Thursday, November 20, 2014

Serikali kutoajiri wahitimu wa vyuo visivyosajiliwa.

Waziri wa nchi ofisi ya Rais, Menejiment ya Utumishi wa Umma,Celina Kombani, akizungumza kwenye mahafali ya 20 ya chuo cha uhazili Tanzania mjini Singida. Kombani aliwaasa wahitimu hao 4,960, kwamba wasiridhike na elimu waliyopata, bali waongeze bidii zaidi katika kujiendeleza.
Kaimu Mkuu wa mkoa wa Singida na mkuu wa wilaya ya Singida, Queen Mlozi, akizungumza kwenye mahafali ya 20 ya chuo cha uhazili Tanzania yaliyofanyika mjini Singida. Jumla ya wahitimu 4,960 walitunukiwa vyeti vya fani mbalimbali.

Baadhi ya wahitimu wa chuo cha uhazili Tanzania waliotunukiwa vyeti mbalimbali na waziri Kombani.

Baaadhi wa wazazi/walezi na wahitimu wa chuo cha uhazili Tanzania, wakijipatia picha kwa ajili ya kukmbukumbu.

WAZIRI wa nchi ofisi ya rais, menejimenti ya utumishi wa umma, Celina Kombani,amesisitiza kwamba serikali haitaajiri wahitimu wo wote kutoka kwenye vyuo ambavyo havijasajiliwa kisheria.

Amedai kwamba vyuo ambavyo havijasajiliwa kisheria, vyuo hivyo vinazalisha wahitimu ‘makanjanja’, ambao serikali haina nafasi nao kabisa.

Waziri Kombani,aliyasema hayo wakati akizungumza kwenye kilele cha mahafali ya 20 ya chuo cha utumishi wa umma Tanzania yaliyofanyika hapa tawi la Singida.

Alisema serikali itaendelea kupokea wahitimu kutoka vyo vilivyosajiliwa kisheria, na hasa chuo cha utumishi wa umma Tanzania.


Kuhusu wahitimu hao 4,960 kutoka matawi yote Tanzania, Kombani aliwaasa kwamba bado wana safari ndefu katika kujiendeleza kielimu,hivyo waongeze juhudi kujiendeleza zaidi.

“Hata mtakapokuwa mmeajiriwa, endeleni kujielimisha kadri uwezo wenu utakavyowaruhusu.Ushindani katika ajira ni mkubwa mno,kwa sasa  ajira inahitaji mhusika awe na upeo mkubwa kielimu”,alifafanua.

Awali mtendaji mkuu wa chuo cha utumishi wa umma Tanzania, Saidi Nassor, alisema wana mpango wa kupanua chuo kwa kuanzisha tawi jipya mkoani Mbeya.


“Tutaongeza madarasa,maktaba za kisasa na ofisi ya tawi la Tabora. Aidha tunatarajia kuanza maandalizi ya michoro ya kituo kikuu cha chuo Ikwiriri wilaya ya Rufiji na tawi la Singida baada ya zoezi la fidia kukamilika kwa aslimia mia moja”alisema Nassor.

Kwa upande wa kanda ya ziwa, Nassor alisema maandalizi ya kupata eneo la kufungua tawi jipya, yanaendelea vizuri na likipatikana,shughuli za ujenzi zitafanyika.


Wakati huo huo,mtendaji huyo alisema wanaendelea kutoa mafunzo ya ndani kwa watumishi waliomo kazini,kwa lengo la kuwakumbusha kuwa na uelewa juu ya kanuni za utumishi na sheria za matumizi ya fedha za umma.


No comments:

Post a Comment