Thursday, February 21, 2013

Naibu Waziri wa TAMISEMI ataka watendaji wa vijiji Singida kufanya kazi ya kuandikisha wanafunzi wa madarasa ya awali na msingi.

 Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Kassim Majaliwa (Mb), akizungumza na walimu wakuu wa shule za sekondari mkoa wa Singida na baadhi ya watendaji wa sekta ya elimu. Mazungumzo hayo ambayo yalikuwa ni pamoja na kuweka mikakati ya kuinua taaluma mkoani Singida yamefanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa mjini Singida. Kushoto ni kaimu mkuu wa mkoa wa Singida ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Ikungi, Manju Msambya na Kulia ni katibu tawala mkoa wa Singida, Liana Hassan.
Baadhi ya walimu wakuu wa shule za sekondari mkoa wa Singida wakimsikiliza kwa makini Mh. Kassim Majaliwa (hayupo kwenye picha).

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Kassim Majaliwa, amesema kuanzia sasa kazi ya kuandikisha wanafunzi kuanza madarasa ya awali na yale ya msingi, itafanywa na watendaji wa vijiji na si walimu wakuu wa shule za msingi.
 Majaliwa amesema hayo wakati akizungumza na walimu wakuu wa shule za sekondari na baadhi ya viongozi wa sekta ya elimu mkoani Singida.
Amesema kutokana na

Polisi mkoani Singida yakamata kilo 10.5 za Bangi na watuhumiwa wawili watiwa mbaroni.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida ACP, Linus Sinzumwa.

Jeshi la polisi mkoa wa Singida limefanikiwa kukamata bunda 30 na misokoto 3,000 ya madawa ya kulevya aina ya bangi ambayo ni sawa na kilo 10.5.
Akizungumza na Singida Yetu Blog kwa njia ya simu, Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida ACP Linus Sinzumwa, amesema kuwa bangi hiyo imekamatwa Februari 16 mwaka huu saa saba mchana ikiwa imehifadhiwa nyumbani kwa Williamu Kajuna (43) mkazi wa maeneo ya Mwenge mjini Singida.
Amesema kuwa baada ya kupata taarifa kutoka kwa

Wakulima mkoani Singida wanufaika kwa msaada wa majembe ya kukokotwa na Ng’ombe yaliyotolewa na Mh.Dewji.

 Baadhi ya wakulima wa jimbo la Singida mjini, wakinufaika na msaada wa majembe ya kukokotwa na Ng’ombe uliotolewa na mbunge wa jimbo hilo, Mohammed Gullam Dewji hivi karibuni.

Friday, February 15, 2013

Wakulima watatu wanusurika kuuawa mkoani Singida kufuatia ugomvi wa shamba

Mkulima John Leonard Njiku akiwa amelazwa katika wodi namba tatu katika hospitali ya mkoa mjini Singida baada ya kuvamiwa akiwa shambani na wenzake  wawili. Njiku amedai kuwa uvamizi huo unachangiwa na ugomvi wa kugombe shamba kati yake na Dk. Damas Simbu aishiye Dar-es-salaam.

 Wakulima watatu wakazi wa kijiji cha Ughaugha (b) manispaa ya Singida, wamenusurika kuuawa baada ya kuvamiwa na watu wanaokadiriwa kuwa 12 wakiwa shambani na kushambuliwa kwa majembe kwa kile kilichodaiwa kuwa ni ugomvi wa kugombea shamba.
Wakulima hao waliovamiwa

SAMMAYUNI WA SINGIDA AONESHA UKATILI ULIOKITHIRI

Jeraha la Mwanamke (30) aliyeunguzwa pasi ya umeme na mumewe mjini Singida.

Jeshi la polisi Mkoani Singida linamshikilia mtu mmoja Baltazar Mushi Sammayuni (33), kwa tuhuma ya kumuunguza mkewe usoni, kwa kutumia pasi ya umeme wakati akiwa amelala usiku wa manane nyumbani kwao.
Kaimu kamanda wa polisi mkoani Singida Thobias Sedoyeka amesema tukio hilo la kusikitisha lilitokea siku ya

Mkuu wa mkoa wa Singida aagiza waalimu wakuu wakajifunze matumizi ya fedha kwa mwalimu mkuu mwenzao

 Mkuu wa mkoa wa Singida Dk.Parseko Kone akizungumza na baadhi ya walimu wa shule ya sekondari Mwanzi Manyoni mjini.Dk.Kone hakufurahishwa na hali duni ya ofisi ya mkuu wa shule hiyo wakati shule ikiwa na akiba ya zaidi ya shilingi milioni sita.
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi mchanganyiko Ikungi wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Olivary Kamili akiwa ofisini kwake akitekeleza majukumu yake. Mkuu wa mkoa wa Singida Dk.Parseko Kone ameagiza walimu wakuu wa shule za msingi na wakuu wa sekondari wafike shule ya msingi mchanganyiko Ikungi, ili wakajifunze juu ya matumizi bora ya fedha za Umma.

