Wednesday, February 26, 2014

Halmashauri ya Singida yatumia shilingi 89 milioni kugharamia ujenzi wa soko.

Naibu waziri Fedha na Uchumi na Mbunge wa jimbo la Iramba magharibi, Lameck Nchemba Mwigullu, akizindua jengo la soko la kisasa la kijiji cha Old Kiomboi wilaya ya Iramba.

HALMASHAURI ya wilaya ya Iramba mkoani Singida imetumia zaidi ya shilingi 89 milioni kugharamia ujenzi wa soko la kisasa la kijiji cha Old Kiomboi.

Hayo yamesemwa na Afisa Mtendaji wa kijiji cha Old Kiomboi,Betha Nakomolwa wakati akitoa taarifa yake kwa Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi na Mbunge wa jimbo la Iramba magharibi,Lameck Nchema Mwigulu aliyezindua soko hilo.

Amesema katika fedha hizo,nguvu kazi ya wanaqnchi,imeokoa zsaidi ya shilingi 8.9 milioni.

Aidha,Nakomolwa amesema Mwigulu amechangia shilingi 7,200,600,mchango wa kijiji (CDG) shilingi 28,550,000,Tasaf awamu ya kwanza hadi ya nne,shilingi 44,379,700 na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida,shilingi laki nne.

Katika hatua nyingine,Afisa Mtendaji huyo,amesema ujenzi wa matundu matatu ya choo cha soko hilo ambao unatarajiwa kugharimu shilingi milioni
10,upo katika hatua ya kukamilika.

“Kwa ujumla shughuli za ukamilishaji wa ujenzi wa soko la jamii kijiji cha Old Kiomboi,zimekamailika japo kuna mapungufu madogo madogo kama kuweka umeme na kenopu ambayo hayazuii kufanyika kwa uzinduzi wa soko hili”,amesema Nakomolwa.


Baada ya kuzindua soko hilo,pamoja na mambo mengine,Mwigulu ameahidi kuhakikisha kushirikiana na wananchi katika kuweka umeme, kenopu na ujenzi wa choo,unamalizika mapema iwezekanavyo.

No comments:

Post a Comment