Sunday, June 1, 2014

Watanzania washauri kupata elimu ya kuendesha biashara.

Mwenyekiti wa klabu ya wafanyabiashara wa NMB tawi la Singida,Kyoma (katikati) akifuatilia mada zilizokuwa zinatolewa kwenye semina yao ya siku moja.Wa kwanza kulia ni katibu wa klabu hiyo,Welu Ntandu na kushoto ni makamu mwenyekiti,Elizabeth Masawe.
Meneja Mahusiano na Biashara wa makao makuu NMB jijini Dar-es-salaam, Dickson Mpangarawe (wa kwanza kushoto),akifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa kwenye semina ya siku moja iliyohudhuriwa na wananchama wa klabu ya wafanyabiashara wa tawi la NMB Singida.Wa pili kushoto,ni Meneja wa tawi la benki ya NMB Singida, Christine Mwangomo.
Mwezeshaji Isack Mnyagi, akitoa mada yake ya ujasiriamali kwa wanachama wa klabu ya wafanyabiashara wa tawi la NMB Singida mjini kwenye semina ya siku moja iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Aque Vitae.
Afisa elimu kwa wafanyabiashara TRA mkoa wa Singida,Zakaria Bwagilo,akitoa mada yake ya umuhimu wa kulipa kodi kwenye semina iliyohudhuriwa na wananchama wa klabu ya wafanyabiashara wa tawi la MNB Singida mjini.

WATANZANIA wanaotarajia kuanzisha shughuli za biashara za aina mbalimbali wameshauri kujenga utamaduni wa kupata elimu na mafunzo ya uendeshaji wa biashara kwanza kabla ya kuanzisha biashara husika.

Wito huo umetolewa hivi karibuni na Mkurugenzi wa Shirika Lisilo la Kiserikali la Integrity Foundation la jijini Dar-es-salaam,Isack Mnyagi wakati akitoa mada ya ujasiriamali  kwa wanachama wa klabu ya wafanyabiashara wa benki ya NMB tawi la Singida.

Amesema uzoefu unaonyesha wafanyabiashara wengi ambao huanzisha biashara bila kuwa na elimu ya kutosha ya biashara,hufilisika kwa kipindi kifupi.

Akifafanua zaidi,amesema “Watu wengi huanzisha biashara kwa kuiga au kutokana na kiburi chao kwamba wanajua kila kitu.Biashara za sasa sio sawa na zile za zamani ambazo zilikuwa na faida ya shilingi kwa shilingi.Biashara za sasa zina ushindani mkubwa kwa hali hiyo, zinahitaji mtu anayetaka kufanya biashara,ahakikishe ana elimu ya kutosha juu ya kuendesha biashara”.

Katika hatua nyingine,Mnyagi amewataka kupiga vita vitendo vya familia kutumia bidhaa za duka bila kulipa kwa madai kwamba vitendo hivyo vinachangia kwa kiasi kikubwa kufilisi duka.

“Pia msipende kununua bidhaa za

Kinana amaliza ziara yake Mkoani Singida kwa kuzuru Singida Vijijini.

Mbunge wa Singida Mashariki Lazaro Nyalandu akimlaki Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana wakati wa mapokezi ya kiongozi huyo wa Chama,  katika kata ya Msisi, Singida Vijijini, jana Mei 26, 2014.
Wanachama wa Jumuia ya Wazazi Kata ya Msisi wakimvalisha mgolole Kianana kabla ya kufungua tawi la Wazazi la Kata hiyo.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizindua tawi la Jumuia ya Wazazi Kata ya Msisi, wilaya ya Singiga Vijijini.
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akishiriki kuvuna mtama katika shamba la mfano la zao hilo katika kata ya Mtinko, Singida Vijijini, Jana. Aliyevaa suti ni Waziri wa maliasili na Utalii, Mbunge wa Singida Mashariki, Lazaro Nyalandu.

Mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Taifa Jimbo la Singida Mjini.

Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini, Mh. Mohammed Dewji (MO), Naibu Waziri wa Fedha ambaye pia Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Mh. Mwigulu Nchemba wakiwa kwenye boda boda, wakati wa msafara wa kuelekea kwenye mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika eneo la viwanja vya People’s Club mjini Singida.
Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Abdulrahman Kinana , sambamba na Katibu wa Itikadi na  Uenezi Nape Nnauye,wakiwasili kwenye viwanja vya People’s Club kwenye mkutano wa hadhara kwa staili ya aina yake kwa kutumia usafiri wa Bajaji.
Katibu mkuu wa CCM , Kinana, (kwanza kulia),akifurahia ujumbe ulioandikwa kwenye bango la wajasiriamali waliohudhuria mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Peoples klabu mjini Singida.
Mkuu wa wilaya ya Singida,Queen Mlozi,(wa kwanza kushoto) akishiriki kutoa burudani kwenye mkutano wa hadhara ulioitishwa kwa ajili ya katibu mkuu CCM taifa,Abrahamani Kinana,kuzungumza na wakazi wa jimbo la Singida mjini.

