Wednesday, April 29, 2015

Wanachama wa CHF Iramba wakosa dawa.

Pichani ni majengo ya kituo cha afya cha tarafa ya Ndago, wilayani Iramba yanayokabiliwa na uhaba mkubwa wa dawa kwa wanachama wake wa Mfuko wa afya ya jamii (CHF)katika kipindi cha miezi mitatu kuanzia Oktoba hadi disemba,mwaka jana

LICHA ya Wilaya ya Iramba,Mkoani Singida kutajwa kuongoza nchini kwa kuwa na wanachama wengi  wa Mfuko wa Afya  ya Jamii Nchini (CHF) baada ya zaidi ya asilimia 60 ya kaya zake kujiunga,lakini bado kuna malalamiko ya huduma duni za afya katika baadhi ya vituo vyake.

Wakizungumza na mwandishi wa habari  hizi,baadhi ya wanachama wa Mfuko huo wamedai kuwa pamoja na kutoa fedha kwa ajili ya kujiunga na CHF ili kuwa na uhakika wa matibabu pindi watakapougua,lakini katika Kituo cha Afya cha Tarafa ya Ndago,wilayani humo bado huduma  ni mbovu.

Walidai kuwa kwa zaidi ya miezi minne sasa,kila wanapokwenda kufuata huduma za matibabu katika kituo hicho cha afya wamekuwa hawapatiwa dawa za magonjwa mbalimbali yanayowasumbua.

Walisema kuwa kutokana na kukosekana kwa dawa katika kituo hicho,wanachama hao wa CHF wamekuwa

Saturday, April 25, 2015

Chadema yajiimarisha yaendesha mikutano ya mafunzo Singida.

Mkurugenzi wa organization na mafunzo CHADEMA Taifa, Benson Kigaila, akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika jana kwenye uwanja wa Peoples mjini Singida  ukiwa na lengo na kuzindua mafunzo yanayoendelea kutolewa nchini kote na chama hicho, kujiimarisha kwa ajili ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika oktoba mwaka huu.

Baadhi ya wanaCHADEMA na wananchi wa mji wa Singida, waliophudhuria mkutano wa hadhara ulioitishwa kwa ajili ya kumsikiliza mkurugenzi wa organization na mafunzo wa CHADEMA Taifa, Benson Kigaila (hayupo kwenye picha) kwenye viwanja vya Peoples mjini Singida.

Mvua zaathiri hekta 2,000 za zao la Pamba Mkoani Singida.

Mkuu wa wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Gishuli Charles (kulia) akitoa maelekezo juu ya mikakati ya kuboresha kilimo cha pamba mbele ya wajumbe wa kikao cha kazi cha kutathimini zao la pamba msimu huu kilichohudhuriwa na wajumbe kutoka bodi ya pamba na wadau wa zao hilo. Dc Charles alikuwa mwenyekiti wa kikao hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa mjini hapa. Kushoto ni kaimu katibu tawala mkoa wa Singida,Mumba.
Baadhi ya wajumbe wa kikao cha kazi cha kutathimini kilimo cha pamba cha msimu huu kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa mjini Singida.

Wizara ya afya yafuta vibali vilivyotolewa na maafisa utamaduni kwa waganga wa tiba mbadala.

Mkuu wa kituo kidogo cha polisi Ndago, Bw.Richard Kimolo (kushoto), Diwani wa kata ya Mbelekese, Bi Monica Samweli (wa pili kutoka kushoto), Katibu mkuu CHAWAMAMU Mkoa wa Singida, Dk.Tano Mika Likapakapa wakiwa kwenye semina ya operesheni tomomeza mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) na vikongwe inayoendelea tarafa ya Ndago, wilayani Iramba.
Mratibu wa Tiba Asilia kutoka Hospitali ya wilaya ya Iramba, Bi Dora Yona(wa pili kukulia) akijiandaa kutoa mada ya waganga wa tiba mbadala kufuata sharia,kanuni na taratibu za utoaji tiba kwa wateja wao.

Pato la mkulima wa Tumbaku nchini limeongezeka na kufikia milioni 4.9 kwa mwaka.

Mkuu wa wilaya ya Manyoni mkoani Singida,Fatma Toufiq, akifungua mkutano wa wadau wa zao la Tumbaku nchini unaoendelea kwenye ukumbi wa mikutano wa chuo cha VETA mjini Singida.Dc huyo alifungua mkutano huo kwa niaba ya mkuu wa mkoa.
Baadhi ya viongozi na wadau wa zao la Tumbaku nchini wanaohudhuria mkutano wa kujadili maendeleo ya zao hilo hapa nchini.

KOICA wakipiga jeki chuo cha walemavu Sabasaba Singida.

