Friday, November 28, 2014

DC aagiza watendaji kujiunga CHF kuvutia wananchi.

Kaimu meneja mfuko wa taifa bima ya afya (NHIF) mkoa wa Singida, Adamu Salum,akizungumza siku ya uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha wananchi wa kijiji cha Simbanguru wilayani Manyoni kujiunga na mfuko wa afya ya jamii (CHF),juzi.Amedai kwamba ugonjwa haubagui wala hautoi taarifa ya ujio wake,hivyo kujiweka upande salama,ni kujiunga na mifuko ya afya ukiwemo wa CHF.
Mganga mkuu wa wilaya ya Manyoni mkoa wa Singida,Dk.Raphael Hangai,akitoa nasaha zake kwenye uzinduzi wa kampeni ya uhamasishaji wananchi kujiunga na mfuko wa afya ya jamii (CHF) uliofanyika katika kijiji cha Simbangurum, ili waweze kujijengea mazingira ya kupata matibabu wakati wote hata ule wasiokuwa na fedha.

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Manyoni mkoa wa Singida,Speet Mseya,akiwahimiza wananchi kujiunga na mfuko wa afya ya jamii (CHF).Kwa mujibu wa mkurugenzi Mseya, kaya yenye mume, mke na watoto wanne walio na umri chini ya miaka 18,wakilipa shilingi 5,000 tu,wote watakuwa na uhakika wa kupata matibabu stahiki kwa mwaka mzima bila kuongeza fedha nyingine.
Kaimu mkuu wa wilaya ya Manyoni,Cosmas Nkali.akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa kampeni ya uhamasishaji wananchi kujiunga na mfuko wa afya ya jamii (CHF).Kwa mujibu wa Cosmas,asilimia ya kaya 19 tu wilayani humo ndizo zimejiunga na CHF na kwamba kaya yenye mume,mke,watoto 4 walio na umri wa chini ya miaka 18,inapaswa hulipa ada ya shilingi 5,000 tu,ili kupata matibabu mwaka mzima bila kuongeza fedha nyingine.
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Simbanguru,waliohudhuria uzinduzi wa kampeni ya uhamasishaji wananchi kujiunga na mfuko wa afya ya jamii (CHF).

MKUU  wa Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida Fatma Hassan Toufiq ameagiza viongozi wa ngazi mbalimbali wakiwemo wenyeviti wa vitongoji, kujiunga na mfuko wa afya ya jamii (CHF) kama njia  mojawapo ya kuwavutia wananchi kujiunga na mfuko huo.

Amedai kwamba ni muhimu kwa viongozi kujiunga na mifuko ya afya  ukiwemo  CHF, kwani  watakuwa wanatekeleza sera ya taifa na ilani ya uchaguzi wa CCM.

DC huyo aliyesema hayo wakati akizungumza kwenye siku ya uzinduzi wa kampeni wilayani humo ya kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko huo, ili kujihakikishia matibabu stahiki kupindi chote hata kile ambacho watakuwa hawana fedha.


Alisema kaya aslimia 19 tu ya wananchi wilayani humu, ndizo zimejiunga na CHF hadi sasa, kwa hiyo kunahitajika nguvu za ziada, ili lengo la kaya zote kujiunga ba mfuko huo liweze kufikiwa.

“Uelimishaji unahitajika kuanzia ngazi ya vitongoji, vijiji, Kata na Tarafa kwa kufanya mikutano ya kuhamasisha na uelimishaji. Pia wenyeviti wa vitongoji, watendaji n.k., ambao bado hawajajiunga na mfuko huu, muoneshe mfano kwa kujiunga”,alisisitiza kwenye hotuba yake iliyosomwa na katibu tawala wa wilaya hiyo,Cosmas Nkali.

Toufiq ametaja baadhi ya faida ya mfuko huo kuwa ni mwananchi kupata  huduma ya matibabu wakati wote hata kama  hana fedha na mfuko utatoa uhakika wa upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kwa muda wote.


Alitaja faida zingine kuwa ni pamoja na kugharamia ukarabati wa majengo ya kutolea huduma na shughuli zingine kama kulipa posho mbalimbali za kamati ya afya za Zahanati na watumishi wa afya.

Katika hatua nyingine, DC huyo aisema  viwango  vya uchangiaji kwa maana ya ada  ya CHF ,vitabadilika kuanzia Julai mwakani katika shilingi 5,000 za sasa hadi shilingi 10,000 kwa kaya moja.

Awali, Kaimu Meneja wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHF) Mkoa wa Singida , Adamu Salum,  alisema ni ukweli usiopingika  kwamba  ugonjwa hautoi taarifa,hauchagui siku wala hauchagui mtu, kwa hiyo upo uwezekano mkubwa kumpata mtu akiwa hana fedha kabisa.


Adamu alisema katokana na ukweli huo, upo  umuhimu mkubwa kwa kila wananchi kujiunga na mifuko ya afya, ili kujijengea mazingira mazuri ya kupata tiba wakati wote.

No comments:

Post a Comment