Tuesday, September 16, 2014

MO apata wapinzani Chadema.

WANACHAMA watatu wa Chama Cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA) mkoa wa Singida, inadaiwa wameonyesha nia ya dhati kumng’oa Mbunge wa jimbo la Singida Mohammed Gullam Dewji, katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwakani.

Wanachama hao ambao inadaiwa wana uwezo mkubwa wa kulipaisha kimaendeleo jimbo hilo ni aliyewahi kuthubutu kumwangusha Dewji kwenye uchaguzi mkuu uliopita na kuangukia pua, Josephat Isango (kwa sasa ni mwandishi wa habari wa gazeti la Tanzania daima).

Katika uchaguzi mkuu wa chama hicho uliofanyika juzi, Josephat Isango ambaye alikuwa akiomba nafasi ya uenyekiti wa mkoa, aliambulia kura mbili, wakati mshindi Shaban Limu akizoa kura 74.

Wengine ni Vicent Mughwai (mdogo wake na mbunge Tundu Lissu) na Selemani Majindu.

Wanachama hao walitangaza nia zao hizo kwenye mkutano mkuu wa uchaguzi wa chama hicho uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Cheyo Clief,mjini Singida.

Kwa upande wa jimbo la Singida kaskazini linaloshikiliwa na Waziri wa Maliasili ya Utalii, Lazaro Nyalandu,wanachama wa
CHADEMA Emanueli Jingu, David Jumbe na Dk.Samweli Mwanja,inadaiwa wameonyesha nia ya kumtoa Nyalandu.

Jimbo la Iramba mashariki linalowakilishwa na Salome Mwambu, linawaniwa na Elia Gundana  Osca,George Gunda na   Alex Kapalale,

Katika hatua nyingine, mkutano mkuu CHADEMA mkoa uliofanyika juzi, umemchagua  Shabani Limu, kuwa mwenyekiti wa mkoa baada ya kuzoa kura 74 na kuwagaragara  wapinzani wake Jese John Msonsa aliyepata kura tano na  Josephath Isango,ameambulia  kura mbili tu.

Nafasi ya katibu ilinyakuliwa na  Patrick Msuta kwa kura 43 na kuendelea kushika nafasi ya katibu wa chama hicho baada ya kuwashinda  Malongo Nguli kwa kuwa na kura 29 na Didasi Philemoni Mwekwa aliyekuwa na kura tisa.

No comments:

Post a Comment