Wednesday, January 8, 2014

Majambazi yalioua askari yajulikana.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida, SACP Geofrey Kamwela, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na tukio la kujulikana kwa Majambazi yaliyoua askari mkoani Singida.

WATU Wanne wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wakazi wa Majengo Itigi tarafa ya Itigi wilaya ya Manyoni Mkoa wa Singida waliouwa askari wakati wa kurushiana risasi majina yao yamekwisha fahamika.

 Majambazi hayo yanadaiwa Desemba 21 mwaka huu saa 4.30 usiku huko katika kijiji cha Tambuka reli kata ya Majengo tarafa ya Itigi wilayani Manyoni yalimuuawa askari polisi D.6466 D/SGT Zakaria Williamu (43),baada ya kumpiga risasi shingoni.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Singida, SACP Geofrey Kamwela alitaja majina ya majambazi hayo kuwa ni Joseph Hamed (21) mkulima na mkazi wa kijiji cha Siuyu wilaya ya Ikungi.

 “Wengine ni Juma Ramadhani (20) mkulima na mkazi wa Kizota Dodoma,Abdallah Hamisi (21) mkulima na mkazi wa kitongoji cha Milera wilaya ya Ikungi na Stanley Mpaki @ Babu Mpaki (28)”amesema.

Kamwela amesema watu hao walikamatwa nyumbani kwa mtuhumiwa Stanley Mpaki ambaye ni mfanyabiashara.

 “Askari polisi waliokuwa kwenye doria siku ya tukio,walipata taarifa kutoka kwa raia wema kuwa ndani ya nyumba ya mfanyabiashara Stanley,kuna majambazi yamejificha humo,haraka walifika kwenye nyumba hiyo na baadhi waliingia ndani na kumwacha D/SGT Zakaria akiwa nje na alipigwa risasi ya shingoni na kufariki papo hapo”,amesema Kamwela kwa masikitiko.

Amesema katika eneo hilo la tukio,bunduki aina ya

SMG no.UA 16071992 na risasi zake 25 na bastola iliyotegenezwa kienyeji yenye uwezo wa kutumia risasi za shotgun zilikamatwa.

 “Uchunguzi juu ya tukio hilo,unaendelea na baada ya uchuguzi kukamilika,watuhumiwa watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili”,amesema.


No comments:

Post a Comment