Thursday, August 21, 2014

Halmashauri ya manispaa ya Singida yaweka taa kandokanodo ya barabara zake kuimarisha ulinzi.

Halmashauri ya manispaa ya Singida, yaweka taa kando kando ya barabara zake katika kuimarisha ulinzi na kupendezesha mji.
Taa hizo ambazo katika awamu ya kwanza zimewekwa kwenye barabara ya Arusha inayoanzia Bomani hadi nyumba za kulala ya Victoria karibu na Mwenge sekondari na ile ya Karume Arusha, zote zikiwa na urefu wa kilometa 2.720

Halmashauri ya manispaa ya Singida, imeweka taa kando kando ya barabara zake za mjini Singida zenye urefu wa kilometa 2.72, pamoja na mengine, kuimarisha ulinzi nyakati za usiku.

Taa hizo za kisasa ambazo zinatarajiwa kuanza kutumika wakati wo wote kuanzia sasa, pia mradi huo unatarajiwa  kuongeza mapato ya ndani ya halmashauri hiyo.

Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Joseph Mchina, alisema mradi huo unatekelezwa na kampuni ya masoko ya Angencies Tanzania Ltd, umeanza Mei mwaka huu, baada ya mkataba kusainiwa na pande zote mbili.

Alisema kwa kuanzia taa hizo zimewekwa kuanzia, Bomani barabara ya Arusha hadi nyumba ya kulala ya Victoria yenye urefu wa kilometa mbili, na barabara ya Karume – Arusha yenye urefu wa mita 720.

Akifafanua, alisema kampuni hiyo itagharamia shughuli zote za huduma hiyo ya mradi huo.

“Pia itaweka
matangazo ya biashara kwenye milingoti ya taa hizo yatakayoingizia mapato kampuni hiyo.  Kutokana na mapato hayo, kampuni hiyo italipa ushuru wa mapato kwa manispaa yetu. Kwa hiyo manispaa tumepata chanzo kingine kipya cha kutuingizia mapato ya uhakika”,alisema Mchina kwa kujiamini.

Aidha, Mkurugenzi huyo  alisema taa hizo zinazotegemewa kuwashwa wiki hii, licha ya kupendezesha mji wa Singida, zitachangia wafanyabiashara kuongeza muda wa kufanya biashara, na hivyo kujiongezea mapato.

“Katika awamu ya pili, tunatarajia taa hizo kuwekwa kwenye barabara ya Mwanza na ile iendayo VETA kupitia Ikulu ndogo” alisema Mkurugenzi huyo.

Manispaa ya Singida imewahi kuwa na taa za barabarani mara baada ya Tanzania kupata uhuru,lakini ilitoweka miacha michache toka ianzishwe.

No comments:

Post a Comment