Thursday, August 21, 2014

Maiti yaokotwa Singida.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida, SACP Geofrey Kamwela.

Mwili wa mwanaume ambaye hajafahamika jina wala  makazi yake anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 28,umeokotwa maeneo ya Misuna makaburini tarafa ya Mungumaji Singida mjini.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida, SACP Geofrey Kamwela, amesema mwili huo umeokotwa saa moja asubuhi ukiwa umetelekezwa kwenye makaburi ya Misuna.

Alisema mwanaume huyo siku ya tukio alikuwa amevaa shati la miramba miramba na suruali aina ya jinsi rangi ya bluu.

“Tulipata taarifa ya tukio hilo kutoka kwa mpita njia na askari walipofika eneo la tukio na kufanya uchunguzi,walibaini kuwa marehemu alifariki dunia baada ya

MO aishukia CCM ukarabati uwanja wa Namfua.

Katibu wa CCM Mkoa wa Singida Naomi Kapambala aaizungumza na waanndishi wa habari juu ya ufafanuzi wa maendeleo ya ujenzi wa uwanja huo.



Zaidi ya wananchi 3,000 Wilaya ya Ikungi Singida kunufaika na soko la asali chini ya mradi wa FU-DI kwa ufadhili wa UNDP.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk Parseko Kone akizungumza na wanavikundi 49 vya ufugaji wa Nyuki katika Wilaya ya Ikungi wakati wa uzinduzi wa mradi wa FU-DI na ugawaji wa mizinga ya Nyuki pamoja na vifaa.
Meneja wa mradi wa FU-DI BBonifasi Leso akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo Ikungi.
Afisa mwandamizi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Amon Manyanya akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mratibu wa mradi wa Nyuki Wilayani Ikungi, Jonathan Njau akitambulisha mradi wake kwa mkuu wa mkoa wa Singida.

Singida yakabiliwa na Upungufu wa watumishi sekta ya Afya.

Mkuu wa wilaya ya Singida.Queen Mlozi, akizungumza kwenye kikao cha mrejesho wa utafiti uliofanywa na timu ya ufuatiliaji na uwajibikaji jamii (Social Accountability Monitoring-SAM) kilichofanyika mjini Singida.Timu ya SAM kwa kushirikiana na baadhi ya madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Singida,kwa pamoja walifanya utafiti juu ya uwajibikaji kwenye vituo vya kutolea huduma ya afya.Kushoto ni mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Singida,Idd Mnyampanda nas kulia ni mwenyekiti wa kikao hicho,diwani wa kuteuliwa, Salma Kundya.
Mkuu wa ofisi ya shirika la Sikika kanda ya Dodoma,Norah Mchaki,akitoa ufafanuzi juu ya utafiti wa uwajibikaji katika vituo vya kutolea huduma vya halmashauri ya Singida.
Diwani wa kata ya Ilongero (CCM) wilaya ya Singida,Ramadhan Samwi, akichangia jambo kwenye kikao cha mrejesho wa utafiti uliofanywa kwa pamoja na timu ya SAM na baadhi ya madiwani wa halmashauri ya Singida, juu ya uwajibikaji katika vituo vya kutolea huduma ya afya.

Mkuu wa wilaya ya Singida,Queen Mlozi,(wa pili kushoto) akifuatilia taarifa ya mrejesho wa timu ya SAM iliyotafiti uwajibikaji katika utoaji wa huduma za afya katika vituo vya afya vya halmashauri ya wilaya ya Singida.Wa kwanza kulia ni mwenyeiti wa halmashauri ya wilaya ya Singida,Idd Mnyampanda na kushoto ni mwenyekiti wa kikao cha mrejesho wa utafiti uliofanywa na timu ya SAM chini ya shirika la Sikika.

HALMASHAURI ya wilaya ya Singida, inakabiliwa na upungufu wa watumishi 144 wa kada mbali mbali wa sekta ya afya, hali inayosababisha huduma za afya kutolewa bila kuzingatia ubora unaohitajika

Hayo yalisemwa na Katibu wa afya katika halmashauri hiyo,Severin Sosthenes, wakati akitoa majibu dhidi ya hoja zilizotolewa na timu ya ufuatiliaji uwajibikaji jamii (Social Accountability Monitoring – SAM) katika halmashauri hiyo.

Alisema halmashauri hiyo ina mikakati kadhaa ya kutatua tatizo la upungufu wa raslimali watu katika sekta ya afya.

