Friday, September 18, 2015

Zaidi ya wakazi 5,000 hatarini kukumbwa na magonjwa ya mlipuko.

Kaimu Katibu Tawala wa mkoa wa Singida, Aziza Mumba akikata utepe kuzindua nyota mpya ya kijani.
Baadhi ya wananchi wa kata ya Mang’onyi wakiwa kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mkuu kumnadi mgombea wa ubunge wa jimbo hilo.

ZAIDI ya wakazi 5,000 wa Kijiji cha Sambaru,kata ya Mang’onyi,wilaya ya Ikungi,Mkoani Singida wamo hatarini kupatwa na magonjwa ya mlipuko kutokana na kujisaidia vichakani kwa kutokuwa na vyoo vya kudumu kutokana na idadi kubwa ya wahamiaji wanaoishi kwenye vitongoji saba vilivyopo katika Kijiji hicho.

Ofisa mtendaji wa Kijiji cha Sambaru,Bwana Baraka Njiku amesema wakazi hao wapo kwenye hatari ya kukumbwa na magonjwa ya kuharisha,kuhara damu pamoja na kipindupindu kutokana na kula uchafu wa kinyesi wanachojisaidia kwenye vichaka vilivyopo karibu na nyumba zao za makazi.

Aidha ofisa mtendaji huyo amefafanua kwamba  wakazi hao wapatao 5,870 wanaoishi katika kaya 899 wanahitaji matundu 899,lakini matundu ya vyoo vya muda yaliyopo ni 320 kati ya mahitaji wa wakazi wote wa Kijiji hicho.

Kwa mujibu wa Bwana Njiku katika Kitongoji cha Taru namba saba chenye kaya 99 kinahitaji jumla ya matundu ya vyoo 498 yaliyopo kwa sasa ni matundu ya muda

Uzazi wa mpango utekelezwe na familia kwa vitendo, ili kustawi vyema na kuimarika kiuchumi

Kaimu Katibu Tawala wa mkoa wa Singida, Aziza Mumba akikata utepe kuzindua nyota mpya ya kijani.
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Aziza Mumba akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Singida wakati wa uzinduzi wa kampeni mpya ya nyota ya kijani kwenye viwanja vya peoples Mjini Singida.
 Kaimu Mganga mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Mussa Kimala akizungumza kwenye sherehe hizo.

Thursday, September 17, 2015

Tundu Lissu amshukia Dk.Slaa kwa madai ya kuponzwa na mkewe.

Mwanasheria wa CHADEMA na mgombea ubunge jimbo la Singida mashariki, Tundu Lissu,akizungumza kwenye mkutano wa kampeni ya Ukawa mkoa wa Singida uliofanyika kwenye uwanja wa Peoples mjini hapa.Pamoja na mambo mengine,Tundu amewaomba wakazi wa Singida, kumpa kura ya ndiyo mgombea urais kwa tiketi ya Ukawa, Edward Ngoyai Lowassa, wabunge na madiwani wa Ukawa,ili kuigaragaza CCM kwa madai imechoka na umechuja mbele ya macho ya Watanzania.

Mgombea ubunge jimbo la Singida mjini kupitia ukawa, Mgana Izumbe Msindai, akiomba kura kwenye mkutano wa kampeni wa Ukawa uliofanyika kwenye uwanja wa Peoples mjini hapa. Msindai ambaye amewahi kuwa mbunge wa jimbo la Iramba mashariki kwa vipindi vitatu mfululizo na mwenyekiti wa wenyeviti wa CCM wa mikoa nchini,amewata wakazi wa jimbo la Singida mjini kujitokeza kwa wingi oktoba 25 mwaka huu kuichana chana CCM kwa kadi zao za kupigia kura.

Hospitali ya Mkoa Singida yapigwa tafu ya mashuka na benki ya Posta nchini.

