Wednesday, January 28, 2015

Ataka taarifa za matumizi zisomwe kujenga imani.

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mkalama mkoa wa Singida, Bravo Lyapembile, katika picha.

MKURUGENZI  mtendaji wa halmashauri ya Mkalama  mkoani singida, Bravo Lyapambile, amewaagiza maafisa watendaji Kata kutoa/kusoma taarifa za michango mbalimbali ikiwemo ya ujenzi wa maabara kwa wakati,ili wananchi waendelee kuamini halmashauri yao.

Amesema kwa njia hiyo wananchi watajenga imani na Halmashauri yao kwamba michango yao inatumika kwa malengo yanayokusudiwa.

Mkurugenzi huyo ameyasema hayo wakati akizungumza na mwakilishi wa SingidaYetuBlog ofisini kwake juu ya maendeleo ya ujenzi wa vyumba vitatu vya maabara katika kila Shule  19 za sekondari za kata za halmashauri hiyo

Bravo  alisema kumekuwepo na malalamiko kutoka kwa baadhi ya wananchi wa Kata, kwamba kwa

Singida yafanikiwa kupanda miti Mil 10

Afisa misitu sekretarieti mkoa wa Singida,Charles Kidua akisoma taarifa yake ya maendeleo ya upandaji miti mkoani Singida katika siku ya upandaji miti iliyofanyika (15/1/2015) kimkoa katika kijiji cha Nkinto wilaya ya Mkalama.
Mkuu wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Kone (kushoto) akimwelekeza mwanafunzi wa shule ya msingi Nkinto wilaya ya Mkalama namna bora ya upandaji miti.Dk.Kone alishiriki upandaji miti katika siku ya upandaji miti kimkoa iliyofanyika katika kijiji cha Nkinto.

Mgomo wa wapiga debe na mawakala wa mabasi mjini Singida

Korongo kubwa lililopo katikati ya kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani linalotishia usalama wa watumiaji wa kituo hicho pamoja na magari.
Baadhi ya mawe yaliyotegwa na mawakala na wapiga bede  kwenye lango la kuingilia kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani cha mjini Singida, kwa lengo la kuishinikiza manispaa iweze kuboresha miundo mbinu iliyoharibiwa na mvua zinazoendela kunyesha hivi sasa.

Aua mke kwa rungu akimtuhumu kuchepuka.

Kamanda wa polisi wa mkoa, Kamishina Msaidizi, ACP. Thobias Sedoyeka akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake (hawapo pichani).

WATU wawili wamekufa mkoani Singida katika matukio tofauti yaliyotokea mwishoni mwa wiki, likiwemo la mwanamke mmoja kupigwa na rungu na mumewe kutokana na kile kinachodhaniwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Kamanda wa polisi wa mkoa, Kamishina Msaidizi Thobias Sedoyeka alisema kuwa tukio la kwanza lililotokea kijiji cha Songambele kata ya Ndago wilayani Iramba Jan 11 mwaka huu majira ya saa 1.00 asubuhi  ambapo Maria Shila (57) aliuawa na mumewe Lucas Kitundu (47).

Akisimulia mkasa huo, Sedoyeka alisema kuwa kabla ya tukio hilo wanandoa hao walikuwa na ugomvi wa mara kwa mara ambapo Kitundu alikuwa akimtuhumu mkewe Maria kutokuwa mwaminifu kwenye ndoa yao.

Alisema kuwa siku ya tukio, wanandoa hao walionekana klabu ya pombe ya kienyeji wakiwa wanalumbana na asubuhi ya siku iliyofuata mwili wa Maria uligundulika ukiwa

Thursday, January 22, 2015

Sina dhambi ya kuuawa na bomu, ang’aka DED Iramba

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Iramba mkoa wa Singida, Halima Mpita, akizungumza na waandishi wa habari juu ya bahasha iliyokuwa na bomu lililolenga kumuawa.

