Saturday, March 30, 2013

Mwalimu wa walemavu amtaka Rais ateue walemavu kushika nafasi za Ukuu wa Wilaya, Mkoa na Uwaziri.

 Mwalimu mkuu msaidizi wa walemavu katika shule ya msingi mchanganyiko Ikungi wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida, Donard Bilali akitoa wito wake kwa rais Kikwete kuangalia uwezekano wa kuteua walemavu kushika nafasi za ukuu wa wilaya,mkoa na uwaziri kama anavyofanya kwa kundi la wanawake.
Mwalimu wa walemavu katika shule ya msingi mchanganyiko Ikungi wilayani Ikungi,Manase Ligula akitoa wapendekezo yake kuwa katiba ijayo,iagize wamiliki wa vyombo vya usafiri,watoe huduma bure kwa walemavu.

Rais wa jamhuri ya muungano Tanzania,Dk.Jakaya Mrisho Kikwete ameshauriwa kuangalia uwezekano wa kuteua walemavu kushika nafasi za ukuu wa wilaya,mkoa na uwaziri kwa wale wenye uwezo na sifa za kuongoza katika nafasi hizo kwa ufanisi.
Wito huo umetolewa na mwalimu mkuu msaidizi wa walemavu katika shule ya msingi mchanganyiko ya Ikungi wilaya ya Ikungi , Donard Bilali wakati akizungumza na Singida Yetu Blog juu ya zoezi la uundwaji wa mabaraza ya katiba.
Amesema serikali ya awamu ya nne iliyoko chini ya rais Kikwete,imefanya

Mh. Dewji atoa msaada kwa taasisi za dini mkoani Singida

 Katibu wa mbunge jimbo la Singida mjini (Mh. Mohammed Dewji) Duda Juma akikabidhi mabati 100 kwa mchungaji Zefania Mkuki wa kanisa la FPCT (Free penecoste church of Tanzania) Unyamikumbi la mjini Singida.
 Katibu wa mbunge jimbo la Singida mjini (Mh. Mohammed Dewji) Duda Juma akimkabidhi Kiongozi wa msikiti wa Hidaya Mtipa mifuko 50 ya Sementi.
 Katibu wa mbunge jimbo la Singida mjini Duda Juma akikabidhi mabati 164 kwa mwenyekiti msaidizi Aloyce J.M wa kanisa la Kigango cha kibaoni.
Katibu wa mbunge wa Singida mjini Duda Juma akimkabidhi sheikh Ihucha Imamu wa msikiti wa Jabal Hiraa mifuko 200 ya Sementi.

umuhimu wa walemavu kushirikishwa kikamilifu katika uundaji wa mabaraza ya katiba.

 Bango la shule ya msingi mchanganyiko Ikungi wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida.

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi mchanganyiko Ikungi,wakiwa darasani.
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi mchanganyiko Ikungi wilaya ya Ikungi Olivary Kamilly akizungumza na waandishi wa habari (hawapo kwenywe picha) juu ya umuhimu wa walemavu kushirikishwa kikamilifu katika uundaji wa mabaraza ya katiba.


Mwalimu mkuu wa shule ya msingi mchanganyiko wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida Olivary Kamilly, amependekeza walemavu washirikishwe kikamilifu katika mabaraza ya katiba kwa madai kuwa ndio wenye uwezo mzuri wa kuwakilisha mahitaji yao.
Mwalimu Kamilly mwenye taaluma ya ufundishaji walemavu, ametoa pendekezo hilo wakati akizungumza na Singida Yetu Blog ofisini kwake, juu ya uundaji wa mabaraza ya katiba.
Amesema mahitaji ya walemavu yataelezwa vizuri zaidi na walemavu wenyewe kwa kuwa wanaishi na ulemavu.
Akifafanua  zaidi, mwalimu huyo mkuu amesema

Asilimia 46 ya wakazi wa kijiji cha Ntwike mkoani Singida wanapata maji safi na salama kutokana na mradi wa maji.