Meneja wa benki ya Posta tawi la Singida, Redenoter Rweyemamu, akizungumza kwenye hafla ya benki hiyo kutoa msaada wa shuka 104 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni mbili, kwa hospitali ya mkoa mjini hapa, inayokabiliwa na uhaba wa shuka na kusababisha wagonjwa kutumia mashuka yao binafsi kitendo ambacho ni kinyume na taratibu.
Mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa mjini hapa, Dk. Daniel Tarimo, akitoa shukrani zake kwa benki ya posta tawi la Singida mjini kwa msaada wake wa mashuka kwa hospitali hiyo.Dk.Tarimo amedai kuwa bado hospitali hiyo inaupungufu wa shuka 2,000 na magodoro 236.
Meneja wa benki ya Posta tawi la Singida mjini (katikati),akimkabidhi Mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa mjini hapa, Dk.Daniel Tarimo mashuka 104. Mashuka hayo yamepunguza makali ya uhaba mkubwa wa shuka na sasa, kuna upungufu wa shuka 2,000 na magodoro 236.

BENKI  ya Posta Tawi la Singida Mjni, imetoa msaada wa shuka 104 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni mbili kwa hospitali ya mkoa ya mjini hapa, ili kupunguza uhaba mkubwa unaoikabili hospitali hiyo.

Akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi msaada huo, Redempter Rywemamu, alisema hatua hiyo imechukuliwa  na benki ya posta,ikiwa ni  ni kuitikia  wito uliotolewa na

Taasisi za fedha ziwezeshe wajasiriamali wadogo.

Mkuu wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Kone, akikagua vyungu vilivyotengenezwa na wajasiriamali wa wilaya ya Iramba ambao wanashiriki maonesho ya 12 ya SIDO kanda ya kati yanayoendelea mjini Singida.
Afisa Mwanadaamizi wa Masoko wa Shirika la viwango (TBS), Gladness Kaseka (kushoto) akimpa maelezo Mkuu wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Kone, juu ya shughuli zinazofanywa na shirika hilo. Dk.Kone alikuwa akikagua mabanda ya wajasiriamali na taasisi mbalimbali wanaoshiriki maonesho ya bidhaa mbalimbali yaliyoandaliwa na SIDO kanda ya kati yanayoendelea mjini Singida.
Mkuu wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Kone, akionyesha kupendezwa na mkuki uliotengenezwa na wahunzi wa kijiji cha Kisonga wilaya ya Iramba wanaoshiriki maonesho ya SIDO kanda ya kati yanayoendelea mjini Singida.

Kaimu Msimamizi wa uchaguzi Singida mjini atupilia mbali pingamizi la CHADEMA dhidi ya mgombea wa CCM

Kaimu msimamizi wa uchaguzi jimbo la Singida mjini, Gerald Muhabuki Zephyrin,akizungumza na SingidaYetu Blog juu ya uchaguzi ubunge jimbo la 
Singida mjini.

PINGAMIZI lililowekwa na Chama Cha Maendeleo na Demokrasia (CHADEMA),jimbo la Singida mjini, dhidi ya mgombea wa CCM Mussa Ramadhan Sima kuwa

Maonyesho ya SIDO kwa wajasiriamali kwa kanda ya kati kufanyika Agosti 26 hadi Septemba Mosi mwaka huu Mkoani Singida.

Mkuu wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Vicent Kone, akitoa taarifa kwa waandishi wa habari  juu  ya kufanyika kwa maonesho ya SIDO kanda ya kati kuanzia Agosti 26 hadi septemba mosi mwaka huu mjini Singida. SIDO kanda ya kati inajumuisha mikoa ya Singida, Tabora na Kigoma.Katika maonesho hayo, bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na wajasiriamali na wafanyabiashara ndogo.

Waandishi wa habari watakiwa kutumia kalamu zao kudhibiti madereva waenda kasi na mabasi nchini.

