Monday, March 18, 2013

Ajali Kazini Haipingiki, Mungu ailaze roho ya Marehemu Mahali Pema Peponi Amen.

Lolote laweza kutokea unapokuwa ukitimiza majukumu ya kazi haswa unapojituma. Yapo mengi mengine ni ya kinadharia lakini mengine ni ya kivitendo hata kuhusisha mwili.
Leo mwenzetu na ndugu yetu dada Elikiza amepoteza uhai wake katika makutano ya barabara ya Shekilango na Bagamoyo eneo la Bamaga wakati akitimiza wajibu wake kama askari wa usalama barabarani kuyapanga na kutoa ishara kwa magari ikizingatiwa leo kulikuwa na msafara wa mkuu wa nchi akiwa katika kutimiza majukumu yake ya kila siku.
Si yeye wala sisi hakuna aliyejua litakalotokea, kwani dakika chache kabla alikuwa akitimiza wajibu wake kama ilivyo ada, lakini ghafla, alipatwa na ajali ya kugongwa na gari iliyokuwa kasi, na kupelea kuanguka na hatimaye kupoteza maisha akiwa katika eneo lake la kazi ambalo ni barabarani.
Mashuhuda wakiwa katika hali ya mshangao na majonzi walijongea kunako mwili wake na kuufunika huku mengi yakizungumzwa kutokana na tukio hilo na pia watu wakilijadili gari lililohusika.
Wana Singida Yetu Blog tunatoa pole kwa familia yake, ndugu, jamaa, marafiki, idara ya usalama barabarani na watanzania wote kwa ujumla, hakuna aliyetegemea kwamba dada yetu sasa hizi hatutakuwa naye tena.
Maisha ndivyo yalivyo lolote laweza kutokea popote. Poleni watanzania.
Ee Mola ipumzishe roho ya marehemu mahali pema peponi Amin.

No comments:

Post a Comment