Mmoja wa watoto waliofika katika ofisi za Kijiji cha Maweni kwa ajili ya kuhudhuria Kliniki tembezi kutoka katika Hospitali ya misheni ya Kilimatinde,wilayani Manyoni akipimwa uzito na wahudumu wa afya wa Hospitali hiyo.
Watoto wakisalimiana wakati wakisubiri kupatiwa huduma za chanjo kutoka kwa wataalamu wa afya kutoka katika Hospitali ya misheni ya Kilimatinde,wilayani Manyoni.
Mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Vicent Kone,jana akitoa taarifa kwa waandishi wa habari (hawapo kwenye picha) juu ya kufanyika kwa maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani kitaifa mkoani Singida.
Baadhi ya waandishi wa habari mkoani Singida,wakiwa kwenye harakati za kupata picha bora ya mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Vicent Kone (hayupo kwenye picha) jana.Mkuu huyo wa mkoa,alikuwa akitoa taarifa ya kufanyika kwa maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani itakayofanyika kitaifa mkoani Singida.
Rais mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani, ambayo kitaifa inatarajiwa kufanyika mkoani hapa Desemba mosi mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisni kwake jana,mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Kone,alisema maadhimisho hayo yanatarajiwa kuanza novemba 24 mwaka huu kwenye viwanja vya peoples mjini hapa, na yatazinduliwa rasmi novemba 25.
Alisema katika wiki ya maadhimisho hayo,wadau mbalimbali watapata fursa ya
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, ACP. Thobias Sedoyeka akiongea na waandishi wa habari Mkoani Singida alipokuwa akitoa taarifa za matukio ya mauaji ya watu sita Mkoani hapa.
Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Mukhola, kata ya Mgori wakiwa katika safari ya kumtafuta mtu aliyewauwa wanawake wawili akiwemo mtalaka wake kwa kugombea mashamba.
WATU sita wamefariki dunia na mtu mmoja kujeruhiwa katika matukio manne tofauti yaliyotokea Mkoani Singida kati ya Okt,31 na Nov,01,mwaka huu.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Singida, ACP.Thobias Sedoyeka alifafanua kwamba matukio hayo yalitokea katika Vijiji vya Kintanula, wilayani Manyoni, kata ya Kindai, katika Manispaa ya Singida, Kijiji cha Kinyamwambo, kata ya Merya Singida vijijini na Kijiji cha Kamenyanga, wilayani Manyoni.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na ACP. Sedoyeka zimesema kuwa katika tukio la kwanza lililotokea okt,31,mwaka huu saa 2:30 usiku watu watano wasiofahamika wakiwa na mapanga walivamia
Mratbu wa shirika la Uwezo mkoa wa Singida, Nason W.Nason, akitoa nasaha zake kwenye mafunzo yaliyohusu kufanywa kwa utafiti juu ya taaluma shule za msingi manispaa ya Singida.Wa pili kulia ni Kaimu Afisa Elimu shule za msingi manispaa ya Singida, Samwel Mwaikenda na (wa pili kushoto) ni Mkurugenzi wa YMC mkoa wa Singida, Fidelis Yunde.
Kaimu Afisa Elimu manispaa ya Singida, Samwel Mwaikenda, akizungumza kwenye ufungaji wa mafunzo ya namna bora ya kufanya utafiti wa taaluma katika shule za msingi manispaa ya Singida.Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa shirika la YMC mkoa wa Singida, Fidelis Yunde.
Kaimu Afisa Elimu shule za msingi manispaa ya Singida, Samwel Mwaikenda, akimkabidhi kijana Juma cheti kwa kuhitimu mafunzo juu ya utafiti wa taaluma katika shule za msingi manispaa ya Singida. Mkurugenzi wa shirika la YMC mkoani Singida, Fidelis Yunde (suti nyeusi) na wa kwanza kulia, ni Mratibu wa shirika la Uwezo Nason W.Nason.
Mgombea urais kupitia tiketi ya CCM, Dkt. John Pombe Magufuli akimwaga sifa kwa aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Singida Mjini (Mbunge Mstaafu), Mohamed Dewji baada ya kutumikia vyema na kwa uadilifu kiti chake cha Ubunge jimboni humo wakati wa mkutano wa kampeni za mgombea urais huyo kwa tiketi ya CCM uliofanyika katika viwanja wa Peoples mjini humo.
Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Singida mjini, Mohammed Dewji akisalimiana na mmoja wa madiwani waliofika kumpokea mara tu baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Singida mjini pamoja na wasaidizi wake.
Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Singida mjini, Mohammed Dewji akiwa ameambatana na Mgombea Ubunge wa jimbo la Bumbuli, January Makamba ambaye pia ni mmoja wa wanakamati wa timu ya ushindi ya kampeni za Mgombea urais kupitia tiketi ya CCM, Dk.John Pombe Magufuli, wakielekea sehemu ya mapokezi mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege Singida mjini.
Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Singida mjini, Mohammed Dewji akilakiwa kwa furaha na watoto wanaoishi kwenye eneo la uwanja wa ndege Singida mjini.