Kinana akagua Ujenzi Daraja la Sibiti linalounganisha Singida na Simiyu.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman  Kinana akitoa orodha ya vijiji vitakavyopata huduma ya umeme katika wilaya ya Mkalama, alipohutubia mkutano wa hadharakwenye  kijiji cha Nkungi, Wilaya humo,  Mei 24, 2014, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na kusikiliza kero za wananchi na kujadsiliana nao njia za kuzitatua katika wilaya ya Iramba mkoani Singida.
Mkuu wa mkoa wa Singida Dk. Parseko Kone (aliyenyoosha mkono) akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia) kuhusu maendeleo ya ujenzi wa daraja linalounganisha mikoa ya Singida na Simiyu katika  mto Sibiti, Kinana alipokagua ujenzi wa daraja hilo akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na kusikiliza kero za wananchi na kujadsiliana nao njia za kuzitatua katika wilaya ya Iramba leo Mei 24, 2014. Wapili kulia ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye ambaye amefuatana na Kinana katika ziara hiyo. Ujenzi wa daraja hilo unaogharimu sh. bilioni 16, unatarajiwa kukamilika Desemba mwaka huu.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitazama nguzo ya daraja linalojengwa kuunganisha mikoa ya Singida na Simiyu katika  mto Sibiti, Kinana alipokagua ujenzi wa daraja hilo akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na kusikiliza kero za wananchi na kujadsiliana nao njia za kuzitatua katika wilaya ya Iramba  Mei 24, 2014.

Mh. Dewji amwaga msaada wa zaidi ya shilingi Milioni 127 kwenye Taasisi za Dini zaidi 80 Jimboni kwake.

Mbunge wa Singida Mjini, Mh. Mohammed Dewji (MO), akizungumza na viongozi wa Mahakama ya Qadhi wakati alipotembelea Mahakama hiyo kuona namna inavyohudumia waumini wa Dini ya Kiislamu katika kutatua migogoro ya ndoa.
Sheikh wa Mahakama ya Qadhi, Ramadhani Kaoja akimweleza Mheshimiwa Mbunge shughuli za Mahakama hiyo pamoja na changamoto mbalimbali zinazowakabili, Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Singida Mjini , Hamis Nguli, wa pili kulia ni Katibu wa Mahakama ya Qadhi, Alhajj B. Mlau.
Mbunge wa jimbo la Singida Mjini MO akisalimiana na waumini wa Msikiti wa Kata ya Mtipa wakati alipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa Msikiti huo, ambapo mara baada ya kuona hatua zilizofikia za ujenzi huo aliahidi kutoa  Mabati 50 pamoja na mifuko 50 ya Saraji kwa ajili ya kukamilisha ujenzi huo.
 MO akitoka kukagua ujenzi wa Msikiti wa kijiji cha Mangwanjuki kata ya Mtipa.
Waumini wa Msikiti wa kijiji ch Mangwanjuki wakimsikiliza Mbunge wao Mheshimiwa MO.

Picha 40 Mh.Dewji akikagua shughuli mbalimbali za maendeleo ya jimbo lake.





Afariki dunia porini akitafuta dawa ya kienyeji.

Kamanda Geofrey Kamwela

MKAZI wa Kijiji cha Chang’ombe kata, tarafa na wilaya ya Manyoni mkoani Singida Andrew Mlunda (40),amefariki dunia akiwa porini kutafuta na kuchimba dawa ya kienyeji.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida,SACP, Geofrey Kamwela amesema marehemu aliondoka nyumbani kwake juzi saa 10.00 jioni akiwa amebeba shoka na kuiaga familia yake kuwa anakwenda porini kutafuta dawa yake ya kifua kwani alikuwa anahisi maumivu.

Kamwela amesema kuwa tangu alipoondoka hakurudi nyumbani hadi giza lilipoingia na kusababisha hofu kwa familia yake.Hata alipopigiwa simu,simu yake ya kiganjani haikuweza kupatikana.

Kutokana na hali hiyo,amesema kuwa familia hiyo ilitoa taarifa kwa majirani na mara moja majirani walianza msako wa kumtafuta ndani ya pori la kijiji hicho.

“Wakiwa porini waliendelea kumpigia simu na kwa bahati walisikia mlio wa simu kutoka kichakani na waliposogea sehemu mlio wa simu ulikuwa unatoka,walimkuta Andrew akiwa tayari ameishafariki dunia”,amesema na kuongeza;

“Walimkuta akiwa ametoka damu nyingi huku shoka lake likiwa pembeni, baada ya hapo,walitoa taarifa katika kituo cha polisi Manyoni mjini na askari walifika mara moja na kuuchukua mwili kwa ajili ya uchunguzi”.

Kamwela amesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa marehemu amefariki dunia baada ya