Wednesday, March 13, 2013

Raia wa Rwanda apoteza maisha katika ajali ya gari mkoani Singida.


Gari aina ya nissan presage axis C.6017 A, mali ya Abbakari  Bakudikiza (32) raia wa Rwanda baada ya kupata ajali kwenye kijiji cha Kisaki manispaa ya Singida na kupelekea Abbakari kufariki dunia papo hapo. Gari hilo lilikuwa likiendeshwa na mke wake raia wa Sweden Videl Ruze ambaye alipata majeraha kichwani na amelazwa hospital ya mkoa na hali yake inaendelea vizuri. Wanandoa hao ambao wameoana miezi sita iliyopita, walikuwa wakitoa Dar-es-salaam kuelekea Rwanda.

Mwanaume raia wa Rwanda Abbukari Bakudukiza (32) amefariki dunia hapo hapo, baada ya gari walilokuwa wakisafiria na mke wake kupata ajali. Ajali hiyo imetokea baada ya kupasuka tairi la mbele na kuacha njia na kisha kupinduka.
Mke wa Abbakari raia wa Sweden ambaye alikuwa akiendesha gari hilo ni Videl Ruze (35).
Gari la familia hiyo ni Nissan presage axis C.6017 A.
Akizungumza na Singida Yetu Blog mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Singida Dk. Suleiman Muttani, amesema kuwa
ajali hiyo mbaya, imetokea  katika eneo la kijiji cha Kisaki manispaa ya Singida.
Amesema Abbakari amefariki kutokana na kuvunja damu nyingi baada ya kupata majeraha makubwa kichwani.
  Dk.Muttani amesema Videl aliyekuwa akiendesha gari hilo yeye amepata michumbuko sehemu za kichwani na amelazwa wodi namba tano, katika hospitali ya mkoa mjini Singida na hali yake inaendelea vizuri, huku mwili wa Abbakari ukihifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya mkoa.
Mkuu wa wilaya ya Singida mwalimu Queen Mlozi aliyemtembelea majeruhi Videl wodini amesema kuwa majeruhi Videl amedai kuwa katika safari yao hiyo ya kutoka Dar-es-salaam wakielekea Rwanda njiani walipata pancha mara mbili.
“Majeruhi huyo amesema kuwa wameoana na Mnyarwanda huyo miezi sita iliyopita na kwa sasa ana mimba changa. Amedai walipoanza kuteremka mteremko wa Kisaki, ndipo tairi la mbele lilipobasti na kupelekea kushindwa kulimudu gari hilo”,alisema.
Mlozi amesema kuwa tayari amekwisha wasiliana na ubalozi wa Rwanda nchini na ndugu wa Abbakari wapo njiani kuja kuchukua mwili wa marehemu.
Kwa upande wa mwanamke huyo kutoka Sweden, amesema pia amewasiliana na ubalozi wa Sweden nchini na wao wanafanya utaratibu wa kuja kumwona majeruhi huyo.

No comments:

Post a Comment