MKURUGENZI mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Iramba mkoani Singida,Halima Mpita aliyenusurika kuawa kwa bomu lililokuwa limehifadhiwa ndani ya bahasha,amefunguka na kudai kwamba anaamini hana dhambi ambayo inaweza kusababisha apewe adhabu ya kuawa kwa bomu.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake,Mkurugenzi huyo alisema ajuavyo yeye ni kwamba ndani na nje ya wilaya ya Iramba  hana adui wa kiwango cha kumsukuma adui huyo aweze kutumia njia ya kijasusi ya    bomu kukatisha maisha yake hapa duniani.

Alisema ujumbe alioukuta ndani ya bahasha iliyokuwa na bomu unaosema  kwamba amedhulumu watu/mtu dili ya  shilingi 90 mililoni,ni uwongo mtupu na umepitiliza.

Singida wafanikiwa kupunguza vifo vya uzazi.

Kaimu mganga mkuu mkoa wa Singida, Dk.Ernest Mgeta, akitoa taarifa yake kwenye uzinduzi mpango mkakati wa mkoa wa Singida wa kuongeza kasi ya kupunguza vifo vya akina mama vitokanavyo na uzazi na vifo vya watoto uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Aqua Vitae mjini Singida.Wa kwanza kushoto ni mkuu wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Vicent Kone na anayefuata ni kaimu katibu tawala mkoa wa Singida, Marando.
Mkuu wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Vicent Kone  akizindua rasmi  mpango mkakati wa mkoa wa Singida wa kuongeza kasi ya kupunguza vifo vya akina mama vitokanavyo na uzazi na vifo vya watoto uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Aqua Vitae mjini hapa.
Baadhi ya viongozi na watendaji mkoa wa Singida waliohudhuria wadau uzinduzi mpango mkakati wa mkoa  Singida wa kuongeza kasi ya kupunguza vifo vya akina mama vitokanavyo na uzazi na vifo vya watoto uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Aqua Vitae mjini Singida.

Thursday, January 15, 2015

MTUKURU waua mtoto wa mwaka mmoja Singida

Kamanda wa polisi mkoa wa Singida, ACP Thobias Sedoyeka akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) ofisini kwake.


POLISI mkoani Singida inamshikilia mwanamke mmoja kwa tuhuma ya kusababisha kifo cha mtoto wa mwaka mmoja na mama mtoto kulazwa baada ya kunywa pombe ya ‘Mtukuru’ nyumbani kwa  mtuhumiwa.

Kamanda wa polisi mkoa, Thobias Sedoyeka alimtaja mwanamke anayeshikiliwa kuwa ni Anastazia Kadama (35) mkazi wa kijiji cha Msule, Misughaa wilayani Ikungi mkoani Singida.

Alisema kuwa tukio hilo ni la Jan 07 mwaka huu majira ya saa 3.15 asubuhi kijijini hapo.

Alisema kuwa siku ya tukio, mtuhumiwa Anastazia aliandaa pombe ya kienyeji iitwayo ‘Mtukuru’ kwa ajili ya kuwaalika majirani kwenda kumsaidia kulima shamba lake lakini kwa bahati mbaya siku hiyo mvua kubwa ilinyesha kiasi cha kuzuia shughuli hiyo kufanyika.

Kutokana na kuhofu pombe hiyo kuharibika, mtuhumiwa inadaiwa kuwa aliamua

TRA mkoa wa Singida, yatoa msaada wa madawati shule ya msingi Isanzu wilaya Mkalama.

Meneja TRA mkoa wa Singida, Samson Jumbe (kushoto) akimkabidhi Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Isanzu wilaya ya Mkalama, Sadick Mbiro Abdallah, msaada wa madawati 25 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni mbili. Katikati mwenye miwani ni Afisa elimu kwa umma (TRA),Zakaria.
Meneja wa mamlaka ya mapato (TRA) mkoa wa Singida, Samson Jumbe akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya msingi Isanzu iliyojengwa na Wajerumani mwaka 1934.Wanafunzi hao wamekalia madawati 25 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni mbili yaliyotolewa msaada na TRA mkoa wa Singida.
Moja ya madarasa yaliyojengwa mwaka 1934 na Wajerumani ya shule ya msingi Isanzu wilaya ya Mkalama mkoa wa Singida.Viongozi mbalimbali akiwemo Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida na aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo la Iramba mashariki Mgana Msindai na David Holela aliyewahi kuwa Naibu Waziri wa Ushirika wamesoma katika shule hiyo.Kwa sasa darasa hilo bado linaendelea kutumika.

