Tuesday, November 11, 2014

Wazalishaji wadogo wahimizwa ubora katika bidhaa zao.

Mwakilishi wa mkurungezi wa usala wa chakula (TFDA), Lazaro Mwambole, akitoa taarifa yake muda mfupi kabla hajamkaribisha mgeni rasmi Katibu Tawala mkoa wa Singida,Liana Hassan kufungua mafunzo ya siku mbili yaliyohudhuriwa na wasindikaji wadogo wa chakula mkoa wa Singida.Wa pili kulia (waliokaa) Katibu Tawala mkoa wa Singida Liana Hassan na Mganga Mkuu wa mkoa wa Singida, Dk, Doroth Gwajima (wa pili kulia).
Katibu Tawala mkoa wa Singida, Liana Hassan, akizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo ya siku mbili yaliyohudhuriwa na wasindikaji wadogo mkoani Singida.Mafunzo hayo yalihusu usindikaji wa vyakula unaozingatia ubora na usalama wa chakula.Kulia ni mganga mkuu wa mkoa, Dk.Doroth Gwajima na kushoto ni Mwenyekiti wa wasindikaji wadogo mkoa wa Singida, Kisenge.

Baadhi ya wasindikaji wadogo wa chakula mkoa wa Singida, wakifuatilia mafunzo ya usindikaji bora na salama wa chakula.Mafunzo hayo yalifanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa kanisa katoliki mjini Singida.
Katibu tawala mkoa wa Singida,Lina Hassan (wa nne kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wasindikaji wadogo wa chakula mkoa wa Singida.Wa tatu Kulia ni mwakilishi wa Mkurugenzi wa usalama wa chakula (TFDA),Lazaro Mwambole.

KATIBU tawala mkoa wa Singida, Liana Hassan, amewahimiza wasindikaji wadogo wa vyakula, kuhakikisha bidhaa wanazozalisha zinakidhi vigezo vya ubora na usalama,ili kujijengea mazingira mazuri ya kudumu katika biashara hiyo.

Hassan ametoa wito huo wakati akizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo ya wasindikaji wadogo wa vyakula yaliyofanyika katika ukumbi wa kanisa Katoliki mjini Singida.

Alisema katika wakati huu wa utandawazi na biashara huria, hakuna msindikaji ambaye ataweza kudumu katika biashara iwapo bidhaa zake hazitakidhi vigezo vya ubora na usalama.


Akifafanua zaidi, alisema “Hii inatokana na ukweli kuwa ubora na usalama wa vyakula ni sharti muhimu kwa wateja wa vyakula tunaowalenga.Ni matumaini yangu kuwa changamoto hii tutaishinda ikiwa tutashirikiana kuzalisha bidhaa zenye ubora na usalama. Kwa njia hii,tutadumu katika mazingira yaliyopo ya ushindani”.

Aidha, Hassan alisema katika mkoa wa Singida, zipo taarifa kuwa kuna changamoto ya kutokidhi matakwa ya sheria kwa hiari, ili kuboresha vigezo vya ubora na usalama wa bidhaa zinazozalishwa.

“Changamoto hizo ni pamoja na majengo kutosajiliwa na TFDA, kuzalisha na kuziingiza bidhaa za chakula sokoni bila kufuata taratibu zilizopo kutumia vifungashio visivyofaa na vilivyoduni na kuhifadhi bidhaa katika maeneo wazi yenye jua kali”,alisema katibu tawala huyo na kuongeza;

“Ni matumaini yangu kuwa baada ya mafunzo haya,mtatoka na maazimio ya utekelezaji ili mkoa wetu uanze kufanya vizuri katika mpango wa matokeo makubwa sasa (BNR) yaliyopangwa na serikali”.


Awali Mwakilishi wa Mkurugenzi wa usalama wa chakula (TFDA), Lazaro Mwambole alitaja baadhi ya mada zitakazotolewa kwenye mafunzo hayo kuwa ni dhana nzima kuhusu usalama wa chakula,taratibu za kisheria za usajili wa majengo ya usindikaji chakula na taratibu za kisheria za usajili wa vyakula vilivyofungashwa.

No comments:

Post a Comment