Tuesday, November 11, 2014

Watoto zaidi ya 66,442 mkoani Singida kupatiwa chanjo mpya ya Malaria na Rubella.

Mkuu wa wilaya ya Singida, Queen Mlozi, akizindua zoezi la chanjo mpya ya Malaria na Rubella kwa manispaa ya Singida.Uzinduzi huo umefanyika kwenye kituo cha afya cha Sokoine mjini Singida. Pamoja na chanjo ya Malaria na Rubella, pia dawa za minyoo na mabusha zilitolewa.
Meya wa manispaa ya Singida Sheikh Salum Mahami, akizungumza kwenye zoezi la uzinduzi wa chanjo ya Malaria na Rubella  kwenye ukumbi wa mikutano wa kituo cha afya Sokoine mjini Singida.Wa pili kulia (waliokaa) ni mkuu wa wilaya ya Singida,Queen Mlozi na anayefuata ni kaimu Mkurugenzi wa manispaa ya Singida.


HALMASHAURI ya manispaa ya Singida, inatarajia kuchanja watoto 66,422, chanjo mpya ya Malaria na Rubella  wakati wa kampeni ya kitaifa inayoanza jana  Oktoba 18 hadi 24 mwaka huu.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mganga Mkuu manispaa ya Singida Dk. Fredrick Mugarula, wakati akitoa taarifa yake kwenye uzinduzi wa chanjo mpya ya Malaria na Rubella uliofanyika kwenye kituo cha afya cha Sokoine mjini Singida.

Alisema katika zoezi hilo, kunahitajika ushirikiano wa dhati  ili kila mtoto aweze kupata haki yake ya msingi ambayo itamsaidia kupambana na maradhi hayo.


“Pasipo chanjo hii, magonjwa ya Surua na Rubella yanaweza kumletea matatizo mengi mtoto ya kiafya yakiwemo vifo, ulemavu wa kudumu, upofu na hata kutokusikia”, alifafanua Dk. Magarula.

Kawa upande wake mgeni rasmi kwenye semina hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Singida Queen Mlozi, ametoa wito kwa Viongozi  wa madhehebu ya dini na wale wa kisiasa kuhamasisha waumini na wachama wao kupeleka watoto wao kupata chanjo hiyo mapya bila kukosa.

Mlozi alisema kampeni hii ni azma ya serikali katika kutekeleza kikamilifu malengo  ya milenia namba nne na tano, ya kulinda afya za na pia kuhakikisha kuwa rusua na rubella, zinatokomezwa kabisa ifakapo mwaka 2020.


“Na kwa sababu kupata chanjo ni haki ya mtoto na kwa kuwa mwenye haki hiyo hana uwezo wa kudai haki yake, serikali itaweka mazigira mazuri ya kumwezesha  mzazi kutimiza wajibu wake kwa kusogeza huduma hi karibu na makazi ya wananchi”, alisema Dk.Magarula.

No comments:

Post a Comment