Tuesday, January 13, 2015

Askofu mstaafu Singida ataka jamii kuepuka vishawishi.

 Kanisa la Pentekoste (FPCT) la mjini Singida.
ASKOFU mstaafu wa kanisa la Pentekoste (FPCT) Singida, mchungaji Paulo Samweli akitekeleza majukumu yake.

ASKOFU mstaafu wa kanisa la Pentekoste (FPCT) Singida, mchungaji Paulo Samweli,amewasihi waumini na wananchi kwa ujumla wajenge utamaduni wa kukataa kushawishiwa kirahisi,kwa njia hiyo wanaweza   kujiepusha na mambo ambayo yanaweza kumsababishia washindwe  kuishi kwa amani na utulivu.

Askofu Samwel ametoa wito huo wakati akihubiri kwenye ibada ya kawaida ya waumini wa kanisa la FPCT la mjini Singida.

Askofu huyo mstaafu, alisema mambo yote maovu likiwemo la uchotaji wa fedha za akaunti ya escrow Tegeta,huanza na

Maandalizi ya ufunguzi wa shule za msingi mkoa wa Singida.



Baadhi ya wabunge mkoa wa Singida wapumulia mashine kwenye nafasi zao majimboni.

Mbunge wa jimbo la Manyoni Mashariki Mh. John Chiligati pamoja na Mbunge wa jimbo la Singida mjini Mh. Mohammed Dewji wakipungia mikono wakazi wa Singida wakati wa mikutano ya chama cha Mapinduzi mkoani humo.


                                                      JIMBO LA MKALAMA.

Hili kwa sasa linafananishwa na ‘mzoga’ kwa madai hadi sasa kuna dalili ya watu 12 wanaonyesha dalili la kuliwania jimbo hilo ambalo zamani lilikuwa likijulikana kwa jina la Iramba mashariki.

Mbunge wa sasa Salome Mwambu wa CCM ambaye anamaliza kipindi chake cha kwanza mwakani,anatarajiwa kutetea nafasi yake hiyo.Hata hivyo anatarajiwa kupata upinzani mkubwa kutoka kwa mwenyekiti wa CCM mkoa wa sasa na mbunge wa zamani wa jimbo la Iramba mashariki,Mgana Msindai.


Baadhi ya watu wengine waliojitokeza ni pamoja na Alan Mkumbo wa TRA makao makuu,Dc wa wilaya ya Nchemba,Francis Izack,Emmanule Mkumbo,mkandarasi Nakei na Emmanuel Mbasha.Hii ni

Miss Singida 2014 Dorice Mollel atoa msaada wa vifaa tiba kwa wodi ya watoto njiti.

Miss Singida 2014 Dorice Mollel akizungumza muda mfupi kabla ya kukabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi ya shilingi 1.2 milioni kwenye wodi ya watoto njiti ya hospitali ya mkoa mjini Singida. Miss Singida huyo ambaye mwaka jana alikuwa pia mshindi wa kwanza Miss kanda ya kati na kushika nafasi ya tatu katika shindano la kumsaka Miss Tanzania, amesema ametoa msaada huo kwa sababu na yeye alizaliwa mapacha njiti.
Miss Singida 2014 Dorice Mollel  akimkabidhi Kaimu Mganga Mfawidhi Hospital ya Rufaa ya mkoa wa Singida, Dk.Daniel Tarimo, msaada wa vifaa mbali mbali vyenye thamani ya zaidi ya shilingi 1.2 milioni kwa wodi ya watoto njiti.
Kaimu Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Singida, Dk.Daniel Tarimo, akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi msaada wa vifaa mbalimbali vya tiba vilivyotolewa msaada na Miss Singida 2014 Dorice Mollel kwenye wodi ya watoto njiti hospitali ya mkoa wa Singida.

