Saturday, April 25, 2015

KOICA wakipiga jeki chuo cha walemavu Sabasaba Singida.

Kaimu mwakilishi wa shirika la KOICA Tanzania, Jieun Park, akizungumza kwenye sherehe za uzinduzi rasmi wa mradi wa uboreshaji wa miundombinu ya chuo cha ufundi kwa watu wenye ulemavu cha Sabasaba mjini Singida.Kushoto ni mkuu wa wilaya ya Singida, Saidi Alli Amanzi na kushoto ni mwenyekiti wa walemavu wa ngozi mkoa wa Singida.
Mkuu wa chuo cha ufundi kwa watu wenye ulemavu cha Sabasaba manispaa ya Singida, Fatuma Malenga,akitoa taarifa yake kwenye sherehe ya uzinduzi wa mradi wa uboreshaji wa miundombinu ya chuo hicho unataorajiwa kutumia zaidi ya shilingi 42.8 milioni zizotolewa msaada na shirika la Korea kusini, KOICA. Kulia ni mkuu wa wilaya ya Singida, Saidi Alli Amanzi.

Mkuu wa wilaya ya Singida, Saidi Alli Amanzi, akizungumza kwenye sherehe za uzinduzi wa mradi wa uboreshaji wa miundombinu katika chuo cha ufundi cha watu wenye ulemavu cha Sabasaba mjini Singida.
Mkuu wa wilaya ya Singida, Saidi Alli Amanzi, akimkabidhi mdau wa kujitolea, Jo Yunsil Chilly, cheti cha utambuzi wake katika kusaidia kupatikana kwa zaidi ya shilingi 42.8 milioni kwa ajili ya kuboresha miundombinu za chuo cha ufundi kwa watu wenye ulemavu Sabasaba manispaa ya Singida.
Mkuu wa Singida Saidi Alli Amanzi akizindua moja ya mabweni yaliyofanyiwa ukarabati chini ya mradi wa uboreshaji wa miundombinu ya chuo cha ufundi kwa watu wenye ulemavu manispaa ya Singida. Kushoto kwake ni Kaimu mwakilishi wa shirika la KOICA Tanzania, Jieun Park.
 Baadhi ya viongozi waliohudhuria sherehe ya uzinduzi rasmi wa mradi wa uboreshaji miundombinu ya chuo cha ufundi kwa watu wenye ulemavu cha Sabasaba manispaa ya Singida.
Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha ufundi kwa watu wenye ulemavu waliohudhuria sherehe ya uzinduzi rasmi wa mradi wa uboreshaji miundombinu ya chuo cha ufundi kwa watu wenye ulemavu cha Sabasaba manispaa ya Singida.

Serikali ya Korea kusini kupitia shirika lake la KOICA Tanzania,imetoa msaada wa zaidi ya shilingi 42.8 milioni kwa ajili ya kugharamia mradi wa ukarabati wa chuo cha ufundi kwa watu wenye ulemavu cha Sabasaba mjini hapa.

Hayo yamesemwa juzi na kaimu mwakilishi wa shirika la KOICA Tanzania, Jieun Park,wakati akizungumza kwenye sherehe za uzinduzi rasmi wa mradi wa uboreshaji wa miundombinu rafiki kwa watu wenye ulemavu wa chuo hicho.

Alisema msaada huo ni sehemu ya sera rasmi ya serikali ya Korea kusini ya misaada ya maendeleo ya kukuza maendeleo katika ngazi za chini.

“Katika mradi huu,pia tutajenga matanki ya maji safi na salama katika mabweni na bwalo la chakula,ili kuzuia wanafunzi kupata magonjwa ya mlipuko kama vile homa ya matumbo na kuharisha”,alifafanua Park.

Aidha kaimu mwakilishi huyo, alisema mradi huo unalenga kuhamasisha uelewa wa jamii juu ya ulemavu na kuwezesha jamii ishiriki katika kutambua umuhimu wa kushiriki kusaidia walemavu wapate fursa sawa ya kushiriki mambo mbalimbali ya jamii.

“Walemavu ni wanajamii muhimu wanaochangia katika uhamasishaji wa nguvu kazi ya kitaifa na kimataifa,hivyo ni muhimu mno wapate haki sawa za kushiriki na kuishi kama raia wengine wasio na ulemavu”alifafanua zaidi.

Kwa upande wake mkuu wa chuo hicho, Fatuma Malenga, alisema chuo pia kimechangia mradi huo shilingi 4.5 milioni.

Malenga alitaja baadhi ya shughuli zizofanyika kuwa ni pamoja na upanuzi wa bweni la wavulana kwa kuongeza vyumba vinne,ujenzi wa vyoo vitatu maalum kwa wanafunzi wanaotumia wheelchair na ujenzi wa njia za kupita kwa wenye wheelchair kwa bweni la wavulana.

Naye mgeni rasmi katika sherehe hiyo mkuu wa wilaya ya Singida Saidi Alli Amanzi,alitumia fursa hiyo kulishukuru shirika la KOICA kupitia volunteer wake Jo Yunsil maarufu kwa jina la Chilly,kwa ufadhi wa mradi wa uboreshaji miundombinu rafiki kwa walemavu wa chuo cha Sabasaba.


Aidha, Dc huyo aliagiza mamlaka zinazohusika ziweke alama za kuonyesha uwepo wa watu wenye ulemavu kwenye barabara inayopita jirani sana na chuo hicho,ili kuimarisha usalama wa walemavu chuo hicho.

No comments:

Post a Comment