Sunday, June 28, 2015

January Makamba adhaminiwa na wanaCCM 8,300 mkoani Singida.

Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba, akipokewa na baadhi ya wanaCCM na wananchi wa mkoa wa Singida jana (26/6/2015) akiwa kwenye harakati zake za kusaka wadhamini ili aweze kuteuliwa na CCM kupeperusha bendera ya CCM kwenye nafasi ya urais kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba, akiwashukuru wanaCCM 8,300 wa mkoa wa Singida, waliomdhamini ili aweze kuteuliwa kupeperusha bendera ya CCM kwenye nafasi ya urais kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Baadhi ya wana CCM na wananchi wa mkoa wa Singida,wakimsikiliza Naibu waziri wa mawasiliano,sayansi na teknolojia,Januari Makamba,wakati akiwashukru wana CCM 8,300 waliomdhamini ili CCM iweze kumteua kugombea nafasi ya urais kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

WaterAid Tanzania, Singpress kushirikiana mradi wa Mwanzo mwema

Mwakilishi wa shirika la WaterAid Tanzania, Ibrahimu Kabole, akitoa ufafanuzi juu ya mradi wa ‘Mwanzo Mwema’ (A Good Start) ambao pamoja na mambo mengine, utashughulikia afya ya uzazi kwa akina mama wajawazito. Mradi huo unafadhiliwa na serikali ya Sweden.Kulia ni balozi wa Sweden hapa nchini, Lennarth Hjelmaker.

SHIRIKA lisilo la kiserikali la WaterAid Tanzania,limeahidi kushirikiana na klabu ya waandishi wa habari (Singpress) mkoa wa Singida, kwenye utekelezaji wa mradi wa ‘Mwanzo mwema’ (A Good Start) unaodhaminiwa na serikali ya Sweden kupitia shirika la Riksfӧbundet FӧR Sexual Upplysning (RFSU).

Ahadi hiyo imetolewa na Mwakilishi wa shirika la WaterAid Tanzania Dk.Ibrahimu Kabole,muda mfupi baada ya mradi wa Mwnzao Mwema utakaogharamu zaidi ya shilingi 1.4 biloni,kuzinduliwa rasmi mjini hapa na balozi wa Sweden nchini Lennarth Hjelmaker.

Alisema mradi wa Mwanzo Mwema utakaotekelezwa kwa kipindi cha miaka mitatu katika halmashauri ya wilaya ya Iramba na manispaa ya Singida,lengo lake ni pamoja na kutoa elimu juu ya uzazi wa mpango,haki za binadamu na mambo yanayoambatana na uzazi.

Dk.Kabole alisema pia

Sungusungu watuhumiwa kuua vijana watatu

Kamanda wa Jeshi la polisi mkoani Singida, ACP Thobias Sedoyeka akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.

VIJANA watatu wakulima na wakazi wa kijiji cha Udimaa wilayani Manyoni mkoani Singida,wamefariki dunia baada ya kupewa kipigo kikali na askari Sungusungu na wananchi wenye hasira kali, kwa tuhuma ya kuvamia duka la mfanyabiashara Robert Francis (23) na kisha kumpora shilingi 1,500,000 taslimu.

Vijana hao ni Mosi Emmanuel (31), Mbasha Mhembano (27) na Mosi Mashauri (31) na wamefariki dunia wakati wakipatiwa matibabu katika hospitali ya wilaya ya Manyoni.

Kamanda wa Jeshi la polisi mkoani Singida, ACP Thobias Sedoyeka, alisema tukio hilo limetokea juni 17 mwaka huu saa nane usiku huko katika kijiji cha Udimaa  wilaya ya Manyoni.

Alisema mfanyabiashara Robert siku ya tukio alivamiwa na vijana hao wanaodhaniwa kuwa ni

Monday, June 22, 2015

Waswidi watoa bilioni 1.4 kugharamia mradi wa Mwanzo mwema.

Balozi wa Sweden nchini,  Mh. Lennarth Hjelmaker, akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa mradi wa ‘Mwanzo Mwema’ (A Good Start) unaofadhiliwa na nchi yake kwa zaidi ya shilingi bilioni 1.4.Pamoja na mambo mengine, balozi huyo ameahidi nchi yake itaendelea kushirikana na Tanzania katika kuboresha sekta mbalimbali ikiwemo ya afya.
Mwakilishi wa shirika la WaterAid Tanzania, Ibrahimu Kabole, akitoa ufafanuzi juu ya mradi wa ‘Mwanzo Mwema’ (A Good Start) ambao pamoja na mambo mengine,utashughulikia afya ya uzazi kwa akina mama wajawazito.Mradi huo unafadhiliwa na serikali ya Sweden. Kulia ni Balozi wa Sweden nchini, Mh. Lennarth Hjelmaker.
Baadhi ya wadau wa afya mkoani Singida, waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa mradi wa ‘Mwanzo Mwema’ (A Good Start) unaofadhiliwa na nchi ya Sweden kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 1.4.

Saturday, June 20, 2015

Halmashauri ya wilaya ya Singida yatoa chanjo ya Vitamin “A” kwa watoto 39,166

Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari za tarafa ya Mtinko wakiwa kwenye na mabango yenye ujumbe wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika iliyofanyika kiwilaya kata ya Ughandi, Singida vijijini.

