Wednesday, November 28, 2012

HIKI NDIO CHANZO CHA AJALI YA SHARO MILLIONEA.

                     Gari alilolua akiendesha Sharo Millionea likionekana kwa upande wa mbele
                            Gari alilolua akiendesha Sharo Millionea likionekana kwa upande wa nyuma

Kwa mujibu wa taarifa toka jeshi la polisi na mashuhuda wa ajali ya msanii Sharo Millionea,Inasemekana marehemu alikua akiendesha gari kwa kasi na ghafla
tairi la mbele upande wa kulia lili basti,hali iliyomfanya ashindwe kulimudu gari na kutoka nje ya barabara.

Alitembea njee ya barabara kwa muda kidogo na alivamia baadhi ya mimea kama vile mahindi yaliokua kando kando ya barabara hiyo ya Maguzoni songa,Muheza.

Gari liliendelea kwenda kwa kasi na kwenda kugonga mtaro,hali iliolifanya gari hilo aina ya Toyota Harrier kuruka na kwenda kukonga mti ulikua pembezoni mwa barabara hiyo na kuugawanya mti huo katikati ambapo upande wa juu wa mti huo ulienda kudondokea mbele na upande wa chini wa mti huo uling'olewa toka kwenye shina.Baadaya ya kugonga mti huo gari la Shalo Millionea lilipinduka mara kadhaa hali ilioifanya gari hili kuharibika vibaya.
 Inaaminika mti huu ndio sababisha Sharo Millionea kupoteza maisha.

More to follow...

No comments:

Post a Comment