Thursday, July 17, 2014

PICHA 10 ZA YALIYOJIRI KWENYE SHINDANO LA MISS SINGIDA 2014

Huyu ndiye Miss Singida 2014 Doris Mole (23) akiwa na mshindi wa pili Blath Chambo na mshindi wa tatu Lulu Abdul.
Mgeni rasmi mama balozi Seif Idd akimkabidhi fedha kiasi cha shilingi laki tano Miss Singida.
 Warembo waliofanikiwa kuingia tano bora ya Miss Singida 2014.

 Majaji wakiwa Kazini kwa makini.
Miss Singida akipita mbele kusalimia mashabiki wa ulimbwende mara baada ya kutangazwa mshindi.
 Miss Singida akicheza muziki na mgeni rasmi.
 Mamiss wenzake wakifurahia pamoja na mshindi Doris Molel.
 Mameneja wa Coca Cola ambao nao walidhamini shindano hilo.

Mke wa Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Iddy mama Assa akizungumza kwenye shindano la kumtafuta Miss Singida 2014.
Mama wa Mipasho Khadija Kopa akifanya vitu vyake jukwaani kabla ya kuanza shindano hilo.

Doris Molel (23) Mwanafunzi katika chuo cha Kumbukumbu cha Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salam anayesomea siasa na Maendeleo ya Jamii mwaka wa tatuametwaa taji la Miss Singida Redds 20014.

Katika shindano hilo lililofanyika jana kwenye ukumbi wa chuo ha Uhazili Mjini hapa Molel, mbali na kutwaa taji hilo alijinyakulia kitita cha shilingi laki tano.

Nafasi ya pili ilichukuliwa na Blath Chambo ambaye aliambilia kiasi cha shilingi laki tatu huku mshindi  wa tatu Lulu Abdul akipata shilingi laki mbili.


Shindano hilo lilipambwa na wasanii mbalimbali akiwemo mama wa mipasho na taarabu, Hadija Kopa na wasanii mbalimbali wa Bongo Flava.

Mapema mgeni rasmi Mke wa Makamu wa Pili wa Zanzibar Assi Balozi Seif Iddy aliwataka washiriki wa mashindano hayo ya ulimbwende hapa nchini kujitambua, kusoma na kujiwekea malengo maalum.

Aidha aliwataka wasidanganyike na kujiona kuwa wao ni bora na hivyo kufanya vitendo viovu vinavyoweza kuhatarisha maisha yao ikiwa ni pamoja na kijiingiza katika mapenzi mapema.


Katika kumuunga mkono muandaaji wa shindano hilo Mkoani Singida, Bora Lemmy Mama Seif Iddi alimpatia kiasi cha shilingi laki sita ili aweze kuongezea washindi zawadi.

No comments:

Post a Comment