Monday, July 6, 2015

CUF yatangaza kuuvunja muungano wa Ukawa Ikungi.

Mwenyekiti wa CUF Wilaya ya Ikungi na ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza kuu la uongozi Taifa,Bwana Athumani Henku akizungumza na mwandishi wa habari hizi.

CHAMA Cha Wananchi (CUF) Wilaya ya Ikungi,Mkoani Singida kimesema kitaandika barua kwenda CUF Makao makuu kuomba kuvunja masharti  kwenye wilaya ya Ikungi,Mkoani Singida yaliyofikiwa katika kikao cha pamoja cha vyama vilivyopo kwenye umoja wa Ukawa kuhusu kuachiana majimbo ya uchaguzi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ubabe wanaofanyiwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo( CHADEMA).

Mwenyekiti wa CUF wilaya ya Ikungi,Athumani Henku alisema CUF wilaya ya Ikungi haipingani kabisa na masharti yaliyofikiwa kwenye kikao hicho cha pamoja na inaunga mkono kwa asilimia mia moja masharti hayo yatekelezwe kwenye wilaya zote za Tanzania,isipokuwa wilayani Ikungi peke yake.

Mwenyekiti huyo alitoa kauli hiyo alipokuwa akielezea masikitiko yake juu ya ubabe,dharau na manyanyaso wanayofanyiwa na Chama Cha

Kaimu RC Singida, Alli Kamanzi, aaga vijana 279 wanaokwenda kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa.

Kaimu mkuu wa mkoa wa Singida, Alli Kamanzi, akitoa nasaha zake za kuwaaga vijana 279 waliochaguliwa kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) katika kambi mbalimbali nchini. Kushoto ni Mwenyekiti wa kikosi cha JWTZ kanda ya kati, meja Kakwayu.

Makala ya kuongeza uzalishaji mazao ya Nyuki kwa kutumia mizinga ya kisasa na kuondokana na mizinga ya asili katika mkoa wa Singida.

HALMASHAURI ya wilaya ya Singida ina ukubwa wa kilomita za mraba 3,787 ambazo wananchi wake hujishughulisha na kilimo na ufugaji.
Mazao ya chakula na biashara yanayolimwa na wananchi hao ni pamoja na mtama,uwele,alzeti,vitunguu na dengu na zao la kipaumbele ni asali kwa ajili ya chakula na biashara.
Halmashauri ya wilaya ya Singida ina maeneo mapana ya ufugaji nyuki ikiwemo misitu ya watu binafsi na misitu ya ardhi ya Kijiji ukiwemo msitu wa Hifadhi wa Mgori,ambapo jumla ya hekta za misitu 55,000 zinatumika katika shughuli za ufugaji nyuki.
Katika Makala hii Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Singida,Linus Mtefu anaelezea namna Halmashauri hiyo ilivyojipanga kuongeza uzalishaji wa mazao ya nyuki ili kuondoa umaskini miongoni mwa wananchi wake.
Anasema Halmashauri ya wilaya ya Singida ina jumla ya

Makala ya madhara yatokanayo na matumizi ya Tumbaku.

Ni Tumbaku ambayo imeshakaguliwa na wataalamu wa kilimo kutoka Bodi ya Tumbaku Tanzania ikikaguliwa na mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa soko la Tumbaku kwa kuanza kununuliwa na makampuni yanayonunua zao hilo.

TUMBAKU ni zao pekee lenye madhara mengi ya kiafya kwa wakulima na wateja wake ambao nusu yao hupoteza maisha duniani kila baada ya sekunde nane,ambapo mtu hufariki kutokana na matumizi ya tumbaku.

Watu wanaotumia tumbaku katika umri mdogo vile vile hufariki mapema sana kabla ya kufikia umri wa miaka 25 na kwamba matumizi hayo ya tumbaku husababisha vifo milioni sita duniani kila mwaka.

Kwa mujibu wa taarifa za wataalamu wa magonjwa yatokanayo ya tumbaku nusu ya vifo vitokanavyo na uvutaji wa sigara ni kwa watu wenye umri wa kati ya miaka 30 hadi 69

Aidha uvutaji wa sigara duniani kote unachangia asilimia 12 ya vifo vyote katika nchi zinazoendelea,na kwamba wanaume ndiyo wanaokufa zaidi kutokana na uvutaji wa sigara.

Idadi kamili ya wavutaji wa sigara Tanzania haijulikani lakini ni ukweli usiopingika kwamba watu wanaoishi kwenye maeneo ya vijijini wanavuta zaidi kuliko waishio kwenye maeneo ya mijini.

ATHARI ZA TUMBAKU KIAFYA:

Athari zinazotokana na matumizi hayo ya tumbaku kiafya ni pamoja na ugonjwa wa