Saturday, May 25, 2013

Kliniki tembezi yazinduliwa wilaya ya Iramba mkoani Singida kwa lengo la kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto.

 Mganga mkuu wa wilaya ya Iramba mkoa wa Singida. Dk.Japhet Simeo akitoa taarifa yake katika hafla ya uzinduzi wa kliniki tembezi katika wilaya hiyo yenye lengo la kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto.Uzinduzi huo umefanyika katika zahanati ya kata ya Ndago wilaya ya Iramba.
 Mkuu wa wilaya ya Iramba Yahaya Nawanda, akizungumza kwenye uzinduzi uliofana  wa kliniki tembezi inayotarajiwa kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto.Kushoto ni mkuu wa wilaya ya Singida,mwalimu Queen Mlozi na kulia ni mkuu wa wilaya ya Manyoni, Fatuma Toufiq.
 Mkuu wa wilaya ya Iramba mkoa wa Singida,Yahaya Nawanda (kulia) akizindua kliniki tembezi kwa wilaya hiyo, kwa kupima mama mjamzito Mary Kiula.
 Mkulima wa kijiji cha Sinziligi kata ya Ndago wilaya ya Iramba,Michael Mguna akisaidiwa kubeba mtoto wake Leonard na mama mmoja ambaye sio mke wake.Michael alidai kuwa mke wake alibanwa na shughuli za nyumbani na hivyo yeye akalazimika kumpekeka mtoto wao kliniki kwa mujibu wa ratiba.Mkuu wa wilaya ya Iramba,Yahaya Nawanda amewataka wanaume wote kujenga utamaduni wa kuwasindikiza wake zao kwenda kliniki.

Baadhi ya akina mama wajawazito na wasio wajawazito wa kata ya Ndago wilaya ya Iramba,waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa kliniki tembezi wilayani humo.Kliniki hiyo, imedaiwa kuwa ni ya kwanza hapa nchini.

Friday, May 17, 2013

Uzembe wa mama lishe kusahau kuzima moto wasababisha Vibanda vinne kuteketea kwa moto mkoani Singida.

Diwani wa Chadema ashambulia Ng’ombe sita wa mpiga kura wake na kufyeka shamba la Alizeti.

Baadhi ya Ng’ombe sita mali ya John Theodore Ghumpi wa kijiji cha Minyinga jimbo la Singida mashariki,waliokatwa katwa juzi na diwani wa CHADEMA kata ya Mungaa Matheo Alex kwa kile kilichodaiwa kuwa ni ugomvi wa kugombea ekari 50 za mbuga.

Mkulima na mfugaji wa kijiji cha Minyinga kata ya Mungaa jimbo la Singida Mashariki, John Theodore Ghumpi akionyesha Ng’ombe wake aliyekatwa kwa shoka na diwani wa kata ya Mungaa Matheo Alex kwa tuhuma ya kugombea mbuga ya ekari 50.
Kaimu OCD wilaya ya Ikungi, Deo Batete akiangalia kwa masikitiko Ng’ombe wa John Theodore Ghumpi aliyekatwa shoka na diwani wa kata ya Mungaa.Wa pili kushoto ni mkuu wa kituo kidogo cha polisi kata ya Mungaa  D/S/SGT Elibariki Urio.
Sehemu ya shamba la Alizeti mali ya mkulima John Theodore Ghumpi mkazi wa kijiji cha Minyinga linalodaiwa kufyekwa na diwani Matheo Alex.
Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Minyinga kata ya Mungaa waliofika nyumbani kwa John Theodore Ghumpi ambaye Ng’ombe wake sita wanadaiwa kukatwa katwa kwa shoka na diwani Matheo Alex na vijana wake wawili .Pia diwani Matheo anadaiwa kufyeka shamba la Alizeti la ekari mbili na nusu.


DIWANI wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kata ya Mungaa jimbo la Singida Mashariki, Matheo Alex amewaacha midomo wazi wapiga kura wake na wananchi wa kata hiyo kwa kitendo chake cha kukata kata ng’ombe sita kwa shoka na kufyeka ekari mbili na nusu za shamba la Alizeti .

Imedaiwa kuwa diwani huyo kijana ametenda kitendo hicho ,kutokana na ugomvi wa kugombea mbuga ya ukumbwa wa ekari 50.

Ng’ombe hao waliokatwa katwa na diwani Matheo akishirikiana na watoto wake, watatu wana mimba, wawili wananyonyesha na moja ni dume wote ni mali ya John Theodore Ghumpi mkazi wa kijiji cha Minyinga kata ya Mungaa. Ng’ombe hao na ekari la shamba la Alizeti lililofyekwa vyote vina thamani ya zaidi ya shilingi 4.5 milioni.