Breaking News…DED Iramba alipukiwa na bomu kitandani.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida, ACP.Thobias Sedoyeka, akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Iramba , Halima Hanjali Peter (47) anusurika kuawa kwa kitu kinachodhaniwa kuwa ni bomu la kutengenezwa kienyeji.

MKURUGENZI mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Iramba mkoa wa Singida,Halima Hanjalli Peter (47), amenusurika kifo kwa kitu kinachodhaniwa kuwa bomu kulipukia kitandani kwake.

Kamanda wa jweshi la polisi mkoa wa Singida, ACP  Thobias Sedoyeka, amesema tukio hilo limetokea leo  saa 1.15 asubuhi huko katika eneo la Kiomboi tarafa ya Kisiriri wilaya ya Iramba.

Alisema kitu kinachodhaniwa kuwa ni bomu la kutengenezwa kienyeji kililipuka na kusababisha madhara ikiwemo kutoboa godoro la spring kiasi cha nusu nchi kwenda chini na upana wa nchi mbili.Hata hivyo hakuna mtu/watu waliojeruhiwa katika mlipuko huo isipokuwa godoro na shuka.

Akifafanua,alisema kuwa Desemba 30 mwaka jana saa nne asubuhi Mkurugenzi huyo alipokea bahasha kutoka kwa sekretari wake ambapo ndani ya bahasha hiyo kulikuwa na kadi ya kumpongeza na ndani yake kulikuwa na kikaratasi chenye ujumbe “poleni sana hatuwezi kufanya dili la

Saturday, January 10, 2015

Zoezi la kupima ulevi kwa madereva wa mabasi, latua Singida mjini.

Mrakibu msaidizi wa polisi (ACP) mkuu wa  kitengo cha elimu kwa umma makao makuu ya usalama barabarani jijini Dar-es-salaam, Abel Swai, akiwahamasisha abiria wa basi la kampuni ya France line lililokuwa likitokea Dodoma kwenda Arusha mjini  kutoa taarifa kwa jeshi la polisi endapo watagundua dereva mlevi,kucheleweshwa au gari ni mbovu,ili hatua za haraka ziweze kuchukuliwa.
Pc Damiani Christiani wa polisi mkoa wa Singida, akitumia chombo maalum kupimia madereva wa mabasi endapo wametumia kilevi wakati wakitekeleza majukumu yao.Zoezi hilo lilifanyika kituo cha mabasi cha Misuna mjini Singida na  linatarajiwa kuendelea Shinyanga mjini.

Baba mzazi wa Nyalandu afagilia mwanae kutaka Urais.

Baba yake Waziri wa Maliasili na Utalii na mbunge wa jimbo la Singida kaskazini,(Lazaro Samwel Nyalandu), mzee Samwel Nyalandu akizungumzia uamuzi wa mtotowake  Lazaro kuwania urasi kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwakani. Amedai amepokea uamuzi huo kwa mikono miwili akiamini kuwa Lazaro atamudu nafasi hiyo nyeti ya urais.
Waziri wa Maliasili na Utalii na mbunge wa jimbo la Singida kaskazini,Lazaro Nyalandu, akitangaza rasmi kuwania nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwakani.

BABA mzazi wa Waziri wa Maliasili na Utalii na mbunge wa jimbo la Singida kaskazini, Samwel Nyalandu (70), alisema amepokea kwa mikono miwili kusudio la mtoto wake kuwania nafasi nyeti ya urais, kwa madai kwamba anao uwezo wa kumudu nafasi hiyo.

Amemwasa kwamba endapo atafanikiwa kupata nafasi hiyo na kuwa mkazi wa Singida wa kwanza kuwa rais, ahakikishe anafuata nyayo za watangulizi wake.

“Pia namwomba akifanikiwa aje kuwa karibu zaidi na wananchi. Sikio lake liwe jepesi kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili wananchi atakaokuwa akiwaongoza au kuwatumikia.

