Mkuu wa wilaya ya Singida Mwalimu Queen Mlozi akizindua upandaji miti katika kijiji cha Kitope manispaa ya Singida.
Mtoto Juma Sungi wa darasa la tatu katika shule ya msingi ya Mwankoko manispaa ya Singida akishiriki kampeni ya kupanda miti kwa lengo la kunusuru manispaa hiyo isigeuke jangwa.
Mkuu wa wilaya ya Singida mwalimu Queen Mlozi akionyesha miche ya miti maji ambayo amedai kuwa inatumika kuvuna mbao na pia kutengenezea sabuni.
Mkuu
wa wilaya ya Singida mwalimu Queen Mlozi akishiriki kampeni ya kupanda
miti ili kuokoa wilaya hiyo isikumbwe na balaa la Jangwa.
Mtoto Juma Sungi wa darasa la tatu katika shule ya msingi ya Mwankoko manispaa ya Singida akishiriki kampeni ya kupanda miti kwa lengo la kunusuru manispaa hiyo isigeuke jangwa.
Mkuu wa wilaya ya Singida mwalimu Queen Mlozi akionyesha miche ya miti maji ambayo amedai kuwa inatumika kuvuna mbao na pia kutengenezea sabuni.
Serikali
wilayani Singida imepiga marufuku mara moja uvunaji ovyo wa misitu, kwa
madai kwamba uvunaji wa aina hiyo, unatishia
wilaya hiyo kugeuka
jangwa.
Mkuu
wa wilaya hiyo mwalimu Queen Mlozi, ametoa agizo hilo la kupiga
marufuku, wakati akizindua awamu ya pili ya kampeni ya vita dhidi ya
jangwa katika wilaya hiyo.
Amesema
kumekuwa na uvunaji wa ovyo wa msitu usiokuwa na uwiano na upandaji wa
misitu, unachochewa kwa kiasi kikubwa na biashara ya mkaa.
Mlozi
amesema hivi sasa kuna malori mengi kutoka wilaya ya Arusha na Manyara,
ambayo yanasafirisha mamia kwa mamia ya magunia ya mkaa kutoka Wilaya
ya Singida, biashara ambayo inataka kuacha wilaya yetu kuwa jangwa,
haikubaliki na hatutaki iendelee ni lazima tuikomeshe.
Mkuu
huyo wa wilaya amesema kuanzia sasa, vizuizi viwekwe kwenye sehemu
husika ili kuyakamata malori hayo ya mkaa na wahusika wachukuliwe hatua
kali za kisheria.
Awali
Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi ya Ant desert environment scheme Kitanto
Said, alisema katika awamu hii ya pili ya kampeni dhidi ya jangwa,
wanatarajia kupanda miti zaidi ya elfu moja.
No comments:
Post a Comment