Kaimu mwakilishi wa shirika la KOICA Tanzania, Jieun Park, akizungumza kwenye sherehe za uzinduzi rasmi wa mradi wa uboreshaji wa miundombinu ya chuo cha ufundi kwa watu wenye ulemavu cha Sabasaba mjini Singida.Kushoto ni mkuu wa wilaya ya Singida, Saidi Alli Amanzi na kushoto ni mwenyekiti wa walemavu wa ngozi mkoa wa Singida.
Mkuu wa chuo cha ufundi kwa watu wenye ulemavu cha Sabasaba manispaa ya Singida, Fatuma Malenga,akitoa taarifa yake kwenye sherehe ya uzinduzi wa mradi wa uboreshaji wa miundombinu ya chuo hicho unataorajiwa kutumia zaidi ya shilingi 42.8 milioni zizotolewa msaada na shirika la Korea kusini, KOICA. Kulia ni mkuu wa wilaya ya Singida, Saidi Alli Amanzi.

Singida yawaonya Waganga wa tiba mbadala kutofanya mapenzi na wateja wao wanaowahudimia.

Maafisa watendaji wa vijiji,kata,Wenyeviti wa vitongoji pamoja na wenyeviti wa vijiji waliohudhuria kwenye semina elekezi juu ya operesheni tokomeza mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi(albini) na vikongwe iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa kituo cha walimu Ndago.
Mratibu wa Tiba Asilia kutoka Hospitali ya wilaya ya Iramba,Bi Roda Yona akitoa mada katika semina hiyo ambayo pia elekezi juu ya operesheni tokomeza mauaji ya watu wenye ulemavu (albino) na vikongwe iliyofanyika kata ya Ndago.

World Vision Tanzania yatumia zaidi ya bilioni 5.3 kuboresha miradi ya Afya Singida.

Kaimu mkuu wa mkoa wa Singida, Saidi Alli Kamanzi na DC wa wilaya ya Singida, akifungua hafla ya makabidhiano wa mradi wa afya ya mama na mtoto (SUSTAIN-MNCH). Wa kwanza kulia ni mkuu wa wilaya ya Ikungi Gichulu Charles na anayefuatia ni mwakilishi wa mkurugenzi wa shirika la World vision Tanzania, Mary Lema.
Baadhi ya wadau wa afya waliohudhuria hafla ya makabidhiano ya mradi wa afya ya mama na mtoto (SUSTAIN -MNCH) iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Aque Vitae Resort mjini Singida.

Shirika la Helvetas kutumia Bilioni 2.7 kuwezesha Wanawake wa Singida katika kilimo cha Mboga na matunda.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Helvetas Tanzania, Daniel Kilimbiya, akitoa mada yake ya utambulisho wa mradi wa awamu ya pili wa kuwawezesha wanawake kulima mboga mboga na matunda ili waweze kujikomboa kiuchumi. Semina hiyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Aqua Vitae mjini hapa, ilihudhurudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo kutoka wilaya ya Singida vijijini, Iramba na Mkalama.
Meneja SIDO mkoa wa Singida Shoma Kibende, akitoa nasaha zake kwenye semina ya siku moja ya uhabarisho wa mradi awamu ya pili unaolenga kuwawezesha wanawake kulima kilimo bora cha mboga mboga na matunda.

Waganga wa tiba mbadala Singida wanaotumia nyara za Serikali kupigia ramli chonganishi watakiwa kuzisalimisha Polisi.

Katibu Mkuu wa CHAWAMAMU Mkoa wa Singida, Dk.Tano Mika Likapakapa (wa kwanza kulia)Mwenyekiti wa serikali ya Kijiji cha Lunsanga,Bw.Richard Kisiwa (katikati) na Mkuu wa Kituo kidogo cha polisi Ndago, Bw.Richard Kimolo.
Afisa kilimo wa kata ya Ndago, Bi Perpetua Pius (kushoto) na Mratibu wa Tiba Asilia kutoka Hospitali ya wilaya ya Iramba,Bi Roda Yona(kulia).

CHAWAMAMU waendesha mafunzo Singida kukabiliana na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi.

Mratibu wa Tiba Asilia kutoka Hospitali ya Wilaya ya Iramba, Bi Roda Yona(kushoto) na Mkuu wa Kituo kidogo cha polisi Ndago, Bwana Richard Kimolo (kulia) wakishiriki mafunzo ya kutoa elimu juu ya operesheni tokomeza mauji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) na vikongwe.
Katibu Msaidizi wa CHAWAMAMU Mkoa wa Singida, Bwana Omari Majengo (kulia) wakiwa kwenye ukumbi wa shule ya msingi Urughu, tarafa ya Ndago wilayani Iramba wakitoa elimu juu ya operesheni tokomeza mauji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) na vikongwe na Kushoto ni Afisa tarafa wa tarafa ya Ndago, Bwana Anthoni Magesa Ntarle.

Wednesday, April 8, 2015

Sherehe za maadhimisho ya siku ya utundikaji mizinga kimkoa yafana.

Mkuu wa mkoa wa Singida Dk.Parseko Kone, akishiriki kutundika mizinga ya nyuki katika siku ya maadhimisho ya utundikaji mizinga kitaifa ambapo kimkoa yamefanyika katika kijiji cha Pohama jimbo la Singida kaskazini.

Vijana wawili wakazi wa kijiji cha Pohama jimbo la Singida kaskazini, wakiteremka baada ya kumaliza kutundika mizinga ya nyuki katika siku ya maadhimisho ya utundukaji wa mizinga kitaifa ambapo kimkoa yalifanyika katika kijiji cha Pohama.