Thursday, May 14, 2015

Singida wasogezewa karibu huduma ya Benki ya Posta Tanzania.

Mwenyekiti wa Benki ya Posta nchini, Lettice Rutashobya (kulia) akimkabuidhi kadi ya benki Mwenyekiti wa mtaa wa Majengo mjini Singida, Stamili Shomari baada ya kupewa offer na benki hiyo kufungua akaunti.
Afisa  Mtendaji Mkuu wa benki ya Posta nchini, Sabasaba Moshingi,akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa tawi la benki ya Posta mjini Singida.

Mwenyekiti wa benki ya Posta nchini, Profesa Lettice Rutashobya, akizungumza kwenye sherehe za uzinduzi wa benki ya posta tawi la Singida.Prof.Rutashobya, ametoa wito kwa Watanzania kufungua akaunti kwenye benki hiyo kwa madai haina kabisa urasimu au mteja kuombwa asilimia kumi ya mkopo. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa mkoa wa Singida, Saidi Alli Amanzi na kulia ni Mstahiki Meya wa manispaa ya Singida,Sheikh Salum Mahami.
Mwenyekiti wa benki ya Posta nchini, Profesa Lettice Rutashobya, akizungumza kwenye sherehe za uzinduzi wa benki ya posta tawi la Singida.Prof.Rutashobya, ametoa wito kwa Watanzania kufungua akaunti kwenye benki hiyo kwa madai haina kabisa urasimu au mteja kuombwa asilimia kumi ya mkopo. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa mkoa wa Singida, Saidi Alli Amanzi na kulia ni Mstahiki Meya wa manispaa ya Singida,Sheikh Salum Mahami.
Baadhi ya wakazi wa mji wa Singida, wakifungua akaunti muda mfupi baada ya benki ya Posta tawi la Singida, kuzinduliwa rasmi.
Baadhi ya watumishi wa benki ya Posta tawi la Singida,waliohudhuria sherehe za uzinduzi wa tawi hilo.

BENKI nyingi nchini zimeacha utamaduni wa kuwanufaisha wateja wake kwa kuwapatia  riba nzuri, na badala yake zimejikita zaidi katika kuwakata gharama kubwa ya uendeshaji,kitendo kinachochangia Watanzania wengi kuogopa kuhifadhi fedha zao benki;imeelezwa.

Akizungumza kwenye sherehe ya uzinduzi wa benki ya posta Tanzania (TPB), Kaimu Mkuu wa mkoa wa Singida na DC wa wilaya ya Singida, Saidi Alli Amanzi, alisema siku hizi Watanzania wachache wanaweka fedha zao benki sio kwamba watanufaika na kitendo hicho,bali wanaogopa wezi.

“Sio uongo,siku hizi ukihifadhi fedha benki,zitaliwa  tu kutokana na gharama za uendeshaji kuwa juu.Naziomba benki ziangalie uwezekano wa kutoa rida nzuri kwa wateja wake, ili ziweze kuvutia Watanzania wengi zaidi kutunza/kuweka fedha zao katika mabenki”,alifafanua  Amanzi.


Aidha, Kaimu mkuu huyo wa mkoa, ametumia fursa hiyo kuwataka Watanzania kuacha kukimbilia kujiunga na mabenki ya nje ya nchi, na badala yake wajiunge kwa wingi na mebenki yetu,ili kuendeleza chetu.

Awali Afisa Mtendaji wa TPB, Sabasaba Moshingi, alisema uamuzi wa kufungua tawi mkoani Singida,umetokana na maombi mengi kutoka kwa wakazi mkoani humu wakidai wanataka kunufaika na huduma bora zinazotolewa na TPB.

“Ninayo furaha kubwa kuona kuwa leo hii ndoto hiyo inatimia na hivyo kuweza kukidhi kilio cha wakazi wa mkoa wa Singida.Tunawaahidi kuwa watafaidika na huduma zetu bora na zenye gharama nafuu sana”alifafanua Moshingi.

Akifafanua zaidi, alisema pia wakazi wa mkoa wa Singida watanufaika na mikopo ya aina mbalimbali inayotolewa na TPB ambayo inakidhi mahitaji ya vikundi,wafanyabiashara wadogo na wakubwa,mikopo ya wafanyakazi na hata wastaafu.

Kwa mujibu wa Moshingi, katika kipindi cha mwaka jana,benki ya posta ilifanikiwa kukuza mikopo kwa aslimia 59 kutoka shilingi 119.7 bilioni hadi shilingi 190 bilioni.

Kwa upande wa amana za wateja zilikuwa kwa aslimia 41 kutoka shilingi 170 bilioni mwaka 2013 hadi shilingi 240.1 bilioni mwaka jana na pia raslimali za benki zilikuwa na kufikia shilingi 297.7 bilioni kutoka shilingi 200.8 bilioni ambayo ni sawa na aslimia 48.


Wakati huo huo, Mwenyekiti wa benki ya TPB,Profesa Lettice Ruta…..amewataka wakazi wa mkoa wa Singida na hasa waishio vijijini,kuomba uwakala wa benki ya TPB,ili kusogeza karibu zaidi huduma za kibenki ambazo zina ubora wa hali ya juu.

No comments:

Post a Comment