Akifafanua zaidi,mzee Samwel alisema kuwa Lazaro alianza kuonyesha kuwa mbele ya safari ya maisha yake atakuwa kiongozi wa watu kwani alipokuwa mtoto mdogo, alikuwa anapenda kukusanya wenzake na kuanza kuwaongoza katika mambo mengi ikiwemo michezo.

Alisema pia alipokuwa shule ya msingi kijiji cha Pohama, alikuwa akiongoza kuanzia darasa la kwanza hadi anamaliza darasa la saba na kuwa mwanafunzi pekee

Friday, January 2, 2015

Nyalandu atangaza rasmi kuwania Urais 2015.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazalo Nyalandu alisalimia wananachi baada ya kuwasili na mkewe Faraja Kota kwenye Mkutano wa jimbo uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Michezo wa Ilongelo, jimboni humo
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazalo Nyalandu alisalimia wananachi baada ya kuwasili na mkewe Faraja Kota kwenye Mkutano wa jimbo uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Michezo wa Ilongelo, jimboni humo.

Singida watumia Bil 1.5/- kutengeneza madaraja.

Kaimu meneja TANROADS mkoa wa Singida, Eng.Leonard Kapongo, akitoa ufafanuzi juu ya matengenezo ya barabara za ngazi ya mkoa, kwenye kikao cha 37 cha bodi ya barabara kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Social Training Centre mjini Singida.

WAKALA wa barabara (TANROADS) mkoani Singida, umetumia zaidi ya shilingi 1.5 biloni kugharamia matengenezo makubwa na madogo ya madaraja ya barabara kuu na za mkoa kwa kipindi cha Aprili hadi Juni mwaka huu.

Hayo yamesemwa na kaimu  meneja TANROADS mkoa wa Singida,Eng.Leonard Kapongo, wakati akizungumza na mwandishi wa SingidaYetuBlog  juu ya utekelezaji wa kazi za barabara kwa kipindi cha Aprili hadi Juni mwaka huu.

Alisema madaraja makubwa ya Mnung’una na Malendi yaliyopo barabara kuu,yalifanyiwa matengenezo makubwa yaliyogharimu zaidi ya shilingi 343.2 milioni.

Aidha,kaimu meneja huyo,alisema jumla ya madaraja

Chadema Singida wapanga kumburuza mahakamani msimamizi wa uchaguzi.

Mjumbe wa kamati ya utendaji CHADEMA manispaa ya Singida, Vicent Mughwai (katikati) akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya kusudio la chama hicho kumfungulia shitaka msimamizi wa uchaguzi wa serikali za mitaa manispaa ya Singida, kwa tuhuma ya kukiuka kanuni za uchaguzi huo. Vicent ndugu yake na mbunge wa jimbo la Singida mashariki na mnadhimu mkuu wa sheria CHADEMA, Tundu Lissu, ametangaza rasmi kumng’oa mbunge wa CCM jimbo la Singida mjini Mohammed Gullam Dewji, kwenye uchaguzi mkuu ujao. Kulia mjumbe wa kamati ya wilaya na katibu kata CHADEMA kata ya Unyambwa na kushoto ni mwenyekiti wa baraza la wazee wilaya CHADEMA Singida mjini.
Baadhi ya viongozi wa ngazi mbalimbali CHADEMA manispaa ya Singida, wakiwa kwenye mkutano wa chama hicho na waandishi wa habari ambapo CHADEMA walitoa taarifa kwa vyombo vya habari juu ya uchaguzi wa serikali za mitaa,vijiji na vitongozi uliomalizika Desemba 14 mwaka huu.

Walimu Singida waidai serikali mil 314/-

Baadhi ya wajumbe wa kikao cha mkoa cha kupangia shule wanafunzi waliofaulu mtihani wa taifa wa kumaliza elimu ya msingi mwaka huu,ili kuanza kidato cha kwanza mwakani.Kikao hicho kilifanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Kanisa Katoliki mjini Singida.

