Tuesday, September 2, 2014

Waandishi waaswa kuhimiza Afya ya Uzazi na Jinsia.

Mratibu wa TACAIDS mkoa wa Singida, Fedes  Mdala, akizindua uhamasishaji wa masula ya ushiriki sawa wa masuala ya Afya ya Uzazi na Ujinsia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Mandewa mjini Singida.
Mratibu wa shirika lisilo la kiserikali la YMC la mjini Singida, Fidelius Yunde, akihamasisha wananchi wakiwemo vijana na wanaume wa Mandewa mjini Singida, umuhimu wa ushiriki sawa wa wanaume katika masuala ya afya ya uzazi na ujinsia.
Kikundi cha uhamasishaji cha YMC cha mjini Singida, kikitoa burudani ya sarakasi kwenye mkutano wa hadhara  uliofanyika katika viwanja vya  Mandewa mjini Singida kwa ajili ya kuhamasisha na kuelimisha wanaume kushiriki masuala ya afya ya uzazi na ujinsia.

Baadhi ya vikaragosi vinavyotumiwa na shirika la YMC kutoa ujumbe/kuhamsisha wanaume kushiriki kikamilifu masuala ya afya na uzazi na ujinsia kwa mkoa wa Singida.
Kikundi cha burudani cha YMC maarufu ‘mtaa wa saba’,wakitoa burudani kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja wa Mandewa Singida mjini,ulioitishwa kwa ajili ya kuhamasisha na kuelimisha wanaume kushiriki masuala ya afya ya uzazi na ujinsia.

WAANDISHI wa habari mkoa wa Singida,wamehimizwa kutumia kalamu zao vema kuwaelimisha wanaume juu ya umuhimu wa kushiriki kikamilifu katika masuala ya usawa wa afya ya uzazi na ujinsia,ili kuharakisha upatikanaji wa mabadiliko kwa upande wa wanaume waweze kushiriki ipasavyo. Kitendo hicho kitasaidia kuimarisha afya za wanawake na watoto.

Changamoto hiyo imetolewa na Mratibu wa TACAIDS Mkoa wa Singida, Fedes Mdala, alipozungumza na wakazi wa Mandewa mjini Singida waliohuduhuria mkutano wa hadhara ulioitishwa na shiriki la YMC, kwa ajili ya kuhamasisha ushiriki sawa kwa wanaume katika masuala ya afya ya wanawake na ujinsia (TMEP).


Alisema utamaduni wa wanaume uliopitwa na wakati wa kudhani kwamba suala la kujadiliana na wenza wao juu ya uzazi wa mpango,kuwasindikiza kliniki, kupika, kufua nguo zikiwemo za watoto na kuchota maji ni kitu kisichokubalika kwa upande wao,umechangia kwa kiasi kikubwa kudhoofisha afya za wanawake na watoto.

Ili  kuondoa dhana hiyo potofu,Mdala alisema waandishi wa habari wana nafasi kubwa kuutokomeza kabisa  utamaduni huo, kwa kuhamasisha na uelimisha wanaume, kwamba wana wajibu wa kutoa ushiriki sawa katika masuala ya afya ya uzazi na ujinsia.

“Waandishi wa habari wakijikita katika kuandika habari au makala zitakazoeleza au kuelimisha kwa kina,juu ya madhara yanayopatikana kutokana na wanaume kutoshiriki kikamilifu masuala ya afya ya uzazi na ujinsia. Wakati huo huo wakabainisha faida zitakazopatikana kutokana na wanaume kuwa mstari wa mbele katika kushiriki kikamilifu masuala ya afya ya uzazi na ujinsia,nina uhakika kwamba afya za wanawake na watoto,zitaboreka zaidi”,alifafanua.


Mdala alitumia fursa hiyo kulipongeza shirika la YMC,kwa juhudi zake za kuhamasisha na kuelimisha jamii na hasa wanaume juu ya umuhimu wa ushiriki sawa wa wanaume katika masuala ya afya ya uzazi na ujinsia.

“Kazi yenu imezaa matunda mazuri,wanaume wengi sasa wamebadilika na wanasindikiza wake zao kliniki.Sio hivyo tu,kazi zote za nyumbani ikiwemo kufua nguo za watoto,kupika,kuchota maji na kuogesha watot,wanaume wanashiriki vizuri tu”,alisema mratibu wa TACAIDS.

Awali mratibu wa YMC, mkoa wa Singida,Fidelius Yunde,alisema toka waanzishe mradi wa ushiriki sawa wa wanaume katika masuala ya afya ya uzazi na ujinsia (TMEP) mwaka 2011,wamefanikiwa kuwafikia vijana 40,000 na vikundi 186 ambayo kati yake 25 vimepanda hadhi na kuwa CBOS.


Kwa mujibu wa Yunde,mradi huo upo katika wilaya  nne za mkoa wa Singida,ambazo ni Ikungi,Singida vijijini,Iramba na Manyoni.

No comments:

Post a Comment