Tuesday, November 25, 2014

Wadau waliohudhuria kongamano la Nyuki mjini Arusha, watembelea shamba la darasa la Nyuki wilayani Ikungi.

Kaimu Mkurugenzi wa idara ya Nyuki Gladness Mkanda,akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mahambe wilaya ya Ikungi muda mfupi baada ya kuongoza wadau wa nyuki kutoka sehemu mbalimbali duniani,kutembelea shamba darasa la ufugaji bora wa nyuki linalomilikiwa na shirika la Future Development Initiatives (Fu-DI).Mkamba alitoa wito kwa wananchi kujiunga katika vikundi vya ufugaji Nyuki ili waweze kujikomboa kiuchumi.
Meneja wa shirika la Future Development Initiatives (Fu-DI), Jonathani Njau, akitoa ufafanuzi juu ya uendeshaji wa shamba darasa la ufugaji nyuki kisasa, kwa mmoja wa wadau wa Nyuki waliohudhuria kongamano la Nyuki duniani lililofanyika mjini Arusha hivi karibuni.
Baadhi ya wadau wa nyuki kutoka sehemu mbalimbali duniani,wakipiga picha mizinga ya nyuki iliyopo kwenye shamba darasa la ufugaji Nyuki kisasa katika kijiji cha Mahambe wilaya ya Ikungi.

Meneja wa shamba la Nyuki la Singida Youth Entrepreneurs and Consultants Co-operative Society  katika kijiji cha Kisaki manispaa ya Singida, Philemon Kiemi (kulia) akisalimiana na mwalimu wake Dr.Shimon Barel wa chuo kikuu Hebrew Jerusalem.
Baadhi ya wadau wa nyuki kutoka sehemu mbalimbali duniani, wakiangalia mizinga iliyopo kwenye shamaba darasa la ufugaji Nyuki kisasa lililopo katika kijiji cha Mahambe wilaya ya Ikungi.
Baadhi ya wadau wa nyuki  kutoka sehemu mbalimbali duniani wakiangalia mizinga iliyopo kwenye shamba la ufugaji nyuki kisasa lililopo kijiji cha Mahambe wilaya ya Ikungi.Wadau hao ni baadhi ya wadau wa nyuki waliohudhuria kongamano la Nyuki lililofanyika hivi karibuni mjini Arusha.
Meneja wa shirika lisilo la kiserikali la Future Development Initiatives (Fu-DI) la wilaya ya Ikungi, Jonathani Njau (kulia) akishiriki kutoa burudani kwa wadau wa Nyuki kutoka  sehemu mbalimbali waliotembelea shamba darasa ufugaji nyuki kisasa,linalomilikiwa na shirika la Fu-DI.Wa pili kulia ni mama yake na meneja Njau (82), naye akishiriki kutoka burudani hiyo iliyopamba ziara ya ugeni mkubwa wa wadau wa Nyuki.

1 comment:

  1. Nawezaje kupata elimu ya ufugaji nyuki... Mimi nipo Arusha

    ReplyDelete