Thursday, November 20, 2014

Serikali yaonya ubadhilifu wa wahitimu.

Wahitimu 1,808 wa fani mbalimbali wa vyuo vya uhasibu tawi la Mwanza na Singida, wakiwa kwenye maandamano ikiwa ni sehemu ya mahafali yao ya 12 yaliyofanyika mjini Singida.

Naibu Waziri wa Fedha, Mh. Mwigullu Lameck Nchemba, akizungumza kwenye mahafali ya 12 ya tawi la Mwanza na Singida, yaliyofanyika katika viwanja vya chuo cha uhasibu mjini Singida. Mwigulu aliwaasa wahitimu hao waweke mbele uadilifu,uaminifu na kuchapa kazi kwa bidii na maarifa ili kujijengea mazingira ya kuaminika mbele ya jamii.

Baadhi ya wahitimu 1,808 wa vyuo vya Mwanza na Singida, wakiwa kwenye mahafali yao ya 12 yaliyofanyika  kwenye viwanja vya uhasibu mjini Singida.

SERIKALI imeonya kwamba wahitimu wa ngazi mbalimbali za uhasibu na ugavi, haitawavumilia endapo watajihusisha na vitendo vya rushwa na ubadhilifu wa mali ya umma, kwa madai kwamba itawachukulia hatua kali za kisheria.

Aidha, imedai kwa sasa wataalamu wa nafasi hizo wapo wengi ambao ni waaminifu na waadilifu na hawana ajira,kwa hali hiyo nafasi ya kubebana haipo tena hivyo mhusika anapaswa kujilinda dhidi ya vitendo hivyo.

Onyo hilo limetolewa na Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba,wakati akizungumza kwenye mahafali ya 12 ya taasisi ya uhasibu Tanzania (TIA) na ya tatu kwa kampasi ya Singida.

Alisema vitendo vya rushwa na ubadhilifu,vina madhara makubwa kwa maisha ya mtu mmoja mmoja na uchumi wa taifa letu kwa ujumla.

“Niwakumbushe tu kwamba, rushwa bado ni adui mkubwa wa haki ya mtu mmoja mmoja na kwa maendeleo pia. Vitendo hivyo vya rushwa na ubadhilifu wa mali ya umma, havikubaliki na havivumiliki kabisa”, alifafanua Mwigulu ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Iramba magharibi.

Katika hatua nyingine, amewataka wale walio na ajira na watakaopata ajira ama za kuajiriwa au za kujiajiri,wakachape kazi kwa bidii,ufanisi,uaminifu,uadilifu,ubunifu,umakini na weledi.

Awali Afisa mtendaji mkuu wa taasisi ya Uhasibu Tanzania, Dk.Joseph Kihanda,alisema wahitimu mwaka huu,ni 1,808 wakiwemo wanaume 883 na wanawake 925 kutoka kampasi za Mwanza na Singida.

Aidha, Dk.Kihanda alisema mapato ya taasisi za kampasi za Mwanza na Singida kwa mwaka wa masomo wa 2013/2014, ni zaidi ya shilingi bilioni 2.8 ikilinganishwa na zaidi ya shilingi 2.7 bilioni zilizokusanywa mwaka wa fedha wa 2012/2013.Hiyo ni sawa na ongezeko la aslimia 3.15.

“Katika mwaka huu wa masomo wa 2014/2015,taasisi inatarajia kukusanya jumla ya shilingi 3,001,150,000 katika kampasi ya Mwanza na Singida kutoka vyanzo mbalimbali vya mapato”,alisema.

Mahafali hayo,pia yalihudhuriwa na Mwenyekiti wa bodi ya usahauri ya wizara,Profesa Isaya Jairo

No comments:

Post a Comment