Saturday, March 30, 2013

Asilimia 46 ya wakazi wa kijiji cha Ntwike mkoani Singida wanapata maji safi na salama kutokana na mradi wa maji.

 Katibu tawala wa wilaya ya Iramba,Yahaya Naniya akizundua mradi wa maji wa kijiji cha Ntwike tarafa ya Shelui uliogharimu zaidi ya shilingi 190 milioni.
 Mhandishi wa idara ya maji wilaya ya Iramba akitoa taarifa yake kwenye kilele cha wiki ya maji iliyofanyika kiwilaya katika kijiji cha Ntwike wilaya ya Iramba.
 Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Ntwike tarafa ya Shelui waliohudhuria maadhimisho ya wiki ya maji kiwilaya yaliyofanyikia kwenye kijiji hicho.
Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Nkokilangi tarafa ya Shelui wilaya ya Iramba,wakichota maji juzi kwenye mto wa durumo juzi.Hata hivyo,maji hayo si salama kwa afya ya binadamu.

Shirika lisilo la kiserikali la mpango endelevu na uboreshaji  mazingira (SEMA), kwa kushirikiana na halmashuari ya wilaya ya Iramba na wananchi wa kijiji cha Ntwike jimbo la Iramba Magharibi, kwa pamoja wamechangia zaidi ya shilingi milioni 190.5 kwa ajili ya kugharamia ujenzi wa mradi wa maji katika kijiji cha Ntwike tarafa ya Shelui.
Afisa mipango wa SEMA Hudson Kazonta amesema hayo wakati akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa mradi huo wa maji ambao ulikuwa ni
sehemu ya kilele cha maadhimisho ya wiki ya maji duniani iliyofanyika kiwilaya katika kijiji cha Ntwike.
Amesema kati ya fedha hizo, shirika la Water Aid, kupitia SEMA, lilitoa zaidi ya shilingi 152.2 milioni kwa ajili ya kugharamia utekelezaji wa mradi huo wa maji.
Kazonta amesema halmashauri ya wilaya ya Iramba, imechangia zaidi ya shilingi 30.5, milioni na wananchi kwa upande wao, wamechangia zaidi ya shilingi 15.2 milioni.
Afisa huyo ametaja baadhi ya shughuli zilizofanyika kwenye mradi huo, kuwa ni pamoja na kuchimba kisima kimoja kirefu, kujenga tanki lenye ujazo wa lita 50,000 ,nyumba ya mashine ya maji na vituo tisa vya kuchotea maji.
Kwa mujibu wa Kazonta, mradi huo ulianza kutekelezwa mwaka wa 2011/2012 na umekamilikaMei mwaka jana.
Kazonta ametumia fursa hiyo, kuwataka wakazi wa kijiji cha Ntwike kuulinda na kuutunza vizuri mradi huo wa maji ili uweze kutoa huduma kwa muda mrefu.
Kwa upande wake Kaimu Mhandisi wa idara ya maji katika wilaya ya Iramba Joel Kisubi, amesema wilaya hiyo ya Iramba yenye wakazi 414,219, wakazi wake wanapata huduma ya maji safi na salama kwa asilimia 46.
Aidha, Joel amesema wilaya hiyo ina jumla ya vyanzo vya maji 699 vya aina mbalimbali na kwamba 617 vinafanya kazi na vilivyobaki 82, havifanyi kazi.

No comments:

Post a Comment