 Katibu tawala wa wilaya ya Iramba,Yahaya Naniya akizundua mradi wa maji wa kijiji cha Ntwike tarafa ya Shelui uliogharimu zaidi ya shilingi 190 milioni.
 Mhandishi wa idara ya maji wilaya ya Iramba akitoa taarifa yake kwenye kilele cha wiki ya maji iliyofanyika kiwilaya katika kijiji cha Ntwike wilaya ya Iramba.
 Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Ntwike tarafa ya Shelui waliohudhuria maadhimisho ya wiki ya maji kiwilaya yaliyofanyikia kwenye kijiji hicho.
Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Nkokilangi tarafa ya Shelui wilaya ya Iramba,wakichota maji juzi kwenye mto wa durumo juzi.Hata hivyo,maji hayo si salama kwa afya ya binadamu.

Shirika lisilo la kiserikali la mpango endelevu na uboreshaji  mazingira (SEMA), kwa kushirikiana na halmashuari ya wilaya ya Iramba na wananchi wa kijiji cha Ntwike jimbo la Iramba Magharibi, kwa pamoja wamechangia zaidi ya shilingi milioni 190.5 kwa ajili ya kugharamia ujenzi wa mradi wa maji katika kijiji cha Ntwike tarafa ya Shelui.
Afisa mipango wa SEMA Hudson Kazonta amesema hayo wakati akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa mradi huo wa maji ambao ulikuwa ni

Thursday, March 21, 2013

Serikali ya wilaya ya Singida imeagiza kuwa kila siku ya Jumatano kuwa siku ya usafi kwa kazi zote kusimama na kufanya usafi tu.

 Mkuu wa wilaya ya Singida Mwalimu Queen Mlozi akikagua kibanda cha mama lishe katika soko kuu mjini Singida.
 Mkuu wa wilaya ya Singida Mwalimu Queen Mlozi akiwa kwenye ziara ya kuhimiza usafi katika manispaa ya Singidaleo. Hapa akihimiza kuondolewa kwa uchafu wa matawi ya migomba katika soko mkuu mjini Singida.
 Mkuu wa wilaya ya Singida Mwalimu Queen Mlozi akiwaagiza akina mama wajasiria mali wauzaji wa mboga mboga katika soko kuu la Singida mjini wahakikishe soko kuu linakuwa safi wakati wote kwa kuondoa takataka.
Mkuu wa wilaya ya Singida Mwalimu Queen Mlozi (kulia) akifurahia jambo na wajasiriamali wauza mboga mboga wa soko kuu mjini Singida.

Tatizo la uhaba wa maji kwa wakazi wa Singida kumalizika mwishoni kwa mwezi ujao.

Serikali ya mkoa wa Singida imesema tatizo la muda mrefu la uhaba wa maji kwa wakazi wa Singida mjini, litakuwa historia ifikapo mwishoni mwa mwezi ujao, baada ya mradi mkubwa wa maji unaofadhiliwa na benki ya kiarabu (BADEA) na shirika la mafuta ulimwenguni (OPEC) utakapomalizika.
Akizungumza kwenye uzinduzi wa wiki ya maji uliofanyika katika eneo la Irao, halmashauri ya manispaa ya Singida, Mkuu wa mkoa wa Singida Dk.Parseko Vicent Kone akifafanua, amesema kuwa utekelezaji wa mradi huu, umefikia kiwango cha aslimia 93 na unategemewa ifikapo

Tuesday, March 19, 2013

TANROADS Singida yatumia zaidi ya sh. Bilioni 2.2 kutengezeka barabara na madaraja 14 kwa kipindi cha Julai ’12 hadi Februari’13.

 Meneja wa TANROADS mkoa wa Singida mhandisi Yustaki Kangole, akitoa taarifa yake kwenye kiako cha bodi ya barabara mkoa wa Singida kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa mjini Singida.
Mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Singida Mathias Mwangu,akichangia maoni  kwenye kikao cha 34 cha bodi ya barabara mkoa wa Singida kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Singida mjini Singida.

