Tuesday, November 11, 2014

Rais aagiza kufunguliwa kwa mgodi wa dhahabu wa Mattany Ikungi.

Rais wa Shirikisho la wachimba madini Tanzania, John Bina, akizungumza na wachimbaji madini wa machimbo ya dhahabu kijiji cha Mhintiri tarafa ya Ihanja wilaya ya Ikungi .Rais Bina pamoja na mambo mengine, aliagiza kufunguliwa kwa mgodi wa dhahabu unaomilikiwa na Mattany Khalifa uliofungwa baada ya kuvamiwa na wachimbaji wadogo.
Mmiliki wa Mattany Gold mine, Mattany Khalifa, akizungumza kwenye mkutano wa hadhara ulioitishwa maalum kwa ajili ya kufunguliwa kwa mgodi wake uliofungwa baada ya kuvamiwa na wachimbaji wadogo.Mwenye kofia ya pama ni Rais wa shirikisho la wachimbaji madini Tanzania, John Bina.

Baadhi ya wachimbaji wadogo wa machimbo ya dhahabu kijiji cha Mhintiri tarafa ya Ihanja wilaya ya Ikungi, wakimsikiliza Rais wa Shirikisho la wachimba madini Tanzania, John Bina aliyekuwa akizumgumza nao.

Rais wa shirikisho la wachimbaji madini Tanzania, John Bina,(mwenye shati la kitenge) akikagua shimo linalodaiwa kutoa kiasi kikubwa cha dhahabu katika muda wa wiki moja na nusu. Shimo hilo linalomilikiwa na Mattany Khalifa, lilivamiwa na wachimbaji wadogo na kusababisha kufungwa kwa zaidi ya siku nne.

RAIS wa shirikisho la wachimba madini Tanzania, John Bina, ameagiza kufunguliwa mara moja kwa mgodi wa dhahabu wa Mattany Ikungi na kuonya kwamba mchimbaji  madini yeyote atakaye kiuka sheria zinazotawala sekta ya madini, atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Bina ametoa onyo hili wakati akizungumza na maelefu ya wachimbaji  madini wadogo wanaojishughulisha na uchimbaji dhahabu katika machimbo ya Mhintiri tarafa ya Ihanja wilaya ya Ikungi.

Alisema mgodi huo unaomilikiwa kihalali na Mattany Khalifa ambao ulifungwa kwa zaidi ya siku nne kutokana na kuvamiwa na baadhi ya wachimbaji, umefunguliwa rasmi kuanza kazi kuanzia oktoba 20 mwaka huu.


“Kuvamiwa kwa mgodi huu,kitendo hicho ni kinyume na sheria zilizowekwa.Kitendo hiki kinasababisha harasa kubwa kwa mmiliki pia kinasababisha uvunjivu wa amani na utulivu.Kama hali hii ikiachwa ikaendelea, kutaleta madhara makubwa kwa wachimbaji wenyewe na mali zao”, alifafanua Bina.

Akifafanua zaidi, alisema tabia hiyo ya kuvamia maeneo yaliyomilikishwa kisheria,haivumiliki  hata kidogo. Wachimbaji watakaorudia,watachukuliwa sheria kali dhidi yao.

 “Sitaki na sipendi kusikia machimbo ya dhahabu Mhintiri yamejaa  wachimbaji haramu.Wachimbaji haramu ni wale wasiokuwa na leseni,vibali na mbaya zaidi, siku zote wanataka kuvunjwa sheria ili waweze kutajirika kwa njia haramu na za mkato,” alisema na kuongeza;

“Nawaombeni tufuate sheria, ili wachimbaji wa hapa waweze kufanya shughuli zao kwa amani na utulivu”.

Kwa upande wake mmiliki wa mgodi huo, Mattany Khalifa, alisema eneo hilo alianza kulifanyia utafiti toka kwa 2012 kwa kibali halali na kufanikiwa kupata leseni ya kulimiki mapema mwaka jana (2013).


“Nwaomba wachimbaji wenzangu, kwanza tuheshimu maeneo yenye leseni.Pia tufanye kazi ya uchimbaji kwa kuzingatia sheria zilizowekwa, pamoja na mambo mengine, tuhakikishe mwenye mgodi anapewa aslimia yake 30 ya mapato na wachimabji wanachama, wabaki na aslimia zao 70”,alisema na kushangiliwa na maelefu ya wachimba madini.

No comments:

Post a Comment