Saturday, January 10, 2015

Zoezi la kupima ulevi kwa madereva wa mabasi, latua Singida mjini.

Mrakibu msaidizi wa polisi (ACP) mkuu wa  kitengo cha elimu kwa umma makao makuu ya usalama barabarani jijini Dar-es-salaam, Abel Swai, akiwahamasisha abiria wa basi la kampuni ya France line lililokuwa likitokea Dodoma kwenda Arusha mjini  kutoa taarifa kwa jeshi la polisi endapo watagundua dereva mlevi,kucheleweshwa au gari ni mbovu,ili hatua za haraka ziweze kuchukuliwa.
Pc Damiani Christiani wa polisi mkoa wa Singida, akitumia chombo maalum kupimia madereva wa mabasi endapo wametumia kilevi wakati wakitekeleza majukumu yao.Zoezi hilo lilifanyika kituo cha mabasi cha Misuna mjini Singida na  linatarajiwa kuendelea Shinyanga mjini.




PC.Abdalla Ramadhani kutoka trafiki makao makuu Dar-es-salaam,akitumia chombo maalum kupimia madereva wa mabasi endapo wametumia kilevi wakati wakitekeleza majukumu yao.Zoezi hilo lilifanyika kituo cha mabasi cha Misuna mjini Singida na linatarajiwa kuendelea Shinyanga mjini.

MRAKIBU msaidizi wa polisi makao makuu kitengo cha elimu kwa umma usalama barabarani (trafiki) ACP, Abel Swai, amewataka madereva wa mabasi nchini, kuhakikisha wanakuwa watanashati kwa kuvaa nguo zinazolingana na unyeti wa kazi yao,ili waweze kujijengea mazingira mazuri ya kukubalika na kuaminika na wateja wao (abiria.

ACP Swai metoa wito huo  wakati akisimamia zoezi la kupima ulevi madereva wa mabasi na kuhakikisha sheria,taratibu na kanuni za usalama barabarani kama zinatekelezwa ipasavyo. Zoezi hilo lilifanyika katika kituo kikuu cha mabasi mjini Singida.

Alisema kwamba wapo baadhi ya madereva wa mabasi licha ya kutofaa sare ya kampuni zao akiwa barabarani,wanavaa nguo ambazo hazifafani na heshima ya kazi anayoifanya, kitendo ambacho baadhi ya abiria kupunguza imani kwake kwa kudhani sio dereva makini.


“Kazi ya udereva wa mabasi ina heshima ya kipekee.Kwa hiyo ni lazima dereva pamoja na kutekeleza kazi yake kikamilifu,pia anapaswa awe nadhifu kwa mavazi yake na vitendo vyake vingi vikubalike mbele ya jamii”,alifafanua zaidi ACP Swai.

Kuhusu zoezi lao,mrakibu huyo msaidizi, alisema sambamba  na zoezi la kudumu la kupima madereva walevi,pia wamekuwa wakikangua madereva watumiaji wa vyombo vya moto,watembea kwa miguu na wasukuma matoroli kama wanazingatia kikamilifu sheria zote za usalama barabarani bila shuruti.

“Lengo letu ni kuwakumbusha madereva,abiria na wananchi kwa ujumla wajibu wao wawapo barabarani.Abiria kama wanagundua gari wanalosafiria ni mbovu,wamecheleweshwa,dereva ni mlezi au makosa yoyote ya jinai, atoe taarifa haraka kwa jeshi la polisi. Hali kadhalika madereva watimize wajibu wao kwa mujibu wa sheria.Wakati wote wazingatie au waheshimu alama na mistari iliyowekwa barabarani”alisema.


Alisema endapo kila Mtanzania atatambua anatakiwa afanye nini ili kuokoa maisha ya mwezake,ajali ya barabarani zinazopotesha maisha ya watu na mali zao,zitapungua kwa kiasi mkikubwa.

ACP Swai ametumia fursa hiyo kuwakumbusha madereva kuacha kutumia pombe wakati wakiwa barabarani kwa madai kwamba zinasabaisha wakose umakini na kunza kutoa maamuzi ambayo ni hatari kwao na wateja wao.Pia amesema ni marufuku mabasi ya masafa marefu kuwa na dereva mmoja,ni lazima wawe wawili.


Katika zoezi la kupima madereva watumiaji wa pombe wakiwa barabarani, lililofanyika mjini hapa jana,madereva wawili  wa nje ya mkoa huu,waligundulika kutumia pombe na wanashikiliwa na jeshi la polisi mjini hapa.

No comments:

Post a Comment