Wednesday, August 28, 2013

HISTORIA MPYA YAANDIKWA, CHIDY BENZ NA NEY WA MITEGO WAPATANISHWA MKOANI SINGIDA.

Yeyote ambae damu yake ipo sana kwenye muziki wa bongofleva ni lazima atakua anafahamu kuhusu ugomvi wa muda mrefu, kutoelewana kwa Chidi Benz na Ney wa Mitego, ishu ambayo ilihusishwa hata kwenye nyimbo zao.
Shuhuda mkuu wa tukio lenyewe ni msanii Madee ambae naanza kwa kumkariri anasema ‘hizi ndio faida za Serengeti Fiesta, kujuana na kukutana na watu wengi, hiki ni kitu ambacho nilikipanga mimi… watu wanafikiria tu sisi tunakwenda kule kufanya muziki, mbali na pesa tunazolipwa vizuri sasa hivi kwenye Fiesta, kuna faida nyingine pia, niliposikia Chidi Benz yupo kwenye Fiesta nilijipanga lazima nifanye hivi manake Chidi na Ney wote nawajua, nimekaa nao’
Kwenye sentensi ya pili, Madee anasema ‘niligundua Chidi ni mwepesi kukasirika, kuna wakati kwenye basi la Wasanii kulitokea kama purukushani kuhusu hawa wawili so nikasubiri tu time nzuri ifike nifanye yangu’
‘Tulikua Club, nilipoona Chidi katulia nikamfata, nikamchukua alafu bila kumwambia kitu nikampeleka alipokuwepo Ney wa Mitego, nikamwambia haya…. simama pale nikupige picha, wakati huo sijasema chochote kuhusu ugomvi na Shilole alikua ndio kasimama na Ney, nikawapiga wakiwa watatu alafu badae nikamwambia Shilole aondoke wakabaki wawili, yani Ney na Chidi’ – Madee
Madee anakwambia baada ya kupiga picha hazikuongelewa stori zozote za ugomvi wa Chidi na Ney, kwanza zilipigwa stori za mtaani tu… za ujana alafu kitu kikaitika manake Ney wa Mitego na Chidi Benz wote walikua na furaha na walikua wanachangia mada kwa pamoja, yani kama washkaji….
Hii ishu ilitokea wakati wa show ya Serengeti Fiesta 2013 Singida ambapo kikubwa alichokua anaongea Chidi ni kuhusu
 Ney kumuimba vibaya kwenye nyimbo zake lakini Ney aliweka wazi kwamba nia yake sio mbaya na wala anachokitaka sio ugomvi bali ni aina ya muziki wake, kwa mujibu wamaelezo ya Madee.
Kingine anachosema Madee ni ‘Ney ndio aina ya muziki wake, hawezi kung’aa mpaka amtaje mtu kwenye nyimbo zake na hiyo ni bishara yake, lakini anavyofanya hivyo sio kwamba anataka ugomvi, ni mtu muelewa na wala sio mtu wa aina hiyo ya ugomviugomvi, baada ya kuwapatanisha wakashikana mikono, tukawaambia wabadilishane namba za simu alafu bata likaendelea… so sasa hivi kila kitu ni fresh’
Kama ulikua hujui, Ney wa Mitego alishawahi kuwa na ugomvi na Madee zaidi ya miaka 10 iliyopita ambapo mama mzazi wa Madee aliwahi kupigwa chupa ya uso mpaka leo anayo alama usoni wakati akiamulia ugomvi wa Madee na Ney wa Mitego ambae alimfata Madee nyumbani kwao akiwa na wenzake wakitaka kumpiga.

No comments:

Post a Comment