambamba na dansaz wake jukwaani wakikamua vilivyo. 

 Baadhi ya wakazi wa Singida waliojitokeza kwa wingi usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta wakishangilia jambo.

 Wasanii wa muziki wa kizazi kipya,Mabeste na msanii mwenzake wakitumbuiza jukwaani usiku huu

 Pichani ni Ofisa Mahusiano wa kampuni  Clouds Fm,Simalenga akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Singida Mjini,Mh Queen Mlozi pamoja na nduguze wakishuhudia tamasha la Serengeti Fiesta likiendelea usiku huu kwenye viwanja vya Singida Motel,Mkoani Singida ambapo wakazi wa mji huo wameitikia wito wa kujitokeza kwa wingi kuwashuhudia wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya

  Anaitwa Ben Paul mmoja wa wasanii mahiri wa Bongofleva katika miondoko ya R&B


 Shillole akiwapa dole mashabiki wake waliokuwa wakimshangilia kwa nguvu.

 Pichani kulia ni Dj Zero akiwa amepozi mtangazaji wa kipindi cha XXL,wote wafanyakazi wa Clouds FM wakishoo love usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012 ndani ya viwanja vya Singida Motel.

MAANDALIZI YA SERENGETI FIESTA 2012 SINGIDA

Stage ikiwa katika Maandalizi ya mwisho


Gari likiingiza jiko la kuchomea nyama