Wednesday, February 5, 2014

Shirika lisilo la kiserikali latumia shilingi 1.5 bilioni kwenye miradi

Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la Health Actions Promotion Association (HAPA) la mjini Singida,David Mkanje akiwa ofisini kwake akitekeleza majukumu yake.

SHIRIKA lisilo la kiserikali la Health Actions Promotion Association (HAPA) limetumia zaidi ya shilingi 1.5 bilioni katika kutekeleza miradi miwili mkoani hapa katika kipindi cha kuanzia janauari hadi desemba mwaka jana.

Miradi hiyo ni wa ushiriki sawa wa wanaume katika afya ya uzazi na jinsia (TMEP), uliofadhiliwa na shirika la RFSU la nchini Sweden kwa zaidi ya shilingi bilioni moja.

Mradi mwingine ni ule wa Pamoja Tunaweza (UFBR) ambao umefadhiliwa na shirika la SIMAVI la nchini Uholanzi, kwa kiasi cha shilingi milioni mia tano.

Hayo yamesemwa hivi karibuni na Mkurugenzi wa HAPA,David Mkanje alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake juu ya shughuli zilizofanywa na shirika hilo kongwe, kwa kipindi cha mwaka jana.

Kuhusu mradi wa ushiriki sawa wa wanaume katika afya ya uzani na jinsia,Mkanje amesema kuwa kata 21 za wilaya ya Manyoni,zimenufaika na maradi huo.

“Kwa upande wa manispaa ya Singida,jumla ya kata 13 ns Singida vijijini kata 28 nazo zimenufaika na mradi huo”,amesema na kuongeza kwa kusema;

“Mradi huu ni wa uhamasishaji kuhusu masuala ya afya ya uzazi na jinsia,ambapo wanaume wanalengwa kuwa chachu ya mabadiliko katika kuhakikisha matatizo yatokanayo na uzazu,yanakwisha”alifafanua Mkurugenzi huyo.

Katika hatua nyingine,Mkanje amesema kuwa mradi wa Pamoja Tunaweza (UFBR), umetekelezwa kwenye wilaya ya
Iramba kwa tarafa ya Ndago,na Mkalama katika tarafa za Kirumi na Nduguti.


“Lengo kuu la mradi huu,ni kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto walio chini ya umri wa miaka mitano.Mengine ni kuhakikisha elimu ya afya ya uzazi inaenea kwenye jamii yote.Kupunguza unyanyasaji wa kijinsia na jamii kujua haki zao hasa kwenye suala la afya ya uzazi”,amesema Mnkaje.

No comments:

Post a Comment