Thursday, October 8, 2015

MO atua Singida kushiriki mkutano wa kampeni za Urais.

Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Singida mjini, Mohammed Dewji akisalimiana na mmoja wa madiwani waliofika kumpokea mara tu baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Singida mjini pamoja na wasaidizi wake.
Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Singida mjini, Mohammed Dewji akiwa ameambatana na Mgombea Ubunge wa jimbo la Bumbuli, January Makamba ambaye pia ni mmoja wa wanakamati wa timu ya ushindi ya kampeni za Mgombea urais kupitia tiketi ya CCM, Dk.John Pombe Magufuli, wakielekea sehemu ya mapokezi mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege Singida mjini.
Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Singida mjini, Mohammed Dewji akilakiwa kwa furaha na watoto wanaoishi kwenye eneo la uwanja wa ndege Singida mjini.

Watoto wakimpokea kwa shangwe aliyekuwa Mbunge wao jimbo la Singida mjini, Mohammed Dewji mara tu baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege Singida mjini kwa ajili ya kuhudhuria kampeni za Mgombea urais kupitia tiketi ya CCM, Dk.John Pombe Magufuli pamoja na kumuombea kura kwa wana Singida.

 Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Singida mjini, Mohammed Dewji akiagana na Mgombea Ubunge wa jimbo la Bumbuli ambaye pia ni mmoja wa wanakamati wa timu ya ushindi ya kampeni za Dkt. Magufuli, January Makamba kabla ya kuelekea kwenye viwanja vya Peoples Singida mjini ulipofanyika mkutano wa kampeni za Mgombea urais kupitia tiketi ya CCM, Dk.John Pombe Magufuli. Kulia ni Msaidizi wa MO, Duda Jumanne.
Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Singida mjini, Mohammed Dewji akipata picha ya ukumbusho na wanaSingida wanaoishi karibu na maeneo ya uwanja wa ndege wa Singida mjini.

No comments:

Post a Comment