Katika mikakati hiyo, alisema katika bajeti yao ya mwaka juzi, walitenga fedha kwa ajii ya watumishi wapya 110.

“Baada ya kutenga fedha hizo, tulizunguka vyuo mbali mbali kuhamasisha wanaomaliza masomo, waombe kuja kufanya kazi kwenye halmashauri yetu,na tukawahakikishia kuwalipa stahiki na stahili zao”,alifafanua katibu huyo.

Sosthens alisema pamoja na juhudi hizo, walifanikiwa kupata watumishi 47 wa kada mbali mbali ambao hadi sasa wanaendelea kufanya kazi katika halmashauri hiyo ingawa idadi inayohitajika bado haijafikiwa.

Katika hoja yake hiyo, timu ya SAM ilitaka kujua ni jinsi gani

Watu watano wakiwemo watatu wa familia moja,wameuawa Mkoani Singida.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Singida, SACP, Geofrey Kamwela.

Watu watano wakiwemo watatu wa familia moja,wameuawa katika matukio tofauti,likiwemo la wanafamilia hao kukatwa katwa kwa mapanga sehemu mbalimbali za miiili yao na watu wasiofahamika.

Tukio hilo la mauaji lililowahusisha wanandoa hao lilitokea siku tano baada ya kuuawa kikatili kwa wanandoa wengine wawili,Bwana Ramadhan Lyanga (80) na Bi Aziza Ali (62) wakazi wa wilayani Iramba.

Akielezea matukio hayo, Kamanda wa polisi Mkoa wa Singida, SACP, Geofrey Kamwela alisema katika tukio la kwanza  lililotokea juni,15,mwaka huu saa 11:00  jioni katika Kijiji cha Masagi,kata ya Mtoa,Tarafa ya Shelui,wilayani Iramba ambapo watu watatu,akiwemo mjukuu waliuawa.

Kwa mujibu wa kamanda huyo wa jeshi la polisi waliouawa ni pamoja na Mombasa Makala (65),mkewe Vaileth Mandi (52) na mjukuu wao Joyce  Augustino (7) anayesoma darasa la kwanza katika shule ya msingi Masagi.

Hata hivyo Bwana Kamwela alisema uchunguzi wa awali unaonyesha kwamba watu hao

Vijana wazichapa kavukavu eneo la stendi ya zamani manispaa ya Singida wakigombea abiria.1



Vijana wawili walikutwa na Kamera yetu wakipigana ngumi kavukavu zisizo kuwa na kiingilio katika eneo la stendi ya zamani wakigombea abiria wanaosafiri kuelekea Wilaya ya Ikungi, hata hivyo katika ngumi hizo zisizopimwa uzito , ziliishia kutoana damu kabla ya kukamatwa na askari na kupelekwa kituoni kwa kosa na kupigana hadharani.

Halmashauri ya manispaa ya Singida yaweka taa kandokanodo ya barabara zake kuimarisha ulinzi.

Halmashauri ya manispaa ya Singida, yaweka taa kando kando ya barabara zake katika kuimarisha ulinzi na kupendezesha mji.
Taa hizo ambazo katika awamu ya kwanza zimewekwa kwenye barabara ya Arusha inayoanzia Bomani hadi nyumba za kulala ya Victoria karibu na Mwenge sekondari na ile ya Karume Arusha, zote zikiwa na urefu wa kilometa 2.720

Halmashauri ya manispaa ya Singida, imeweka taa kando kando ya barabara zake za mjini Singida zenye urefu wa kilometa 2.72, pamoja na mengine, kuimarisha ulinzi nyakati za usiku.

Taa hizo za kisasa ambazo zinatarajiwa kuanza kutumika wakati wo wote kuanzia sasa, pia mradi huo unatarajiwa  kuongeza mapato ya ndani ya halmashauri hiyo.

Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Joseph Mchina, alisema mradi huo unatekelezwa na kampuni ya masoko ya Angencies Tanzania Ltd, umeanza Mei mwaka huu, baada ya mkataba kusainiwa na pande zote mbili.

Alisema kwa kuanzia taa hizo zimewekwa kuanzia, Bomani barabara ya Arusha hadi nyumba ya kulala ya Victoria yenye urefu wa kilometa mbili, na barabara ya Karume – Arusha yenye urefu wa mita 720.

Akifafanua, alisema kampuni hiyo itagharamia shughuli zote za huduma hiyo ya mradi huo.

“Pia itaweka