Friday, May 17, 2013

Kanisa la Pentekoste mkoani Singida lapiga marufuku uvaaji suruali kwa staili ya mlegezo.

 Kwaya ya Rivaivo inayomilkiwa na kanisa la Free Pentekoste Church la mjini Singida, ikitoa burudani na kuelimisha jana wakati wa ibada ya kanisa hilo.
 Jengo la kanisa la Free Pentekoste (FPCT) Tanzania tawi la Singida mjini.


Kanisa la Free Pentekoste (FPCT) Tanzania Singida mjin limepiga marufuku uvaaji wa suruali wa aina ya ‘mlegezo’ unaoacha makalio nusu uchi katika majengo ya ibada, kuanzia sasa.

Kanisa hilo limedai kuwa uvaaji wa suruali wa aina hiyo, haukubaliki mbele ya Mungu na hata kwa jamii iliyostaraabika.

Askofu wa kanisa hilo mchungaji Paulo Samwel, ametoa agizo hilo wakati akizungumza na waumini wa kanisa hilo muda mfupi kabla ya kumkaribisha mchungaji Boniface Ntandu kuhubiria waumini waliofurika kwenye kanisa hilo lililopo katikati ya mji wa Singida.

Amesema kuwa baadhi ya waumini na hasa vijana,wamejenga utamaduni wa kuvaa suruali nusu makalio wakati wakiwa kwenye
nyumba za ibada.

Wakiketi kwenye viti  nguo zao za ndani (chupi), zinakuwa nje na hivyo kuwapunguzia  usikivu waumini.

Askofu Paulo amesema uvaaji huo ambao umeigwa kutoka kwenye kompyuta na sehemu zingine, kuanzia sasa usivaliwe ndani ya nyumba za ibada kwa madai kwamba unafaa zaidi katika maeneo ya soko.

Katika hatua nyingine, Askofu Paulo, alitumia fursa hiyo kuwapongeza waumini wa kanisa hilo kwa juhudi zao halali za kujijengea nyumba bora za kuishi.

Askofu huyo pia, alitumia nafasi kuwataka waumini ambao tayari wanamiliki nyumba bora, wahakikishe wanamiliki vyombo vya usafiri (magari) kwa ajili ya maendeleo yao ya kiroho na kimwili.

No comments:

Post a Comment