Kutoweka kwa mashahidi wa mashitaka kesi inayowakabili vigogo wa CHADEMA Singida kwasababisha kesi kuahirishwa

 Mshitakiwa wa kwanza katika kesi ya kumtolea lugha ya matusi mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi Mwita Waitara Mwakibe akitoka nje ya mahakama ya hakimu mkazi mjini Singida baada ya kesi yao kuahirishwa leo, Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 11 mwaka huu,baada ya mashahidi wa upande wa mashitaka kuingia mitini.
Wakili wa washitakiwa vigogo wa CHADEMA Onesmo Kyauke (katikati) akiwaeleza jambo wateja wake muda mfupi baada kesi ya wateja wake kuahirishwa hadi Machi 11 mwaka huu.Vigogo hao wanaoshitakiwa kwa kumtolea

Jaji Laurance Kaduri azindua vikao vya mahakama Singida

 Jaji Laurance Kaduri wa mahakama kuu kanda ya Dodoma akikagua gwaride la kuashiria kuanza kwa vikao vya mahakama hiyo vitakavyochukua mwezi mmoja kuanzia leo (11/2/2013).Vikao hivyo vinaendelea  katika mahakama ya hakimu mkazi mjini Singida.

Kikosi cha askari 50 wa kutuliza  ghasia mjini Singida kikitoa heshima kwa jaji Laurance Kaduri.

Mbunge wa jimbo la Singida mjini Mohammed Dewji atoa msaada wa baiskeli kwa walemavu

 Mbunge wa jimbo la Singida mjini Mh. Mohammed Gullam Dewji akizungumza na mmoja kati ya walemavu watano aliowakabidhi baiskeli za magurudumu matatu kwa ajili ya kuwasaidia kumudu maisha yao hivi karibuni.Pamoja na msaada wa baiskeli hizo, Dewji pia alitoa msaada wa Wheel Chair 24 kwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Singida.Thamani ya msaada huo ni zaidi ya shilingi milioni 14.
Mbunge wa jimbo la Singida mjini, Mohammed Gullam Dewji ametoa msaada wa viti 24 maalum vya wagonjwa (wheel chairs) vyenye thamani ya zaidi ya shilingi 24 milioni, kwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Singida.
Pamoja na viti hivyo mbunge huyo ametoa msaada wa baiskeli za magurudumu matatu kwa walemavu watano wa jimboni kwake.
Akizungumza kwenye makabidhiano ya msaada huo, Dewji amesema msaada huo ni mwendelezo wa misaada mbalimbali anayoitoa jimboni kwake, kwa ajili ya kusaidiana na serikali kuboresha huduma mbalimbali zikiwemo za sekta ya afya.
Alisema ana aimani kwamba

Matembezi ya mshikamano katika kuadhimisha miaka 36 ya kuzaliwa CCM yafana mkoa wa Singida

 Makamu wa pili wa rais Zanzibar na mlezi wa CCM mkoa wa Singida, Balozi Seif Idd (mwenye kofia) akishiriki matembezi ya mshikamano ya CCM mkoa wa Singida,yaliyofanyika leo kama sehemu ya maadhimisho ya CCM kutimiza miaka 36 toka kianzishwe.Mwenye bukta ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida Mgana Msindai na wa pili kulia ni mke wa balozi Seif.
 Mlezi wa CCM mkoa wa Singida, Balozi Seif Idd (wa tatu kushoto) akishiriki matembezi ya CCM ya  kilometa tano ya mshikamano yaliyofanyika mjini Singida leo.Mwenye truck suit ya blue ni mkuu wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Kone na wa pili kulia ni mke wa Balosi Seif Idd.Wa pili kushoto ni mbunge wa jimbo la Manyoni mashariki, John Chiligati.
 Mkuu wa mkoa wa Singida Dk.Parseko  Kone,( wa tatu kulia) akishiriki matembezi ya mshikamano ya CCM yakiwa ni sehemu ya maadhimisho ya CCM kutimiza miaka 36 toka kizaliwe.Wa pili kulia ni MNEC manispaa ya Singida, Hassan Mazala.Wa kwanza kulia ni mkuu wa wilaya ya Mkalama, Edwerd Ole Lenga na anayefuatia ni mbunge wa jimbo la Manyoni mashariki, John Chiligati.
 Mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Kone (mwenye truck suit ya blue) akiongoza wanaCCM kufanya mchakamchaka kwenye matembezi ya mshikamano ya CCM mkoa wa Singida.
 Katibu wa CCM mkoa wa Singida, Naomi Kapambala ( wa mbele) akiongoza kuimba nyimbo za uhamasishaji kwa wanaCCM walioshiriki matembezi ya mshikamano mbele ya ofisi ya CCM mkoa wa Singida.