Thursday, May 7, 2015

Sherehe za sikukuu ya wafanyakazi duniani (Mei Mosi) mkoa wa Singida zafana.

Mkurugenzi mtendaji wa halmshauri ya wilaya ya Iramba mkoa wa Singida, Halima Mpita (wa kwanza kushoto akishirikiana na viongozi wa ngazi mbali mbali mkaoni Singida, kuimba wimbo wa mshikamano kwenye kilele cha sherehe za wafanyakazi duniani (mei mosi) zilizofanyika jana kwenye uwanja wa Namfua mjini hapa.
Kaimu mkuu wa mkoa wa Singida, Saidi Alli Amanzi (wa pili kushoto) akishiriki kuimba wimbo wa mshikamano kwenye kilele cha sherehe za wafanyakazi duniani (mei mosi) zilizofanyika jana kwenye uwanja wa Namfua mjini Singida.
Baadhi ya wafanyakazi wa TANROADS mkoa wa Singida wakiongozwa na meneja wao mhandisi Leonard Kapongo (katikati mbele anayepiga makofi) wakishiriki maandamano ikiwa ni sehemu ya sherehe ya sikukuu za wafanyakazi duniani zilizofanyika kwenye uwanja wa Namfua mjini hapa.

Moja ya mabango kwenye sherehe za wafanyakazi-mei mosi, kutoka hospitali teule ya wilaya ya Singida iliyopo katika kijiji cha Makiungu, likihimiza awafanyakazi kujiandikisha kupiga kura na serikali ilipe mapunjo yote, mishahara kabla ya uchaguzi mkuu oktoba 2015.
Mratibu wa TUCTA mkoa wa Singida, Edwin Nampesya, akisoma risala ya shirikisho la vyama uhuru vya wafanyakazi Tanzania (TUCTA) mkoa wa Singida, kwenye kilele cha sherehe za wafanyakazi duniani (mei mosi) zilizofanyika kwenye uwanja wa Namfua mjini hapa.
Kaimu mkuu wa mkoa wa Singida na DC wilaya ya Singida, Saidi Alli Amanzi, akimkabidhi cheti cha mfanyakazi bora Nyalandu, ambaye ni Katibu tarafa wa tarafa ya Nduguti wilaya ya Mkalama, jana kwenye kilele cha sherehe za wafanyakazi duniani (mei mosi) zilizofanyika kwenye uwanja wa Namfua mjini hapa.

No comments:

Post a Comment