Tukio hilo la kusikitisha, limetokea mei 13 mwaka huu saa 5.00 asubuhi katika kijiji cha Minyinga jimbo la Singida Mashariki.

Diwani Matheo ambaye miaka miwili iliyopita aliwahi kushitakiwa katika mahakama ya hakimu mkazi mjini Singida kwa kosa la kuvunja/kuharibu kwa makusudi kizuizi (geti) la kudhibti ushuru wa mazao ya misitu na kumpiga mlinzi wa geti hilo,anatuhumiwa pia kufyeka ekari mbili na nusu za shamba la Alizeti.

Akisimulia mkasa huo wa kusikitisha, Joseph Albino (mtoto wa kaka yake mkubwa na John mwenye ng’ombe zilizokatwa) amesema siku ya tukio alipita jirani na kaya ya diwani Matheo na kukuta diwani akiwa kwenye kikao na watu wasiopungua kumi.

Akifafanua, Albino amesema alipoonwa na diwani, diwani huyo aliwaamrisha waliokuwa kwenye kikao hicho,kuwa waanze

Mtoto wa miaka 3 auawa kwa kushambuliwa na nyuki,Mtu mmoja agogwa na gari,wafanyabiashara 10 wajeruhiwa vibaya Mkoani Singida.

Kamanda mpya wa jeshi la polisi mkoa wa Singida, ACP. Geofrey Kamwela akitoa taarifa kwa waandishi wa habari (hawapo kwenye picha) juu ya matukio matatu tofauti yaliotokea Mkoani Singida.

Watu wawili mkoani Singida,wamefariki dunia katika matukio tofauti likiwemo la mtoto mwenye umri wa miaka mitatu kushambuliwa na nyuki na kusababisha kifo chake.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida, ACP Geofrey Kamwela alimtaja mtoto aliyeshambuliwa na nyuki kuwa ni Japhet Mahenda mkazi wa kijiji cha Ighombwe jimbo la Singida mashariki.

Alisema Mei 11 mwaka huu saa nne asubuhi,Japhet wakati akicheza na watoto wenzake, walianza kuua nyuki wachache waliokuwa

Kanisa la Pentekoste mkoani Singida lapiga marufuku uvaaji suruali kwa staili ya mlegezo.

 Kwaya ya Rivaivo inayomilkiwa na kanisa la Free Pentekoste Church la mjini Singida, ikitoa burudani na kuelimisha jana wakati wa ibada ya kanisa hilo.
 Jengo la kanisa la Free Pentekoste (FPCT) Tanzania tawi la Singida mjini.


Kanisa la Free Pentekoste (FPCT) Tanzania Singida mjin limepiga marufuku uvaaji wa suruali wa aina ya ‘mlegezo’ unaoacha makalio nusu uchi katika majengo ya ibada, kuanzia sasa.

Kanisa hilo limedai kuwa uvaaji wa suruali wa aina hiyo, haukubaliki mbele ya Mungu na hata kwa jamii iliyostaraabika.

Askofu wa kanisa hilo mchungaji Paulo Samwel, ametoa agizo hilo wakati akizungumza na waumini wa kanisa hilo muda mfupi kabla ya kumkaribisha mchungaji Boniface Ntandu kuhubiria waumini waliofurika kwenye kanisa hilo lililopo katikati ya mji wa Singida.

Amesema kuwa baadhi ya waumini na hasa vijana,wamejenga utamaduni wa kuvaa suruali nusu makalio wakati wakiwa kwenye

Mkuu wa Wilaya ya Singida aitisha mkutano wa hadhara kuzungumzia mradi wa umeme wa upepo.

Mwenyekiti wa kijiji cha Unyambwa manispaa ya Singida, Athumani Omari Njera akifungua mkutano wa hadhara ulioitishwa kwa ajili ya mkuu wa wilaya ya Singida (hayupo kwenye picha) kuzungumza na wananchi wa kijiji hicho kuhusu mradi wa kufua umeme wa upepo.
Mkuu wa wilaya ya Singida, mwalimu Queen Mlozi akizungumza na baadhi ya wananchi wa kijiji cha Unyambwa kuhusu mradi wa kufua umeme katika kata ya Unyambwa manispaa ya Singida.
Mkulima wa kijiji cha Unyambwa Juma Mwiru akichangia hoja ya mradi wa kufufua umeme wa upepo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kitongoji cha Ijanuka manispaa ya Singida.
Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Unyambwa waliohudhuria mkutano wa hadhara ulioitishwa na mkuu wa wilaya ya Singida, Mwalimu Queen Mlozi kuzungumza nao kuhusu mradi wa kufua umeme wa upepo.