Wednesday, January 8, 2014

Halmashauri ya Ikungi kukusanya Tsh 25.6 bilioni 2014/2015.

 Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida, Bw. Protace Magayane,akitoa ufafanuzi wa jambo katika kikao maalum cha Madiwani kwa ajili ya kupitisha bajeti ya halmashauri hiyo ya mwaka wa fedha wa 2013/2014 jana.Wa pili kushoto walioketi ni mkuu wa wilaya ya Ikungi, Manju Msambya na anayefuata ni mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Bw. Selestin Yunde.’
 Mbunge wa viti maalum (CHADEMA) mkoa wa Singida, Bw. Christo Waja akichangia hoja kwenye kikao maalum cha Madiwani kilichokuwa kikipitisha bajeti ya mwaka ujao wa halmashauri hiyo.Kikoa hicho kilipitisha mapendekezo ya bajeti ya zaidi ya bilioni 25.
Diwani wa kata ya Ikungi (CCM) wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida, Bw. Haji Mukhandi akichangia hoja katika kikao maalum cha bajeti ya halmashauri ya wilaya ya Ikungi kwa mwaka wa fedha ujao.
Diwani wa viti maalum (CCM) kata ya Ikungi, Bi. Asha Munjori, akitoa uchangia mapendekezo ya bajeti ya halmashauri ya Ikungi ya mwaka wa fedha wa 2013/2014 kwenye kikao maalum cha Madiwani.

HALMASHAURI ya wilaya ya Ikungi mkoani Singida inatarajia kukusanya zaidi ya shilingi bilioni 25.6 kutoka kwenye vyanzo vyake mbalimbali vya mapato  katika mwaka wa fedha wa 2014/2015.

Hayo yamesemwa hivi karibuni na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo,Ally Nkhangaa wakati akiwasilisha mapendekezo ya bajeti kwa mwaka ujao wa fedha.

Amesema zaidi ya shilingi 723 milioni zitatoka kwenye vyanzo vya mapato vya halmashauri yenyewe na zaidi ya shilingi 336 milioni ni ruzuku kutoka serikali kuu ikiwa ni fidia ya kodi na ushuru uliofutwa.

Nkhangaa amesema wanatarajia kupatiwa ruzuku na serikali kuu zaidi ya shilingi 15.4 bilioni kwa ajili ya kulipia mishahara ya watumishi wa umma.

“Serikali kuu pia itatupatia ruzuku ya zaidi ya shilingi 1.9 bilioni kwa ajili ya kugharamia matumizi yasiyo ya mishahara na ruzuku nyingine ya zaidi ya shilingi 7.5 bilioni kwa matumizi ya kugharamia miradi ya maendeleo ya wananchi”,amesema.

Nkhangaa ambaye ni Diwani wa kata ya Ntunduu (CCM), alitaja baadhi ya mambo yaliyozingatiwa katika bajeti ni kuandaa mpango mkakati wa halmashauri wa miaka mitano kwa kuzingatia dira ya maendeleo ya kitaifa ya 2025 na ilani ya uchaguzi ya chama tawala.

Alitaja mambo mengine yaliyozingatiwa kuwa ni upimaji wa viwanja makao makuu ya wilaya Ikungi na mpango wa matumizi bora ya ardhi katika vijiji na kujenga ofisi ya halmashauri, nyumba ya Mkurugenzi Mtendaji, nyumba za watumishi na ununuzi wa samani za ofisi.

“Pia bajeti hii imezingatia kuongeza

uzalishaji katika kilimo kwa kukarabati skimu za umwangiliaji na kushirikisha wakulima katika uzalishaji wa mbegu bora, uboreshaji wa miundo mbinu ya barabara na maji”,alifafanua Nkhangaa.

No comments:

Post a Comment