Tuesday, May 19, 2015

Wagombea wa nafasi za uongozi Mkalama waonywa kutochafuana katika kipindi hiki.

Mbunge wa viti maalumu (CCM) Mkoa wa Singida, Bi Martha Mlata (wa pili kutoka kulia) akimkabidhi pikipiki Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Mkalama, Bi Elipendo Machafuko (aliyepanda pikipiki) atakayotumia kuwatembelea wanachama wa jumuiya hiyo. Wengine walioshuhudiwa hafla ya makabidhiano hayo ni pamoja na Katibu wa CCM wilaya ya Mkalama,Bw.Amosi Shimba(wa kwanza kulia),Bi Hadija Kisuda-mwenyekiti wa UWT wilaya ya Singida vijijini(wa tatu kutoka kulia) na katibu wa UWT Mkoa wa Singida,Bi Anjela Robert(wa kwanza kutoka kushoto).
Mbunge wa viti maalumu (CCM) Mkoa wa Singida, Bi Martha Mlata (wa kwanza kulia) akiwakabidhi makatibu wa matawi ya jumuiya ya UWT baiskeli moja kwa kila kata.

Mbunge wa viti maalumu(CCM)Mkoa wa Singida, Bi Martha Mosses Mlata akiongea na wananchi pamoja na wanachama wa UWT Kata ya Ibaga, tarafa ya Kirumi alipokuwa katika ziara ya kukiimarisha chama cha Mapinduzi wilayani Mkalama.
Katibu wa UWT Mkoa wa Singida, Bi Anjela Robert (wa kwanza kushito) akimuelekeza mbunge wa viti maalumu (CCM) Mkoa wa Singida,Bi Martha Mlata(wa pili kutoka kulia) kuonyesha zawadi aliyowapelekea wanachama wa jumuiya hiyo.Wengine ni Bi Christina S.Hamisi (wa kwanza kulia), Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Mkalama, Bi Elipendo Machafuko (wa tatu kutoka kulia) na mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Iramba, Bi Jenifer Miano (wa pili kutoka kushoto).
Katibu wa CCM wilaya ya Mkalama, Bw.Amosi Shimba (wa pili kutoka kushoto) akimkabidhi zawadi ya Mbuzi aliyetolewa na wanachama wa jumuiya hiyo.Wengini ni Mbunge wa viti maalumu (CCM) Mkoa wa Singida, Bi Martha Mlata (wa pili kutoka kulia) akimpokea Mbuzi, Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Ikungi, Bi Christina S.Hamisi (wa tatu kutoka kulia), Bi Jenifer Miano-Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Iramba (wa nne kutoka kulia)na Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Singida vijijini, Bi. Hadija Kisuda (wa tano kutoka kushoto).
Katibu msaidizi wa CCM Wilaya ya Mkalala, Bi Martha Zingula (wa pili kutoka kulia) akimkaribisha Mbunge wa viti maalumu(CCM) Mkoa wa Singida, Bi. Martha Mlata(wa tatu kutoka kulia) alipotembelea wilayani hapa kwa ziara ya kukiimarisha chama na wa nne kutoka kulia ni Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Singida vijijini, Bi Hadija Kisuda.
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la UWT wilaya ya Mkalama waliohudhuria kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa ofisi za Chama cha Mapinduzi(CCM) Wilaya ya Mkalama.
Baadhi ya pikipiki zilizokabidhiwa kwa wenyeviti wa wilaya wa UWT katika Mkoa wa Singida kwa lengo la kuwarahisishia suala la usafiri.

CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) Wilaya ya Mkalama kimekemea tabia ya baadhi ya wanachama wake wenye nia ya kutaka kugombea nafasi za uongozi kwenye uchaguzi mkuu ujao wa Rais,wabunge na madiwani baadaye mwaka huu kuacha mara moja kuanza kuwachafua viongozi waliopo madarakani.

Onyo hilo limetolewa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wilaya ya Mkalama, Elipendo Machafuko alipokuwa kifungua kikao cha baraza la jumuiya hiyo wilayani Mkalama, mara tu baada ya kumpokea Mbunge wa viti maalumu (CCM) Mkoa wa Singda, Matha Mlata aliyekuwa na ziara ya siku moja wilayani hapa.

Kwa mujibu wa Machafuko wakati wakielekea kwenye uchaguzi mkuu mwezi oktoba,mwaka huu kumeanza kujitokeza wingu la watu wenye nia ya kugombea nafasi za uongozi kuanza kuwachafua viongozi waliopo madarakani,jambo ambalo linaweza kuleta mfarakano ndani ya chama.

“Tunaenda kwenye mchakato wa uchaguzi,liko wingu la kuchafuana sanaa..kama unamchafua Matha Mlata bado yupo madarakani, hivi wewe ukichafuliwa utafurahi, utatabasamu, ukimchafua mwenyekiti wa Halmashauri wakati bado anatawala kule Halmashauri atafurahi,iko hii tabia,ipoo?alihoji  mwenyekiti huyo wa UWT Mkalama.

Akizungumza na wajumbe wa baraza la UWT wilaya ya Mkalama,Mbunge wa viti maalumu (CCM) Mkoa wa Singida, Martha Mlata alisema demokrasi ndani ya Chama Cha Mapinduzi ni ya kujivunia sana kwani inampa nafasi kila mwanachama kugombea,kuchagua na kuchaguliwa katika nafasi yeyote ya uongozi.

“Jamani ndani ya chama cha mapinduzi kuna demokrasia,simmeona watu wengine demokrasia hamna sasa hivi tu mnyukano,sisi kuna demokrasia inapofika wakati watu wanajitokeza ili watu wawapime,watu wachaguliwe” alisisitiza Mlata


Hata hivyo Mlata ambaye pia ni mjumbe wa Baraza la UWT Taifa aliwaweka wazi wanachama wa jumuiya hiyo kuwa yeyote yule mwenye nia na uwezo wa kuwatumikia wananchi wa Mkoa huo wakati ukifika wajitokeze kuchukua fomu na kujaza ili waombe nafasi zitakazotangazwa na chama.

Naye Katibu wa UWT Mkoa wa Singida, Angela Robert Milembe alitumia fursa hiyo kuwatahadharisha watendaji wa jumuiya hiyo kwamba msaada wa vitendeakazi vilivyotolewa na Mbunge Mlata visije vikawa chanzo cha kuwafarakanisha na badala yake viwazidishie umoja na mshikamano zaidi.

Awali katibu wa CCM wilaya ya Mkalama, Amosi Shimba akimkaribisha Mjumbe huyo wa Baraza la UWT Taifa aliwahakikishia wajumbe na wanachama wa chama hicho kwamba misaada hiyo iliyotolewa na mbunge huyo siyo rushwa bali anatekeleza ilani ya chama tawala.


“Kwa sababu mbunge aliyepo madarakani anayoyafanya siyo rushwa,niombe kutoa wito kwa viongozi wengine mliopo madarakani,msipate kigugumizi, msisite, kukisaidia chama kijipange kujiandaa kwenda kwenye mchakato,mama Mlata kila la kheri”alisisitiza huku akishangiliwa na wajumbe waliohudhuriaa kikao hicho.

No comments:

Post a Comment