WALIMU mkoani Singida wanaidai serikali zaidi ya sh milioni 314 yakiwa ni malimbikizo ya madeni yao mbalimbali ya siku za nyuma kwa vipindi tofauti hadi kufikia Desemba mwaka huu.

Ofisa elimu wa mkoa wa Singida, Fatma Kilimia alisema mjini hapa mwishoni mwa wiki kuwa walimu mbalimbali wa shule za msingi na sekondari mkoani Singida walikuwa wanaidai serikali jumla ya sh milioni 390.5.

Alikiambia Kikao cha Bodi ya Uchaguzi wa wanafunzi watakaojiunga na Kidato cha Kwanza mwakani  kuwa baada ya halmashauri husika kufanya uhakiki wa kutosha, madeni yote yaliwasilishwa Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI kwa hatua zaidi lakini hadi sasa ni sh milioni 76.4 tu zimelipwa.

Kwa mujibu wa Kilimia, walimu wa Halmashauri ya wilaya ya Ikungi wanaidai serikali jumla ya sh milioni

11,380 Singida, wachaguliwa kujiunga kidato cha kwanza

Katibu tawala mkoa wa Singida, Liana Hassan, akizungumza kwenye kikao cha mkoa cha kupangia shule wanafunzi waliofaulu mtihani wa taifa wa kumaliza elimu ya msingi mwaka huu,ili kuanza kidato cha kwanza mwakani.Wa kwanza kulia ni katibu tawala msaidizi kwa upande wa sekta ya elimu sekretarieti ya Mkoa,Fatuma Kilimia na kushoto ni mkuu wa wilaya ya Singida,Queen Mlozi.
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Singida, Christowaja Mtinda, akizungumza kwenye kikao cha mkoa cha kupangia shule wanafunzi waliofaulu mtihani wa taifa wa kumaliza elimu ya msingi mwaka huu, ili kuanza kidato cha kwanza mwakani.

Mwendesha bodaboda atekwa na kuchinjwa Singida.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida, ACP, Thobias Sedoyeka.

WATU watatu mkoani Singida,wamefariki dunia katika matukio tofauti, likiwemo la dereva wa boda boda kuchomwa kisu shingoni na usoni juu ya jicho la kushoto.

Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Singida,ACP,Thobias Sedoyeka,alimtaja dereva wa boda boda aliyechomwa kisu na kufariki dunia,kuwa ni Sudi Jumanne (26) mkazi wa Sabasaba mjini hapa.

Alisema mwili wa dereva Sudi uliokotwa na raia wema Novemba 22 mwaka huu saa moja asubuhi,huko maeneo ya uwanja wa ndege mjini hapa.

 Sedoyeka alisema Sudi alichomwa kisu na mtu/watu wasiofahamika shingoni karibu na bega la kushoto na usoni juu ya jicho la kushoto.

Kamanda huyo alisema katika tukio la pili,Kundi Oshima (75) mkulima na mkazi wa kijiji cha Iyumbu wilaya ya Ikungi,amefariki dunia baada ya kukatwa katwa mapanga kisogoni, shavu la kushoto na mtu/watu wasiofahamika.

Alisema tukio hilo limetokea Novemba 22 mwaka huu saa saba usiku huko katika kijiji na kata ya Iyumbu tarafa ya Ihanja wilaya ya Ikungi.

“Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa chanzo cha mauaji hayo,ni imani ya kishirikina.Kwa sasa tunamshikilia Dalush Mwandu (51) kwa mahojiano zaidi”,alisema.

Sedoyeka alisema pia Novemba 23 mwaka huu saa 10.20 jioni huko katika maeneo ya bwawa Singidani mjini hapa,kitoto kichanga kinachokadiriwa kuwa na umri wa siku mbili cha kiume,kimeokotwa kikiwa kimefariki dunia.

“Chanzo cha kutupwa kwa motto huyo,bado hakijajulikana na hakuna mtu/watu waliokamatwa kuhusiana na tukio hilo”.alisema kamanda Sedoyeka.

Mwakyembe atamani benki ya bodaboda