Vikundi vya ngoma vilivyokuwa vikitumbuiza kwenye sherehe za siku ya mtoto wa Afrika.

Waziri Membe azoa wadhamini zaidi ya 1900 Mkoani Singida.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (kulia) akiusalimia umati wa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wa Mkoa wa Singida, waliofika katika Ofisi ya CCM ya Mkoa huo Juni 18.2015, kwa ajili ya kumdhamini iliaweze kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, ambapo aliweza kupata wadhamini zaidi ya 1,900. Kushoto ni Katibu wa CCM wilaya ya Ikungi, Aluu Segamba.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (kulia) akizungumza na umati wa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), na wananchi  wa Mkoa wa Singida, waliofika katika Ofisi ya CCM ya Mkoa huo Juni 18.2015, kwa ajili ya kumdhamini iliaweze kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, ambapo aliweza kupata wadhamini zaidi ya 1,900.

Ajali yaua sita na kujeruhi wengine 40 Singida.

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kuchukua fomu za kugombea urais.
Dereva wa lori kubwa RAC 317 N raia wa Uganda,Waguuma Mohammed, akizungumzia ajali ya lori lake kugongwa kwa nyuma na basi T.174 CAV mali ya Enock Mwita wa jijini Mwanza.
Mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Singida, Dk.Daniel Tarimo, akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya ajali mbili tofauti ikiwemo ya basi ambazo zimeuawa abiria sita na kujeruhi abiria wengine 44.

Friday, June 19, 2015

Waziri Nyalandu atangaza nia na kuchukua fomu, asema uwekezaji kwenye rasilimali umma ni muhimu.

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu na mkewe Bi.Faraja Nyalandu wakiingia uwanja wa Namfua Mjini Singida kabla ya kuhutubia wananchi kwa kutangaza nia ya kugombea Urais.

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM Wilaya wa Singida, Barnabas Hanje kabla kutangaza nia ya kugombea urais wa Tanzania kwenye mkutano uliofanyika uwanja wa Namfua Mjini Singida.
Bi. Faraja Nyalandu akiongea na wananchi kabla ya hotuba ya mumewe Mhe. Lazaro Nyalandu ya kutangaza nia ya kugombea  urais wa Tanzania.

Wednesday, June 3, 2015

Halmashauri ya Manispaa Singida yapewa msaada wa zaidi ya Mil 250 kwa ajili ya malori ya taka ngumu.

Kijiko mali ya manispaa ya Singida kilichonunuliwa kwa shilingi 110 milioni,kikipakia taka ngumu kutoka kwenye dampo la soko la vitunguu mjini hapa jana.
Malori mawili mapya mali ya manispaa ya Singida yaliyotolewa na serikali kuu kwa ajili ya kuzoa taka ngumu. Thamani ya malori hayo ni zaidi ya shilingi milioni 140. Na chini picha ya kijiko hicho .
Serikali kuu imeipatia msaada  halmashauri ya manispaa ya Singida, kijiko na malori mawili makubwa vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi 250 milioni,kwa ajili ya uzoaji wa taka ngumu.

Hayo yamesemwa juzi  na mkurugenzi wa manispaa ya Singida, Joseph Mchina, wakati akizingumza na waandishi wa habari juu msaada huo ambao utasaidia kwa kiwango kikubwa kuboresha hali ya usafi katika mji wa Singida,na  pia zitapunguza gharama kubwa ya uzoaji taka ngumu.

Alisema malori hayo mawili ya tani 20 kila moja, thamani yake ni shilingi 70 milioni kila moja na kijiko ni shilingi 110 milioni.

 “Kwa mwezi tulikuwa tunatumia zaidi ya shilingi

Wakazi wa manispaa ya Singida walalamikia uongozi kushindwa kuzoa taka ngumu.

Baadhi ya maghuba yaliyopo katika Manispaa ya Singida yakiwa yamefurika taka ngumu kwa muda mrefu sasa kama ambavyo Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Bwana Joseph Mchina alivyokiri katika maelezo yake kushindwa kuzoa kutokana na magari ya kuzolea taka kuchelewa kufika.
WAKAZI wa Halmashauri ya Manispaa ya Singida wameulalakia uongozi wa Manispaa hiyo kwa kushindwa kuzoa taka kwenye maghuba ya kukusanyia taka ngumu zinazokusanywa na wananchi wa mji wa Singida,licha ya wananchi hao kutozwa ushuru wa shilingi elfu tano kwa kila mwezi kwa ajili ya uzoaji wa taka hizo ngumu.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi hao,Abdallah Daudi Kibiriti,Mwandoghwe Gwao na Avi Mohamedi walifafanua kuwa uongozi wa Manispaa hiyo,akiwemo mkurugenzi kwa kushirikiana na madiwani waliokabidhiwa dhamana ya kusimamia maendeleo kwenye maeneo yao,lakini maslahi zaidi yamewekwa katika kulipana posho za vikao na safari za mara kwa mara za mkurugenzi huyo.

Walifafanua wananchi hao kwamba kutokana na kuwepo kwa hali hiyo,ni wakati wowote ule