Saturday, May 25, 2013

Kliniki tembezi yazinduliwa wilaya ya Iramba mkoani Singida kwa lengo la kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto.

 Mganga mkuu wa wilaya ya Iramba mkoa wa Singida. Dk.Japhet Simeo akitoa taarifa yake katika hafla ya uzinduzi wa kliniki tembezi katika wilaya hiyo yenye lengo la kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto.Uzinduzi huo umefanyika katika zahanati ya kata ya Ndago wilaya ya Iramba.
 Mkuu wa wilaya ya Iramba Yahaya Nawanda, akizungumza kwenye uzinduzi uliofana  wa kliniki tembezi inayotarajiwa kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto.Kushoto ni mkuu wa wilaya ya Singida,mwalimu Queen Mlozi na kulia ni mkuu wa wilaya ya Manyoni, Fatuma Toufiq.
 Mkuu wa wilaya ya Iramba mkoa wa Singida,Yahaya Nawanda (kulia) akizindua kliniki tembezi kwa wilaya hiyo, kwa kupima mama mjamzito Mary Kiula.
 Mkulima wa kijiji cha Sinziligi kata ya Ndago wilaya ya Iramba,Michael Mguna akisaidiwa kubeba mtoto wake Leonard na mama mmoja ambaye sio mke wake.Michael alidai kuwa mke wake alibanwa na shughuli za nyumbani na hivyo yeye akalazimika kumpekeka mtoto wao kliniki kwa mujibu wa ratiba.Mkuu wa wilaya ya Iramba,Yahaya Nawanda amewataka wanaume wote kujenga utamaduni wa kuwasindikiza wake zao kwenda kliniki.

Baadhi ya akina mama wajawazito na wasio wajawazito wa kata ya Ndago wilaya ya Iramba,waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa kliniki tembezi wilayani humo.Kliniki hiyo, imedaiwa kuwa ni ya kwanza hapa nchini.

No comments:

Post a Comment