Mkuu wa Kitengo cha usalama barabarani Wilaya ya Singida (DTO), Antony Sempanga akimwonesha Mwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani Mkoa wa Singida Akhlan Ghalib,kifaa cha kisasa cha kupima mwendo kasi (speed radar) wakati wa akitoa taarifa juu ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani Mkoa wa Singida kwa waandishi wa habari (hawapo pichani).
Mkuu wa Kitengo cha usalama barabarani Wilaya ya Singida (DTO), Antony Sempanga akiwaonesha waandishi wa habari jinsi speed radar ya kisasa inavyofanya kazi.
 Antony akiwa na kifaa cha kupima mwendo kasi.
Antony akionesha waandishi wa habari nama ya kupokea sms kwa njia ya mtandao kutoka kwenye speed radar kwenda kwenye simu ya mkononi.

Hillary Shoo wa Jambo Leo Singida, anyakua cheti maalumu kwa uandishi bora wa habari za Usalama Barabarani mkoa wa Singida.

Mwandishi wa habari wa Gazeti la Jamboleo Mkoa wa Singida, Hillary Shoo,akipokea cheti maalumu kutoka kwa Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Singida, Aziza Mumba ikiwa ni mchango wake mkubwa katika kuandika habari za kuelimisha jamii juu ya wiki ya nenda kwa usalama barabara Mkoa wa Singida, halfa hiyo ilifanyika jana kwenye viwanja vya kituo cha mabasi yaendeyo mikoani, kulia ni Kamanda wa polisi Mkoani humo Thobias Sedoyeka.

Serikali kuboresha zaidi mazingira ya kufanyia shughuli za wajasiriamali mkoani Singida.

Meneja mradi wa kuwajengea uwezo wafanyabiashara wadogo,Florentina Sallah, akitoa nasaha zake kwenye ufunguzi wa mafunzo ya siku tano yanayohudhuriwa na wafanyabiashara wadogo 150 wa mkoa wa Singida.Wa kwanza kulia ni Mkuu wa mkoa wa Singida,D k.Parseko Kone na anayefuatia ni,Dk.Willhelm Ngasamiaku,mhadhiri wa uchumi idara ya uchumi chuo kikuu cha Dar-es-salaam.
Mkuu wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Kone,akizungumza kwenye uzinduzi wa mafunzo ya siku tano yanayohudhuiwa na wafanyabiashara wadogo 150 yanayoendelea kwenye ukumbi wa mikutano wa chuo cha maendeleo ya wananchi mjini hapa. Dk.Kone ameahidi kuwa serikali mkoani hapa itaendelea kuwajengea mazingira mazuri wafanyabiashara hao, ili shughuli zao ziwe za tija zaidi.
Mhadhiri wa uchumi idara ya uchumi chuo kikuu cha Dar-es-salaam, Dk.Wilhelm Ngasamiaku,akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa mafunzo ya wafanyabiashara wadogo 150 wa mkoa wa Singida yanayoendelea kwenye chuo cha maendeleo ya wananchi mjini hapa.Wa pili kulia ni mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Kone na wa kwanza kulia ni mkuu wa wilaya ya Singida,Iddi Amanzi. Kushoto ni Meneja mradi wa kuwajengea uwezo wafanyabiashara wadogo,Florentina Sallah.

Mwanafunzi atumia bastola ya mama kutaka kujiua.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida, ACP Thobias Sedoyeka, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) ofisini kwake.

MWANAFUNZI wa darasa la sita katika shule ya msingi Abelt, Singida mjini Stanley Markdonard (13), amenusurika kufa katika jaribio lake la kutaka kujiuawa kwa kujipiga risasi mbili tumboni kwa kutumia bunduki aina ya bastola, mali ya mama yake mkubwa, Joyce Mark Minde.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida, ACP Thobias Sedoyeka, alisema tukio hilo lisilo la kawaida limetokea Agosti tatu mwaka huu majira ya mchana huko katika mtaa wa Saba Saba kata ya Mandewa manispaa ya Singida.

Alisema siku ya tukio,Stanley alivizia mama yake mkubwa akiwa kazini aliweza kuvunja mlango wa kabati na kuchukua silaha hiyo aina ya browning 7.65 MM mark No.B.097046,na kujipiga risasi mbili tumboni.

Alisema Stanley amelazwa katika hospital ya misheni ya St.Gasper Itigi wilaya ya Manyoni, na hali yake ni mbaya. Chanzo cha tukio hilo