Wakala wa barabara (TANROADS) mkoa wa Singida, umetumia zaidi ya sh. 2.2 bilioni kugharamia matengenezo mbalimbali ya barabara zake na madaraja 14, kwa kipindi cha kuanzia Julai mwaka jana hadi Februari mwaka huu.
Akitoa taarifa yake mbele ya kikao cha 34 cha bodi ya barabara, kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa mjini Singida, Meneja wa TANROADS mkoa wa Singida Mhandisi Yustaki Kangole, amesema baadhi ya fedha hizo, Sh. 301.6 milioni, zimetumika kugharamia

HIZI NDO HABARI KUBWA ZA MAGAZETI YA LEO JUMANNE MARCH 19,CHECK JINSI CHADEMA ILIVYO IANGUKIA SEREKALI,JINSI TRAFIKI ALIVYOKUFA AKIONGOZA MSAFARA WA RAIS,RAGE AKIMBILIA TFF NA MENGINE MENGI.





Monday, March 18, 2013

Ajali Kazini Haipingiki, Mungu ailaze roho ya Marehemu Mahali Pema Peponi Amen.

TANROADS Singida yaagizwa kusimamia wakandarasi wa barabara kwa ukaribu ili kuepuka ujenzi chini ya kiwango.

 Mkuu wa mkoa wa Singida Dk.Parseko Vicent Kone akifungua kikao cha 34 cha bodi ya barabara mkoa wa Singida leo. Kikao hicho kimefanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi ya  mkuu wa mkoa mjini Singida.

 Baadhi ya wajumbe wa kikao cha 34 cha bodi ya barabara mkoa wa Singida, wakifuatilia kwa makini kikao hicho kilichokuwa chini ya mwenyekiti ambaye ni  mkuu wa mkoa wa  mkoa wa Singida Dk.Parseko Vicent Kone (hayupo kwenye picha).

Mkuu wa mkoa wa Singida Dk. Parseko Vicent Kone ameuagiza wakala wa barabara (TANROADS), kusimamia kwa karibu na kuhakikisha wakandarasi wanaopewa kazi ya kujenga barabara, wanajenga kwa viwango vilivyoainishwa kwenye mikataba yao.
Dk. Kone amesema kwa njia hiyo kutasaidia mno kupunguza mianya ya kupoteza fedha za umma na  pia, kuondoa malalamiko kutoka kwa viongozi na wananchi, kwamba ujenzi husika haufanani na fedha zilizotumika.
Mkuu huyo wa mkoa ametoa agizo hilo leo wakati akifungua

TFDA Kanda ya Kati Singida yateketeza bidhaa mbalimbali zisizo na viwango zenye thamani ya zaidi ya sh. milioni 7.1.

Mkaguzi wa dawa wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Kanda ya Kati, Dkt.Engelbert Mbekenga, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo kwenye picha) juu ya msako unaoendelea wa kukamata bidhaa zilizokwisha muda wake wa kutumika na zile zilizopigwa marufuku kutumiwa. Hivi karibuni mamlaka hiyo iliteketeza bidhaa zilizoisha muda wake na zile zenye sumu za thamani ya zaidi ya silingi milioni 7.1 zilizokamatwa wilaya ya Iramba na Singida vijijini.

Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Kanda ya Kati, imeteketeza bidhaa mbalimbali ikiwemo vipodozi vyenye viambato vya sumu, zenye thamani ya zaidi ya Sh. milioni 7.1.
Bidhaa zingine zilizoteketezwa ni pamoja na vyakula na vinywaji vilivyokwisha muda wake wa kutumika na zile zenye ubora hafifu.
Hayo yamesemwa na Mkaguzi wa TFDA Kanda ya Kati Dkt. Englibert Mbekenga, muda mfupi baada ya

HIZI NDO HABARI KUBWA ZA MAGAZETI YA LEO JUMATATU MARCH 18,CHECK MIJI 10 ILIYOJEGWA CHINI YA ARDHI,POLISI WAPEKUA OFISI ZA CHADEMA,PAPA BENEDICT AANZA MAISHA YA MFUNGWA NA MENGINE MENGI.





KIBONZO CHA LEO


KIPANYA CHA LEO