Afisa mtendaji wa kata ya Iguguno Josia Pangani akizungumzia tukio la kulawitiwa na kisha kunyongwa hadi kufa wanafunzi wawili wa familia moja wa shule ya msingi Lukomo wilaya ya Mkalama.
Mama mzazi wa watoto waliobakwa na kisha kunyongwa hadi kufa Veronica Nuru mkazi wa kijiji cha Lukomo wilaya ya Mkalama, akizungumzia tukio la kuuawa kikatili watoto wake.
Makaburi walikozikwa wanafunzi wawili waliolawitiwa na kisha kunyongwa hadi kufa.
Watoto wawili wa familia moja wameuawa kikatili mkoani Singida baada ya kulawitiwa na watu wasiojulikana, kisha kunyongwa kabla ya milii yao kwenda kufungwa kwenye mti porini.
Watoto hao wametajwa kuwa ni Esta Daudi (14) na Anita Shila (9) wote wanafunzi wa darasa la saba na tatu katika shule ya msingi Lukomo kata ya Iguguno wilaya ya Mkalama mkoani Singida.
Afisa mtendaji wa kata hiyo Josia Pangani, amesema tukio hilo limetokea majira ya saa 12 jioni wakati watoto hao wa kike wakiwa wanachunga mifugo kwenye pori jirani na nyumbani kwao.
Pangani amesema baada ya muda wa kurejesha mifugo zizini kufika, wazazi wa watoto hao walishangaa kutowaona watoto wala mifugo, hali iliyosababisha kuanza juhudi za kuwatafuta.
Amesema juhudi hizo hazikuweza kuzaa matunda siku hiyo hadi kesho yake walipoikuta miili ya watoto hao ikiwa imefungwa kwenye mti.
Baada ya uchunguzi wa kitaalamu kufanyika, ilibainika kuwa walibakwa, kunyongwa shingo, kisha kufungwa vitambaa usoni na watu wasiojulikana.
Habari za kipolisi zinasema kuwa watu wawili akiwemo baba mzazi wa watoto waliouawa