Monday, July 21, 2014

NSSF, Singida yatumia Bilioni 1.52 kukopesha vikundi sita vya wajasiriamali.


Meneja wa shirika na hifadhi ya jamii NSSF, Magreth Mwaipeta akizungumza na wanachama wa kikundi cha Aminika gold Mine Ltd cha Sambaru Wilaya ya Ikungi, Singida.

Mwenyekiti wa chama cha ushirika cha Aminika Francis Mbasha akizungumza kwenye mkutano baina ya wanakikundi na NSSF.  

Meneja wa NSSF Mkoa wa Singida Magreth akizungumza na wajumbe wa bodi pamoja na wanachama wa kikundi cha Aminika cha Sambaru Wilayani Ikungi.

Wanachama wa chama cha Aminika Gold Mine wakiwa kwenye ukumbi wa ofisi ya madini wakati wa semina ya uhabarisho.

Makamu Mwenyekiti wa chama cha ushirika cha Aminika akisisitiza jambo kwa wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi nje ya ukumbi wa madini Singida mjini.
Wanachama wa chama cha Aminika Gold Mine wakimsikiliza meneja wa NSSF Mkoa wa Singida.

MFUKO wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), umetumia zaidi ya shilingi bilioni 1.52 kwa ajili ya kuvikopesha vyama  sita vya ushirika Mkoani Singida.

Hayo yamebainishwa jana mjini hapa na Meneja wa NSSF Mkoa wa Singida, Magreth Mwaipeta wakati akizungumza kwenye semina ya uhabarisho baina ya shirika la kikundi cha wachimbaji wa madini ya dhahabu cha Aminika Gold Mine cha kijiji cha Sambaru Wilayani Ikungi.

Mwaipeta alisema mikopo hiyo imetolewa kwa riba nafuu kwa vikundi hivyo ili waweze kujikwamua kutokana na umaskini iongoni mwao.

Aidha alivitaja vikundi hivyo vilivyopewa mkopo na kiasi cha fedha kwenye mabano kuwa ni kuwa ni Veta Singida (milioni 500), Mtinko (milioni 164), Amani Manyoni (milioni 223), Kumekucha Itigi (milioni 50) ,Tumaini (89) milioni na Ndago cha Wilayani Iramba( milioni 500).

Alisema vikundi hivyo vimepata mikopo hiyo baada ya
kukidhi masharti ya shirika hilo ikiwa ni pamoja na amana za chama asilimia hamsini,ambapo kiwango cha chini kukopa ni shilingi milioni 50 na cha juu ni bilioni moja.

Meneja huyo alikuwa akijibu swali aliloulizwa na mwanakikundi cha Aminika,Hillary Shoo, aliyetaka kujua shirika hilo mpaka sasa limekopesha vikundi vingapi kuanzia mwezi Januari mwaka huu mpaka hivi sasa.

Mapema Mwenyekiti wa chama cha ushirika cha Aminika Francis Mbasha alisema lengo la chama kukutana na NSSF ni ili kupata elimu ya namna ambavyo kikundi hicho kinaweza kunufaika na mikopo inayotolewa na shirika la NSSF.

No comments:

Post a Comment