Friday, April 4, 2014

Singpress yapata katibu mtendaji mpya.

Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari (Singpress) mkoa wa Singida, Seif Takaza akifungua mkutano mkuu wa kawaida wa klabu hiyo uliofanyika mjini Manyoni mwishoni mwa wiki.Kulia ni makamu mwenyekiti Damiano Mkumbo na kulia ni kaimu katibu mtendaji,Emmanuel Michael.
Baadhi ya wanachama wa klabu ya waandishi wa habari (Singpress) mkoa wa Singida,wakifuatilia mkutano mkuu wa kawaida wa (mwaka 2013) klabu hiyo uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa kanisa Katoliki mjini Manyoni.

KLABU ya waandishi wa habari (Singpress) mkoa wa Singida imemchagua kwa kishindo Pascal Tantau (32),kuwa katibu wake mtendaji kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Abby Nkungu ambaye anadai kwa sasa afya yake ina mgogoro.

Pascal kijana aliyemaliza chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) alipata kura 15 za ndio,mbili zilimkataa na moja iliharibika.

Pascal atakuwa madarakani hadi mwishoni mwakwani (2015) uchaguzi mkuu utakapofanyika kwa mujibu wa katiba ya klabu hiyo.

Pascal aliwashukuru wanachama wenzake kwa kumwamini na kumkabidhi nafasi hiyo nyeti. Ameahidi kwamba atawatumikia kwa nguvu zake zote na kwa maarifa lengo kuu ikiwa ni  klabu hiyo iweze kupaa kimaendeleo katika kipindi chake cha uongozi.

“Niwaahidi pia kwamba katika uongozi wangu nitatumia mbinu shirikishi ili kila mwananchama aweze kutoa mchango wake mbalimbali kuendeleza klabu na kuboresha ustawi wa wananchama.Nitajitahidipia kuhakikisha klabu inakuwa na mahusiano mazuri na wadau wake mbalimbali”, alisema kwa kujiamini.

Abby Nkungu amelazimika kujiuzulu nafasi ya ukatibu mtendaji wa Singpress,kwa madai kwamba ameagizwa na daktari wake aishiye nchini
Kenya, kuwa asifanye kazi yoyote ambayo atalazimika kutumia akili nyingi.

Ilielezwa mbele ya mkutano huo mkuu, kwamba Nkungu aliweza kuombwa na kamati tendaji kusaidia kuandaa maandalizi ya mkutano mkuu,alikataa kata kata.

Hata alipoitwa tena na kamati tendaji ili aweze kufafanua zaidi juu kutakiwa na daktari wake awe kwenye mapumziko yasiyo na bughudha yo yote…yaani ‘total rest’,wakati anaendelea na kazi kama kawaida zikiwemo za safari ndefu pia alitupilia mbali wito huo.

Kutokana na hali hiyo mkutano mkuu huo umeazimia Nkungu asigombee tena uongozi wowote katika klabu ya Singpress kwa muda wote wa maisha yake yaliyobaki.Pia amesimamishwa uanachama kwa kipindi cha miezi tisa.


Hii ni mara ya pili,Nkungu kusimamishwa uanachama wa klabu ya Singpress.

No comments:

Post a Comment